unafiki ni dhambi wanaweza kumficha ili waje wampe uwaziri mkuu, kama kurudisha gharama ambazo atawasaidia kufanyia kampaini mwaka huu,
maaana mnafiki ni mnafiki tu hata usiku ni mnafiki,
Mnachosahau ni ukweli kwamba Dr. Slaa si mroho wa madaraka, na wala hana interest na Urais.
Tatizo ni kuwa waanzilishi wa propaganda hii ni ccm na pia CDM wanatumia propaganda hii kuendelea kuvuna wanachama kutoka ccm,ila nina hakika 100% lowasa hawezi kujiunga CDM na hata ccm wanalijua hili,CDM wanajua kabisa kumruhusu lowasa kujiunga nao nikukibomoa chama kwa haraka na hakika,wale wanachama wafia chama wengi wataondoka CDM na wengine wataachana na siasa...madhara yakumpokea lowasa CDM ni mabaya na makubwa sana,maana watapoteza watu muhimu sana ambao wana imani kubwa sana na CDM na pia itakuwa ni tusi kubwa ambalo CDM watakuwa wamelifanya dhidi ya watanzania wapenda mabadiliko yenye nia ya dhati yakubadili mfumo huu wakinyonyaji na wenye gap kubwa la kiuchumi
Magufuli alianza na mungu na atamaliza na mungu ,miamba yote ya wanafiki na shetani itasagana yenyewe,na mwisho alichokipanga mungu mwanadamu hawezi kukipangua kwa namna yoyote hile,
Suala sio kuhama CCM wote kuhamia Chadema.Suala ni itikadi ya vyama hivi viwili.Itikadi ni sawa na imani ya dini,siyo rahisi kumshawishi mkristo akawa mwislamu au kinyume chake,ukiona mtu anabadili dini basi hakujengwa kwenye misingi ya imani ya dini hiyo tangu mwanzo.Vyama vya siasa ni hivyo hivyo.:bowl:
Labda aje kuwa mwanachama wa kawaida vinginevyo narudisha kadi.atasafishwaje huyu fisadi?hapo Zitto atawapigia bao.
Kaka hata huyu naye ni wale wale tumepigwa changa la macho tu.Huyu naye ni mwizi tu kama wenzake.Wala hWana tofIti na huyu wanaijua bei yake ndiyo maana wamemteua.
Walioachwa ndiyo walikuwa bora kuliko huyu aliyeteuliwa na Mkullu ili kumsaidia kuficha dhambi zake.
Chenge ndani ya ngumba,Ngeleja na wenzake duh,kaka usitegemee Embe kwenye mtikiti.
Hazungumzwi Dr Slaa kama individual, anazungumzwa kama Mgombea anaebeba haiba ya Upinzani
Katika hili mwenyekiti wangu amekengeuka kama ni kweli ameamua kumkaribisha Lowasa. Ni Kuua CDM na upinzani kwa ujumla haiwezekani mtu makini kumkaribisha fisadi na siku zote umemwita fisadi leo unamkaribisha si bure kunabiashara hapa inafanyika. Hivi Dr Slaa unamuweka wapi na aibu hii kubwa? Nina hakika CDM wapo watu makini wataupinga huu upuuzi
kapime mkojo inaezakuwa mimba hiyo.
kibaraka wa fisadi mramba katika ubora wake.Tulia sindano ikuingie mambo ya CDM hayakuhusu
Toka lini umeanza kuisemea Cdm?
Wafu mnazidi kuweweseka tu
mkuu hapana wenye jicho la tatu walimuona na kweli atasaidia kufumua mifumo yote michafu ,anauwezo huo na amefanya hivyo ,nakuhakikishia mkuu kitu cha kwanza cha kumpima ni baraza la mawaziri wake.
kutoka kupinga ufisadi mpaka ku-promote.
Bila shaka hizi zitakuwa akili za bangi.
Sasa ni dhihiri kuwa CHADEMA iko kwenye mikakati mizito ya kumshawishi au kuafikiana na Edward Lowassa ili aweze kuhama CCM na kujiunga CHADEMA na hapo hapo apewe nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Nikiwa kama mshambuzi wa mambo ya siasa humu JF, mtanzania mpenda maendeleo na mpenzi wa CHADEMA jambo hili limenishtua na kunisikitisha sana.
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa na magazeti kadhaa ya leo akisema, Lowassa anakaribishwa CHADEMA na hana tatizo lolote, na hapo hapo baadhi ya wabunge na viongozi wa juu wa CHADEMA wamenukuliwa ama wakiunga mkono ujio au kumumunya maneno kuhusu hilo.
Mpaka sasa sijui, ni nini kimewaingia viongozi wa CHADEMA kuanza kukubali jambo hili. Nini msukumo wao?
Ni nani asiyemjua Lowassa? Huyu ni mwanasiasa mchafu, ambaye amewekeza muda, pesa na watu wake wengi sana katika siasa ili afanikiwe tu kuwa rais wa Tanzania.
CHADEMA bado tu humjajifunza kutokana na makosa? Yuko wapi Samweli Sitta, John Shibuda nk?
Mtaacha lini kusubiri makapi ya CCM ili kuyapokea na kuwapa nafasi za ugombea katika uchaguzi?
Hivi mnajua kwanini watanzania wengi waliwapenda na kuwaamini?
Hivi agenda ya kupambana na Ufisadi hamhitaki tena?
Hivi viongozi wa CHADEMA mnatambua siasa itaendelea tu hata baada ya October 25?
Hivi mnajua kwanini watanzania walitoa maisha yao hata kufa kuona CHADEMA inasonga mbele?
Inakuwaje muwe na mawazo ya kupata madaraka tu kiujanjaujanja kwa kutumia mtaji wa Fisadi Lowassa hata kwa gharama ya kuuza Identity yenu ya kisiasa na agenda zenu?
Hivi mnajua athari za kisiasa baada ya October kama mkimpokea Lowassa sasa?
Hivi CHADEMA itakuwaje kisiasa kama Lowassa atagombea kwa tiketi ya CHADEMA na akafanikiwa kushinda au bahati mbaya akashindwa?
Hivi CHADEMA mnajua Lowassa ana malengo gani na huo urais?
Hivi mnajua kwa nini CCM kwa gharama kubwa kabisa ilihakikisha Lowassa hapewi nafasi ya kugombea?
Hivi hamjiamini kuwa nyie wenyewe mnaweza pasipo msaada wa makapi ya CCM?
CHADEMA mnawezaje kuacha mbachao kwa msala upitao?
CHADEMA NI NANI ALIYEWALOGA?
Yaani baada ya miaka yote ya upambanaji wa ufisadi tunakaribisha mafisadi..... haiingii akilini, nami nitajitoa siku hiyo hiyo CDM
Hazungumzwi Dr Slaa kama individual, anazungumzwa kama Mgombea anaebeba haiba ya Upinzani