ally linje
JF-Expert Member
- Feb 28, 2013
- 222
- 50
Daah lowasa kweli anautaka urais aseee
Anautaka ili akafanye biashara ya nchi.... Hatari haufai kabisaaa arudi Monduli tuu
Daah lowasa kweli anautaka urais aseee
rumours are made by haters of lowasa spread by fools and accepted by ------ ...mtoa maada yawezekana ni hater wa lowasa ama in fool anaesambaza hii kitu , msomaji angalia sana usije ukaamini huu upuuzi unless we ni idiot
Ushauri wangu kwa Chama aka CCM.
HIZI TAARIFA ZIWE ZINAPRINTIWA HALAFU ZINAGAWIWA KWA WATU WOTE, MJINI NA VIJIJINI ILI HILI FISADI LIKOSEA KURA KWA KIASI CHA MAFURIKO.
HEKA HEKA CCM, HAKIKISHENI HIZI TAARIFA ZINAFIKA KIJIJINI KABISA. NDO DAWA YA HILI FISADI NA NGO LA CHADEMA.
Huu upuuzi uliletwa siku nyingi hapa JF ukawekwa kwenye jukwaa la udaku.
Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.
Mh.Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo
Na Mwandishi wetu | Gazeti la Sauti Huru
Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.
Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)
Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.
Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"
Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.
" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;
"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".
...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'
"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.
Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "
"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"
Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.
"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"
"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."
Source: Gazeti la Sauti Huru
My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.
Nini maana ya udaku?Sidhanı km udaku nı uongo.
Anautaka ili akafanye biashara ya nchi.... Hatari haufai kabisaaa arudi Monduli tuu
"Mkwe" wa mwenye chama ameharibu na kuua upinzani bila washabiki (sio wanachama) wa upinzani kujua. Wanachama wa vyama vya upinzani wamelijua hili mapema na ndi maana wameamua kukaa kimya.
"Mkwe" yupo kibiashara zaidi hasa ukizingatia sasa hivi disco lake halimuingizii pesa ki hivyo, familia yake imemshinda hadi ameachana na mkewe kabaki na watoto, huku yeye akitakiwa kulipa karibu 10m kila mwezi kama matumizi, unategemea hela za kumtunza mkewe anapata wapi kama asipofanya biashara kwenye siasa ambapo anayo fursa? Tunahitaji upinzani wa kweli ili tuingie ikulu, sio tuwaingize ikulu wachumia matumbo, hao ndio wataliua kabisa hili taifa na kuliingiza matatani.
Ninachoona ni kuwa October 27 matokeo yakitangazwa, na kuwa declared kuwa mamvi ameshindwa, mamvi atatangaza kuhama chama, maana "mkwe" hatokubali kumkabidhi uenyekiti mamvi, na hapo ndipo waropokaji humu ndani wote watakapomkumbuka "Padri" na kumwomba aje ajenge chama, maana he is the only one left ambaye anaamiwiwa na wanachama (sio washabiki).
Poleni wenye chama chenu ambacho kimeuzwa na "mkwe"
Maandamano CHADEMA jadi yenu...tutawaacha mtusindikize IKULU kwa maandamano pia, taratiiiiiibu. #CCM #Hapakazitu maandamano ukawa
The post of 2011 has been recalled in 2015!
Surely, JF is the wind that exposes the chicken's anus!
Magazeti mengine ni kichekesho
Kesho unaweza kusikia from SAUTI HURU kwamba Mama Anne Makinda amefunga ndoa na Mzee Edwin Mtei ikiwa imeletwa na mwandishi wetu
Magazeti haya sijui serikali inayaangilia vipi?
Duh huyu jamaa alifikiri mbali,sasa huu ndyo ukweli maadui wawili wameungana..
Hvi kesho anarudisha fom nec au ndo afya haiko vyema?? Taarifa plz
Duh. Kuna ambaye alisha wahi kuchangia uzi huu 2011? Ama wazee wa kitengo wame insert hii kitu?