Nakubaliana kabisa na mtoa hoja na kutaka hao wanaomzima kinywa eti akaulize mahali pake, tangu lini JF pakawa mahali penu? aulize hapa hapa, na hata mimi nakubaliana na wewe Mbowe hana haki ya kutuamulia wana Chadema, waache mihemuko amkaribishe huyo fisadi wake aone kitakachowakuta, labda kama kura wanapiga wao, umaarufi wa chadema sio wa viongozi ni wa sisi wanachama, ndio sisi tunapigwa mabomu, na kuswekwa rumande kila siku. Hatutaki hayo makapi kama anashida ya chama asubiri baada ya uchaguzi waje kujiunga kama wanachama wakawaida, tutawatengenezea mafunzo maalumu ya kuwafundisha kuwa wanachama wa chama kilichosimama kwa mateso, sisi hatukuingia hapa kwa pilau na kanga, tumekanyaga mbigili na chupa wakae hatutaki ebola huku hatutaki najisi huku wakae huko wamalizane na wezi wenzao wa huo mpango wa Richmond, tunataka wakamatwe kama wakina Mramba na wafikishwe mahakamani na huyo Rostam wao