Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

yaani CDM wana muomba Lowassa ajiunge nao hii ajabu kweli bora yeye ndiyo angeomba basi.
 
Miye nilidhani wewe ni mwanachama wa cdm kumbe ni m-ccm. Pikipiki usoila yakuwashani?
 
mbona mnaweweseka sana!! viongozi wanajua nini wanachofanya, na siku zote siasa hazina uadui wa kudumu. Mi ninachotaka kwa sasa ni ccm itoke tu, siangalii ni njia gani itakayotumika, kufika hapo,
 
Karibu Sana UKAWA lowasa nilitamani siku moja itokee hivi sasa ukawa lazima tuchukue inchi pamoja Sana lowasa
 

Asante.Tulishindwa kumwelewa JKN alipotuambia huyu tuliyenaye bado mtoto,tulapumbazwa na fedha zilizomwagwa kwa wajumbe na baadhi ya watanzania kumpigia debe sana.

Leo tunakaribisha yale yale tuliyokatazwa.Tuachane na madiwani,wabunge,na wagombea wote wa urais watakaowek peaa ili kununua uongozi.Tujiulize akisha pata uongozi analipaje?

Leo tunadeni kubwa lisiloweza kulipika na mkopo.huo umeishia kulipa madeni ya kupata uongozi.Tumeona Kura za NDIYOOOOOOO zisizosaidia Taifa zikipigwa bungeni wala kuwa na tija kwa Taifa sababu ya woga wa kukatwa pale ubunge utakapo koma.Wabunge wetu wanahongwa vijisent ili waweze kupitisha hata miswada isiyo na tija kwa Taifa ukiangalia 90% ya wabunge wameingia kwa kununua nafasi hizo.

Jamani tuseme basi sasa.
 
Chadema mkomboz wa taifa, ukitubu na kuacha utasamehewa.. Karibu kamanda
 
Karibu Lowassa utuambie wote waliyohusika na Richmond najua ulikuwa kafara. Ili mambo yaende
 
Inawezekana mtoto wa mmiliki danguro kubwa la kwanza Tanzania then Tanganyika akawa msafi kweli?No,haiwezekani kwa kuwa huyu ni mtu aliyezaliwa kwenye uovu uliopindukia na dhambi ya baba yake bado inamtafuna.What does this imply,ni kwamba kumtegemea Mbowe awe mtu msafi kwa lolote ni kama kutaka kuchuma embe kwenye Mchungwa,jambo lisilowezana kabisa.Kwangu kwa Mbowe lolote linawezekana.
 
Nimenasa mpango mzito wa siri wa kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi mwaka huu kiulainii bila kutumia nguvu kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na Urais. Mpango wenyewe umeanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2011 kwa mamluki wengi kupandikizwa chadema kuanzia ngazi ya mtaa mpaka taifa; Nawahakikishia kuwa CCM itashinda kata nyingi na majimbo mengi bila kupingwa baada ya mamluki kujitoa pindi watakapokuwa wamepitishwa na NEC; Katika nafac ya urais ndugu Magufuli anatarajia kushinda kiulaini baada ya mgombea wa chadema ambae anatarajiwa kuwa Lowasa kujitoa katika mbio hizo baada ya kuwa nae ameshapitishwa na Tume ya uchaguzi. Lowasa ni sehemu ya mpango huo wa kuhakikisha ccm inashinda kiulaini huwezi mtenganisha lowasa na ccm na Kikwete
 
Jipange tena mkuu.. Upo kama waandishi wa Yale magazeti yanayoandika bikira ya flank ilitolewa na flani. Nenda halafu uje tena
 

Kama mtaendelea kumwamini Mbowe basi mmepotea,Mara kumi mngempigania Dr Slaa awe Mwenyekiti kipindi kile,Nimesikia mambo mengi machafu kuhusu huyu jamaa,kwamba hata kwenye ESCROW pia alishiriki kupiga ila sikutaka kuamini,ila kwa kumsafisha Lowassa sasa kumenifanya niamini niliyoyasikia,jamaa ni mjanja mjanja tu hana lolote.
 
cha ajabu wanao ponda wote ni ccm tuna juana humu na hizo ID zenu,tangu lini mkawa na mapenzi na chadema mpaka mnajifanya mna huruma eti cdm itapotea kwa vile lowassa ana tia maguu cdm rasmi kesho mwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…