Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

unafiki ni dhambi wanaweza kumficha ili waje wampe uwaziri mkuu, kama kurudisha gharama ambazo atawasaidia kufanyia kampaini mwaka huu,
maaana mnafiki ni mnafiki tu hata usiku ni mnafiki,

Hawakumbuki JKN alisemane kuhusu Mchaai aliyezoea kula nyama ya binadamu.Hata wamfanyeye hata acha kamae utamu wake lazima atataka kula tu.

Waache wajidanganye...
 
Katika hili mwenyekiti wangu amekengeuka kama ni kweli ameamua kumkaribisha Lowasa. Ni Kuua CDM na upinzani kwa ujumla haiwezekani mtu makini kumkaribisha fisadi na siku zote umemwita fisadi leo unamkaribisha si bure kunabiashara hapa inafanyika. Hivi Dr Slaa unamuweka wapi na aibu hii kubwa? Nina hakika CDM wapo watu makini wataupinga huu upuuzi
 
Suala sio kuhama CCM wote kuhamia Chadema.Suala ni itikadi ya vyama hivi viwili.Itikadi ni sawa na imani ya dini,siyo rahisi kumshawishi mkristo akawa mwislamu au kinyume chake,ukiona mtu anabadili dini basi hakujengwa kwenye misingi ya imani ya dini hiyo tangu mwanzo.Vyama vya siasa ni hivyo hivyo.:bowl:
 
Tatizo ni kuwa waanzilishi wa propaganda hii ni ccm na pia CDM wanatumia propaganda hii kuendelea kuvuna wanachama kutoka ccm,ila nina hakika 100% lowasa hawezi kujiunga CDM na hata ccm wanalijua hili,CDM wanajua kabisa kumruhusu lowasa kujiunga nao nikukibomoa chama kwa haraka na hakika,wale wanachama wafia chama wengi wataondoka CDM na wengine wataachana na siasa...madhara yakumpokea lowasa CDM ni mabaya na makubwa sana,maana watapoteza watu muhimu sana ambao wana imani kubwa sana na CDM na pia itakuwa ni tusi kubwa ambalo CDM watakuwa wamelifanya dhidi ya watanzania wapenda mabadiliko yenye nia ya dhati yakubadili mfumo huu wakinyonyaji na wenye gap kubwa la kiuchumi

pole sana kama haujui subuli kwanza ,wafiacha kipi na cha nani?
 
Magufuli alianza na mungu na atamaliza na mungu ,miamba yote ya wanafiki na shetani itasagana yenyewe,na mwisho alichokipanga mungu mwanadamu hawezi kukipangua kwa namna yoyote hile,

Kaka hata huyu naye ni wale wale tumepigwa changa la macho tu.Huyu naye ni mwizi tu kama wenzake.Wala hWana tofIti na huyu wanaijua bei yake ndiyo maana wamemteua.

Walioachwa ndiyo walikuwa bora kuliko huyu aliyeteuliwa na Mkullu ili kumsaidia kuficha dhambi zake.

Chenge ndani ya ngumba,Ngeleja na wenzake duh,kaka usitegemee Embe kwenye mtikiti.
 
Mpuzi huyu kwakuwa nimtu wa arusha hawabagui mbona zitto aliomba kujiunga na ukawa zuzu huyu akaweka umungu mtu wake
 
Suala sio kuhama CCM wote kuhamia Chadema.Suala ni itikadi ya vyama hivi viwili.Itikadi ni sawa na imani ya dini,siyo rahisi kumshawishi mkristo akawa mwislamu au kinyume chake,ukiona mtu anabadili dini basi hakujengwa kwenye misingi ya imani ya dini hiyo tangu mwanzo.Vyama vya siasa ni hivyo hivyo.:bowl:

mkuu tulia kwanza yapo mawili yatakukuta mwaka huu
1, kumtangaza waziwazi ili tuchanje mbuga kweda ikulu au
2, kutumia pesa zake na wewe ukiwemu kwenye kampaini zao na malipo yake nafasi ya uwaizri mkuu au bihashara,

hakuna namna ya kuyakwepa haya maana makubaliano tayari japo kwa siri sana lakini ukweli haufichiki,maamuzi makuu ni ya wenye chama mtu na mkwe wake basi,
na kimia hiki kinasoma upepo,lakini hakisaidi wala hakitabadilisha yaliyopangwa,
 
Kaka hata huyu naye ni wale wale tumepigwa changa la macho tu.Huyu naye ni mwizi tu kama wenzake.Wala hWana tofIti na huyu wanaijua bei yake ndiyo maana wamemteua.

Walioachwa ndiyo walikuwa bora kuliko huyu aliyeteuliwa na Mkullu ili kumsaidia kuficha dhambi zake.

Chenge ndani ya ngumba,Ngeleja na wenzake duh,kaka usitegemee Embe kwenye mtikiti.

mkuu hapana wenye jicho la tatu walimuona na kweli atasaidia kufumua mifumo yote michafu ,anauwezo huo na amefanya hivyo ,nakuhakikishia mkuu kitu cha kwanza cha kumpima ni baraza la mawaziri wake.
 
Hazungumzwi Dr Slaa kama individual, anazungumzwa kama Mgombea anaebeba haiba ya Upinzani

Siyo hilo tu na chama pamoja na wanachama wake.Huwezi kuleta simba eti anilindie Mbuzi wangu.Duh!!!
 
Katika hili mwenyekiti wangu amekengeuka kama ni kweli ameamua kumkaribisha Lowasa. Ni Kuua CDM na upinzani kwa ujumla haiwezekani mtu makini kumkaribisha fisadi na siku zote umemwita fisadi leo unamkaribisha si bure kunabiashara hapa inafanyika. Hivi Dr Slaa unamuweka wapi na aibu hii kubwa? Nina hakika CDM wapo watu makini wataupinga huu upuuzi

pesa ndugu hacha kabisa
ndo maana watu wanasema siasa ni unafiki,na ukweli sio kuwa ndo wanaanza kuongea LEO ni muda mrefu sana tena kwa siri sana,vipo vikao vya siri vimekuwa vikifavyika pa kificho sana,inawezeka wasimlete wazi ili kuwadanganya watanzania lakini ukweli SLAA ATATUMIA PESA YAKE KUZUNGUKA KUFANYA KAMPAINI
SI NI SAWA NA KUMUWEKA WAZI TU ILI AWASAIDIE MAANA NI MZOEFU NA MBINU NYINGI ANAZIJUA ZA USHINDI,

 
mkuu hapana wenye jicho la tatu walimuona na kweli atasaidia kufumua mifumo yote michafu ,anauwezo huo na amefanya hivyo ,nakuhakikishia mkuu kitu cha kwanza cha kumpima ni baraza la mawaziri wake.

Alishindwa kuonxoa rushwa,wizi na ufisadi kwenye wizara yake.Alihusika kuuza nyumba za serikali na.kugawa kwa hawara yake.Hata uniambiaje nitakujibu nilivhojibu.

Huyu ni Mbwa mwitu amevaa ngozi ya kondoo.Na ukitaka kuwa Thomaso kuwa tu lakini
Tunaye mfahamu hafai hata kutuchungia kuku.

Kilicho tokea ndani ya chungu huwezi jua kulikuwa na nini kwenye jiko.Ukiona Maharage yameiva ujue mkaa umeteketea.
 
kutoka kupinga ufisadi mpaka ku-promote.
Bila shaka hizi zitakuwa akili za bangi.


yameisha mwagika hayazoleki,wala hatuitaji utetezi wa vyombo vya habari na vikao vya ukanusho ,hizo habari watu wanazo muda mrefu sana na mienendo yote ,
so haisaidi nashauri tumchukue atatusaidia ushindi mwaka huu,
 
nimecheka sana kwenye red hapo. hivi kwa akili yako unafikiri wanachokihubiri chadema ndo wanaochokiishi? hawa ndo wale wa fuata maneno yangu achana na matendo wangu.
huko wamebaki misukule tu na wale wenye masilahi. wanjanja tulishashituka kitambo tukaendelea na yetu.

Sasa ni dhihiri kuwa CHADEMA iko kwenye mikakati mizito ya kumshawishi au kuafikiana na Edward Lowassa ili aweze kuhama CCM na kujiunga CHADEMA na hapo hapo apewe nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Nikiwa kama mshambuzi wa mambo ya siasa humu JF, mtanzania mpenda maendeleo na mpenzi wa CHADEMA jambo hili limenishtua na kunisikitisha sana.

Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa na magazeti kadhaa ya leo akisema, Lowassa anakaribishwa CHADEMA na hana tatizo lolote, na hapo hapo baadhi ya wabunge na viongozi wa juu wa CHADEMA wamenukuliwa ama wakiunga mkono ujio au kumumunya maneno kuhusu hilo.

Mpaka sasa sijui, ni nini kimewaingia viongozi wa CHADEMA kuanza kukubali jambo hili. Nini msukumo wao?
Ni nani asiyemjua Lowassa? Huyu ni mwanasiasa mchafu, ambaye amewekeza muda, pesa na watu wake wengi sana katika siasa ili afanikiwe tu kuwa rais wa Tanzania.

CHADEMA bado tu humjajifunza kutokana na makosa? Yuko wapi Samweli Sitta, John Shibuda nk?
Mtaacha lini kusubiri makapi ya CCM ili kuyapokea na kuwapa nafasi za ugombea katika uchaguzi?

Hivi mnajua kwanini watanzania wengi waliwapenda na kuwaamini?
Hivi agenda ya kupambana na Ufisadi hamhitaki tena?

Hivi viongozi wa CHADEMA mnatambua siasa itaendelea tu hata baada ya October 25?
Hivi mnajua kwanini watanzania walitoa maisha yao hata kufa kuona CHADEMA inasonga mbele?

Inakuwaje muwe na mawazo ya kupata madaraka tu kiujanjaujanja kwa kutumia mtaji wa Fisadi Lowassa hata kwa gharama ya kuuza Identity yenu ya kisiasa na agenda zenu?
Hivi mnajua athari za kisiasa baada ya October kama mkimpokea Lowassa sasa?
Hivi CHADEMA itakuwaje kisiasa kama Lowassa atagombea kwa tiketi ya CHADEMA na akafanikiwa kushinda au bahati mbaya akashindwa?

Hivi CHADEMA mnajua Lowassa ana malengo gani na huo urais?
Hivi mnajua kwa nini CCM kwa gharama kubwa kabisa ilihakikisha Lowassa hapewi nafasi ya kugombea?

Hivi hamjiamini kuwa nyie wenyewe mnaweza pasipo msaada wa makapi ya CCM?
CHADEMA mnawezaje kuacha mbachao kwa msala upitao?

CHADEMA NI NANI ALIYEWALOGA?
 
Yaani baada ya miaka yote ya upambanaji wa ufisadi tunakaribisha mafisadi..... haiingii akilini, nami nitajitoa siku hiyo hiyo CDM

Na kama ndiyo hivyo sina sababu ya kujiandikisha kupiga kura!Ili iweje?Nampigia kura fisadi,mwizi wa mali za umma,mla rushwa asiye na haya mpaka kutaka kununua urais?

Hivi hawaoni huyu aliyemsaidia kuununua urais ametufikisha wapi?

Kweli wakimuingiza CDM waisubirie kadi yangu huko huko ufipa.
 
Back
Top Bottom