Sasa ni dhihiri kuwa CHADEMA iko kwenye mikakati mizito ya kumshawishi au kuafikiana na Edward Lowassa ili aweze kuhama CCM na kujiunga CHADEMA na hapo hapo apewe nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Nikiwa kama mshambuzi wa mambo ya siasa humu JF, mtanzania mpenda maendeleo na mpenzi wa CHADEMA jambo hili limenishtua na kunisikitisha sana.
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa na magazeti kadhaa ya leo akisema, Lowassa anakaribishwa CHADEMA na hana tatizo lolote, na hapo hapo baadhi ya wabunge na viongozi wa juu wa CHADEMA wamenukuliwa ama wakiunga mkono ujio au kumumunya maneno kuhusu hilo.
Mpaka sasa sijui, ni nini kimewaingia viongozi wa CHADEMA kuanza kukubali jambo hili. Nini msukumo wao?
Ni nani asiyemjua Lowassa? Huyu ni mwanasiasa mchafu, ambaye amewekeza muda, pesa na watu wake wengi sana katika siasa ili afanikiwe tu kuwa rais wa Tanzania.
CHADEMA bado tu humjajifunza kutokana na makosa? Yuko wapi Samweli Sitta, John Shibuda nk?
Mtaacha lini kusubiri makapi ya CCM ili kuyapokea na kuwapa nafasi za ugombea katika uchaguzi?
Hivi mnajua kwanini watanzania wengi waliwapenda na kuwaamini?
Hivi agenda ya kupambana na Ufisadi hamhitaki tena?
Hivi viongozi wa CHADEMA mnatambua siasa itaendelea tu hata baada ya October 25?
Hivi mnajua kwanini watanzania walitoa maisha yao hata kufa kuona CHADEMA inasonga mbele?
Inakuwaje muwe na mawazo ya kupata madaraka tu kiujanjaujanja kwa kutumia mtaji wa Fisadi Lowassa hata kwa gharama ya kuuza Identity yenu ya kisiasa na agenda zenu?
Hivi mnajua athari za kisiasa baada ya October kama mkimpokea Lowassa sasa?
Hivi CHADEMA itakuwaje kisiasa kama Lowassa atagombea kwa tiketi ya CHADEMA na akafanikiwa kushinda au bahati mbaya akashindwa?
Hivi CHADEMA mnajua Lowassa ana malengo gani na huo urais?
Hivi mnajua kwa nini CCM kwa gharama kubwa kabisa ilihakikisha Lowassa hapewi nafasi ya kugombea?
Hivi hamjiamini kuwa nyie wenyewe mnaweza pasipo msaada wa makapi ya CCM?
CHADEMA mnawezaje kuacha mbachao kwa msala upitao?
CHADEMA NI NANI ALIYEWALOGA?