Well said mkuu. Ni ukweli usio fichika, ukawa hawana mgombea wa maana ambaye tunaweza kumkabidhi nchi. Ni janga tupu, hawajajipanga. Wanategemea kukopa kutoka ccm, na kujitapa kote wanavyojitapaga, ni kichekesho. Sikutegemea ndio maana Prof Lipumba aliona upuuzi akaamua kubwaga manyanga, tupilia kule na kuendelea na hamsini zake.Jamani kuna uvumi ulioenea kwenye mitandao kuwa Lowasa akija Ukawa anapewa nafasi ya kugombea uraisi kupitia muungano huo. Sasa najiuliza, hivi Ukawa wamejiandaa kweli kushika dola ikitokea wameshika? Maana kama wanategemea kukodi mtu kutoka ccm ndo aje apeperushe bendera manake Ukawa hawana uwezo wa kushika dola. Asanteni
Nahama rasmi
Jidanganyeni hivohivo.
Well said mkuu. Ni ukweli usio fichika, ukawa hawana mgombea wa maana ambaye tunaweza kumkabidhi nchi. Ni janga tupu, hawajajipanga. Wanategemea kukopa kutoka ccm, na kujitapa kote wanavyojitapaga, ni kichekesho. Sikutegemea ndio maana Prof Lipumba aliona upuuzi akaamua kubwaga manyanga, tupilia kule na kuendelea na hamsini zake.
Mbona mm cjamskia lowassa mwenye kwenye vyombo vya habari akitangaza kujiunga chadema!?
We naona ni mgeni katika siasa zetu hizi. Unataka kusema hujamwelewa Mbowe mpaka leo hii? ???Ni leo nimepata kuona habari mitandaoni na magazetini kuwa Mh mbowe katoa kauli ya kumkaribisha Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa kujiunga na chama chetu pendwa chadema.
Awalli sikutaka kuamini na bado sijaamini kuhusu hizi fununu,na kama ni kweli, namtaka Mh Aikael Freeman mbowe atoe maelezo fasaha amemkaribisha lowasa aje kufanya nini? Sote tunamjua Lowasa na tuhuma nzito za kifisadi, tuna mfahamu vizuri Lowasa na kundi lake la mbwa mwizi linalomzunguka.
B inafsi simkatai lowasa kama binadamu bali napinga tabia yake ya uwizi rushwa, uroho na ubinafsi.
Natahadharisha kusema kuwa CHADEMA tunaipenda toka moyoni ndio maana hatutingishiki na sunami za ccm kwa kuwa tunaamini Chadema ni chama safi na chenye uhakika wa kutuletea mabadtiko chanya kwa taifa. Kwa nilivyoona kauli hizi ni dhahiri chama kinaenda kuanguka kwa kuwakatisha tamaa wananchi.
Lowasa ni nani ktk chadema, cjama kimeimarika vya kutosha nila uwepo wa lowasa, nini mnachotegemea kwa Lowasa kwa sasa, ccm imemuona hafai ikamtema wewe unamkaribisha bila hata aibu, unataka kutuaminisha kuwa nyie ni maswahaba? Kama ndivyo iweje ccm tuinyoshee mkono?
Mh Mbowe umetukera sana sinaamani kabisa hadi uje utupe ufafanuzi zaidi nini maana yake.
Anakaribishwa kuwa mwanachama lakini si kuongoza nchi, unajua ukiwa muislamu ukaingia ukristo kubali kuwa hutakuwa mchungaji au padre siku ya kuingia na kbatizwa pia ukiwa mkiristo ukajiunga na uislamu yaani ukaslim suitegemee kuwa utakuwa Shekhe mara ukiingia lazima ichukue muda na ndicho tunachokitaka kwa Lowasa. Viva Ukawa Viva Tanzania tunayoitakalowasa hasafishiki hata kwa JIk....
Acha siasa za Ukanda wewe Lembeli kwani anatoka Kaskazini?Mchukueni wassira Chadema, au kwa kuwa hatoki kaskazini?
Hiii habari ni ya kweli?
Mi nafikiri awepo atubu na asipewe nyadhifa kwa kipindi cha miaka 10 kwanza.
Mkuu sikusikia/kusoma habari magazetini. Amemtaja kabisa 'Edward Lowassa' au kwa kusema ni chama cha watanzania wote, ndiyo mtu una feel kuwa invited?