Susuviri
JF-Expert Member
- Oct 6, 2007
- 3,713
- 891
Hii si ya 2011 mkuu? Ilipuuzwa lkn leo tunaona yote yakitimia!
Hizo story ziko nyingi sana.Ukweli gani wakati kila kitu kipo wazi!!? Au wew ndie haufahamu Ukweli maana mtu mwenye busara hauwezi utakubali ujinga anaoufanya Mbowe, sasa kama nawewe ni miongoni wa waliokubali kununuliwa na Kibabu cha Monduli kupitia kwa Fisadi Mbowe jiandae kisaikolojia maana unaelekea kushindwa October hatuwezi kuchagua Mfanyiabiashara wa siasa... Magufuli anatoshaaaa banaaa
kwanini usiweke huo ukweli hapa kama unapingana na mwandishi wa hii thread???Hizo story ziko nyingi sana.
At least I know the reality I can stand to speak it.
Ntafute nikupe gazeti lote la kuhama kwa Lowassa na upokelewaji wake
Tiote upo..??Kwa upande mmoja sitaki kuamini kwamba Mbowe anaweza kukubali kujichimbia kaburi la kisiasa kwa kukubali kupokea vipande thelathini vya shaba. Hata hivyo, nikijua jinsi hawa jamaa walivyo na mbinu na kiu ya kujaribu kununua kila mtu, siondoi uwezekano wa hili kutokea na kwa hili nakubaliana na analysis ya Banyimwa.
Sitaki pia kumuondoa Zitto katika hili kwani ukaribu wa Zitto na hawa mafsadi ni mkubwa kuliko hata ule wa Mbowe na mafisadi. Nakumbuka alivyopigia debe Dowans na baadae Mwanahalisi kumuanika.
Kwa hiyo CDM wachunge hili na kulifuatilia kwa kina lakini vile vile huyu Zitto ni wa kumuangalia zaidi maana ilisemwa humu kwamba much as anaipenda sana CDM, lakini anaipenda sana pesa kuliko CDM.
Habari hii inaweza ya kupikwa lakini imepikwa kwenye mazingira yanayoelekea kuwa kweli:
Tanzania Daima kumpamba ENL
Mbowe yupo kibiashara zaidi
Mbowe hajawahi kumsifia/kumpamba Dr. Slaa hata siku moja (fuatilia), maana yake hapendezewi naye jinsi alivyo moto kwa mafisadi
Mbowe hawajawahi kutoa kauli yoyote ya kumlaani/kumsema ENL au RA
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Duh!kweli JF is Where we dare to talk Openly.
Mbowe= Nick Clegg. lol.
Ukweli ni kwamba mambo kama haya katika siasa yapo haswa katika nchi zetu hizi zakibongo. Ukweli ni kwamba JK will never let Lowassa be president (atatumia CC kukata jina lake, na sababu itakayosemwa ni ile ile iliompoteza Malecela kuwa Mwalimu alikua hamtaki na pia scandal na kujiuzulu kwake kunamfanya asifae).
Kwahiyo kuna logic kubwa hapa. Inawezekana sana hizi zikawa campaign za Zitto kujaribu kumpunguza nguvu Mbowe (kama ni uongo) lakini vile vile inawezekana ikawa kwamba ni mchongo wa CCM kuivunja nguvu CHADEMA (JK and his people might have found that it would be useful to undermine Lowassa through this and at the same time undermine CHADEMA). Lakini kwa kuzingatia jitihada za Lowassa kujisafisha na kujihalalisha kuwa na nafasi ya kiti cha Rais ametoa pesa nyingi kuwezesha wabunge wengi wa CCM na hata wa upinzani kushinda uchaguzi.
Makadirio yasio rasmi kutoka wanasiasa mbali mbali zinasema kuwa ametoa pesa kwa takribani asilimia 75% ya wabunge waliopo Bungeni hivi sasa. Pamoja na kununua viongozi wengine wa CCM, viombo vya usalama ikiwemo TISS na vile vile vyombo vya habari kama tunavyofahamu tayari.
Hii inaonyesha strategy ya huyu bwana ni kucontrol channels zote zinazotumika kuchuja na kuchagua Rais. Bila shaka anawatu wake Central Committee lakini JK anaweza mpoteza aidha kwa kutumia sababu ambazo nimetaja hapo juu haswa kama CHADEMA na vyombo vingine vya kisiasa vikiendelea kumuandama katika miaka hii mitano ijayo. Hivyo kwa kuzingatia tactics it is extremely logical and likely that these allegations are true.
There is a clear motive on Lowassa's part as well as Mbowe ( kama ilivyotokea kwa Clegg, na kama hali ilivyo Kenya kwa mfano). Ukweli ni kwamba hii kitu ni mbaya na inahitaji kuchunguzwa zaidi na kutumia misingi ya kuto kupendelea au kufikiria kwa kutumia hisia za uzalendo wa ki-CHADEMA. In other words, these allegations warrant serious objective investigation and analysis.
Lisemwalo lipo na kama halipo basi linachongwa na 2015 mtaliona.
Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.
Mh.Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo
Na Mwandishi wetu | Gazeti la Sauti Huru
Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.
Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)
Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.
Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"
Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.
" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;
"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".
...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'
"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.
Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "
"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"
Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.
"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"
"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."
Source: Gazeti la Sauti Huru
My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.
Mwandishi wa thread hii atakuwa anayetaka kuwaambukiza wote wazimu wake! Hataji lini, wapi, kiasi cha pesa na jinsi zilivyolipwa! Watanzania si wajinga kiasi hicho! Akajipange upya na ahusishe vyombo wanavyotumiaga!