Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

sijawahi kumwamini mbowe wote na lowassa wana kitu kimoja wanachofanana wote wanataka kuingia ikulu kwa njia yoyote. cdm wamepata umaarufu kwa kupinga ufisadi lakini leo hii mwenyekiti anapomakribisha mtu waliyekuwa wanamuimba ni fisadi sijui wanatoa picha gani.Pia kuna wanachama waliojitolea kwa hali na mali wengine mpaka wamepoteza maisha lakini anawadharau kwa ajili ya hayo makapi.kama mwenyekiti alitakiwa aijenge chadema kama chama na sio kusafiria nyota ya mtu
 
Mbona CCM mnalialia sana? hamtaki Lowassa aende Chadema wakati huo huo huko kwenu mmekata jina lake kwa hila hivi mnataka aende wapi? Hebu acheni upuuzi mwacheni achague mwenyewe.
 
huyu
mzee akienda cdm mimi kwa mara ya kwanza nitatafuta kadi ya chama chochote poteleambali hata kile cha mtikila
 
Mbona CCM mnalialia sana? hamtaki Lowassa aende Chadema wakati huo huo huko kwenu mmekata jina lake kwa hila hivi mnataka aende wapi? Hebu acheni upuuzi mwacheni achague mwenyewe.

Duu janga lingine hili
 
Nakubaliana kabisa na mtoa hoja na kutaka hao wanaomzima kinywa eti akaulize mahali pake, tangu lini JF pakawa mahali penu? aulize hapa hapa, na hata mimi nakubaliana na wewe Mbowe hana haki ya kutuamulia wana Chadema, waache mihemuko amkaribishe huyo fisadi wake aone kitakachowakuta, labda kama kura wanapiga wao, umaarufi wa chadema sio wa viongozi ni wa sisi wanachama, ndio sisi tunapigwa mabomu, na kuswekwa rumande kila siku. Hatutaki hayo makapi kama anashida ya chama asubiri baada ya uchaguzi waje kujiunga kama wanachama wakawaida, tutawatengenezea mafunzo maalumu ya kuwafundisha kuwa wanachama wa chama kilichosimama kwa mateso, sisi hatukuingia hapa kwa pilau na kanga, tumekanyaga mbigili na chupa wakae hatutaki ebola huku hatutaki najisi huku wakae huko wamalizane na wezi wenzao wa huo mpango wa Richmond, tunataka wakamatwe kama wakina Mramba na wafikishwe mahakamani na huyo Rostam wao
 
Taarifa hii inaukweli ipo kwenye magazeti ya leo likiwemo LA Tanzania Daima ambalo huandika habari chanya za chadema pia gazeti la mwananchi ambalo siku za karibu linaandika habari chanya za chadema
 
Chadema kumkaribisha fisadi lowasa hata kwa tetesi tu ndo byebyeeee!!
 
Akikatwa!Na kupachikwa fisadi lowasa,ntarudisha kadi ya chadema asubuhi saa 1.na ntaacha kufuatilia siasa za bongo!

Mkuu hata mimi hasa nikivuta hisia kwamba nyuma ya lowasa kuna watu hawa rostam,chenge,karamagi nakata tamaa kabisa na siasa za bongo..fisadi leo amekuwa lulu
 
Lowasa nae kazingua kuhamia chadema, chama ambacho viongozi wake wengi hata 1st degree hawana.
 
Dr.Slaa tunakuomba umtoe Lowassa kwenye orodha yako ya mafisadi.
 
Tanzania daima ni gazeti la Mbowe - aka CDM, sasa haliwezi kwa namna yoyote kutoa taarifa za uongo
 
ukombozi utakuja kweli? awe mwanAchama wa kawaidaa kinyume na hapooo... mtashangaa..
 
Chadema inahitaji kufanya maamuzi sahihi;-
lowassa ni mtihani mpya kwao na ni kipimo cha weledi wao hvyo suala la kumpokea ama lah ni suala ambalo linapaswa kuangaliwa mara mbili mbili kwani kumpokea bwn EL kwaweza kuwa na matokeo ya aina mbili aidha hasi ama chanya kutokana na wimbi la kashfa alizonazo bwana huyu hvy suala hilo linaweza kupoteza ile identity ya chama ya kupambana na ufisadi kama wataweza kumpokea fisadi papa kama anavyojulikana miongon mwa wananchi ,kwa hy kaz kwenu chadema hiki ni kipimo cha msimamo wenu kama chama
 
Back
Top Bottom