Makoye Matale
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 6,490
- 2,104
NILIAMBIWA WACHAGA WANAPENDA PESA LEO NIMEAMINI:thinking::thinking::thinking::thinking:
acha mambo yako! huoni au ukiclick first page huoni wachangiaji walichangia mwaka gani?Hii post imetengenezwa leo saa 23:30 kana kwamba ilikuwa 31.3.2011. Jaribu kufuatilia mtiririko wa matukio utaona ni kweli ninachoandika. Haina ukweli wowote kabisa.
Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.
Mh.Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo
Na Mwandishi wetu | Gazeti la Sauti Huru
Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.
Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)
Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.
Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"
Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.
" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;
"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".
...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'
"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.
Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "
"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"
Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.
"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"
"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."
Source: Gazeti la Sauti Huru
My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.
Nina wasiwasi na mods katika hili! Kama vipi wekeni na poll ya JK si msafi! Acheni kutumika!
JF ni jukwaa huru ambapo members wote wana uhuru wa kutoa mawazo yao na uchambuzi wa kina bila uoga.
This is where we dare we dare to talk openly.
Una uhuru wa kutoa maoni yako upendavyo lakini huna uhuru wa kuzuia maoni ya wengine ili mradi kanuni za jukwaa zinafuatwa.
Tafadhali anzisha uzi wako kuhusu JK tutachangia vile vile kwa uwazi bila woga. Huwezi washinikiza mods wakufungulie uzi.
Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.
Mh.Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo
Na Mwandishi wetu | Gazeti la Sauti Huru
Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.
Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)
Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.
Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"
Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.
" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;
"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".
...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'
"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.
Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "
"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"
Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.
"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"
"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."
Source: Gazeti la Sauti Huru
My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.
Hivi wewe Una akili kweli??? Basi Mimi ninazo kuliko za kwako unaetaka niamini upambavu wa kupika!! Ukisoma mwanzo wa hii thread mchangiaji mmoja kwa jina "TUTAFIKA" amenidhihirishia hii kitu imetengenezwa na wataalamu wa IT maana amesema mmeogopa maandamo that's why mnatafuta sababu za kumchafua Lowasa ndani ya chadema?? Jiulize nayo maandamano ya Lowasa ndani ya CHADEMA Ni yapi na yalitokea lini??? Deal imebuma kawaaminishe mburulazz wenzio sio miye binti wa kisukuma, shame on ur hopeless face...... Kwi, kwi, kwi, kwi, kwi, kwibodaboda2 aliyekutuma kakosea nadhani hoja hapa sio kupinga tu kila jambo, kuelewa pia ni suala zuri, nani alijua haya 2011 el kwa cdm alikua fisadi papa, na leo hii msafi kama pamba, kwanini unatapatapa kutafuta gazeti na stori imeelezewa fresh kabisa hapa, hautaki amini kua mbowe ni mfanyabiashara au hautaki nini??? maana kama asingehamia tungesema haikua kweli au ilikua kweli ila mbowe aligoma kumpokea sasa amepokelewa kwa shangwe na imegundulika hivyo kua ni mchezo ulipangwa.
Mkuu soma comment ya "TUTAFIKA"mwanzo wa hii thread ujiulize wameogopa mafuriko ya lini mpaka wakaweka bango Lao hapa la kuadaa watu kuwa Ni la2011! Na mafuriko ya lowasa ndani ya CHADEMA Ni mwezi huu!! Ili ujue imetengenezwa hii issue na nimesaka Hilo gazeti chocho zote kwa mwaka huo sijalipa, CCM Deal yenu imebumaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaandoroboooooooo nyieaaaaaa kuuuuuumbeee!!!
aiseeee!!!
inmaana hata miaka yote alipokuwa ccm alikuwa amekinunua chama na serikali yake ndo maana mlishindwa kumshtaki na mmeishia kusema kw mbaaaali km mbwa anavobweka kwa uoga eee.eti fisadi.
aiseee sasa km mtu anaweza kukinunua chama na serikali hadi mkakosa nguvu basi hii nchi ni yake na tunataka kiongozi wa uwezo huu.welldone lowasa ntakupa kura yangu.
Mkuu soma comment ya "TUTAFIKA"mwanzo wa hii thread ujiulize wameogopa mafuriko ya lini mpaka wakaweka bango Lao hapa la kuadaa watu kuwa Ni la2011! Na mafuriko ya lowasa ndani ya CHADEMA Ni mwezi huu!! Ili ujue imetengenezwa hii issue na nimesaka Hilo gazeti chocho zote kwa mwaka huo sijalipa, CCM Deal yenu imebumaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaandoroboooooooo nyie
Kwa upande mmoja sitaki kuamini kwamba Mbowe anaweza kukubali kujichimbia kaburi la kisiasa kwa kukubali kupokea vipande thelathini vya shaba. Hata hivyo, nikijua jinsi hawa jamaa walivyo na mbinu na kiu ya kujaribu kununua kila mtu, siondoi uwezekano wa hili kutokea na kwa hili nakubaliana na analysis ya Banyimwa.
Sitaki pia kumuondoa Zitto katika hili kwani ukaribu wa Zitto na hawa mafsadi ni mkubwa kuliko hata ule wa Mbowe na mafisadi. Nakumbuka alivyopigia debe Dowans na baadae Mwanahalisi kumuanika.
Kwa hiyo CDM wachunge hili na kulifuatilia kwa kina lakini vile vile huyu Zitto ni wa kumuangalia zaidi maana ilisemwa humu kwamba much as anaipenda sana CDM, lakini anaipenda sana pesa kuliko CDM.
Stunning!
Hii habari ilisikika huko nyuma na watu wakaipotezea lakini jamani lisemwalo lipo na kama halipo basi laja.
Mimi nikiangalia mwelekeo hata wa gazeti la Tanzania Daima hivi karibuni ninapata picha kwamba kuna jambo linachemka n siyo muda mrefu tunaweza kuona kitu cha kushangaza. Gazeti hili ambalo huko nyuma lilikuwa makini sana, kwa sasa limegeuka kuwa mdomo mahiri wa bwana Lowassa kila anapokuwa na lolote la kumpandisha chati. Hata suala la Dowans linavyopigiwa debe chanya na akina Hapiness Katabazi na wenzake ni jambo ambalo si la kupuuza.
Lakini hili la bwana Kibanda kuwa ndiye "mmiliki" wa jarida la UMOJA ambalo duru za uchuguzi zinasema ni mradi wa kumtakasa mkubwa huyu, na wakati huo huo akiwa ni mhariri mtendaji wa Tanzania Daima ni mambo yanayoleta mkanganyiko wa kujenga mashaka.
Chadema liangalieni hili kwa jicho lisilo la kishabiki ili kama lipo lizuiwe mapema maana litakiua chama au kukiondolea imani kwa wananchi.
Khaa!! Ndiyo maana kura yangu niliyomuwekea Dr Slaa sasa Nampa Dr Magufuli. NI HAKI YANGU