Mbona Watu Hawahoji Kuhusu CV ya Huyu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona Watu Hawahoji Kuhusu CV ya Huyu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Shinto, Mar 1, 2011.

 1. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ======================================================
  EDUCATION
  International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993

  TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985

  St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981

  St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]

  Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
  Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973

  Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
  Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969

  Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
  Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
  Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960
  ========================================================

  Ndugu wana JF. Hiyo ni Elimu ya "President" wetu Dr. Wilbord Slaa. Inapatikana katika CV rasmi ambayo aliiwasilisha bungeni.

  Wana JF, tumekuwa wakali ku-scrutinize elimu za watu hasa wanapotoa mawazo yanayopingana na itikadi na mwenendo jumla wa CDM. Rejea thread hapa iliyokuwepo wiki iliyopita iliyokuwa ikimchambua DR. BANA. Mengi yalisemwa kuhusu elimu yake nk.

  Lakini nimeipita CV ya mteule wetu Dr. (PHD). Slaa, napata maswali mengi. Hakuna amount of faith I have wala my love to the person and the party imeweza kuniondolea utata huu. Hasa ukizingatia tunavyokuwa wakali na kejeli kwa wengine.

  Ukiangalia elimu ya Dr. ni ya kiseminari through and through! Ingekuwa mtu mwingine hiyo ingekuwa negative credit hapa JF na angepata a lot of stick!

  Mbaya zaidi kwa Dr (PH. D) sioni sehemu aliyofanya Bachelor wala Masters Degree! Kutoka CERTIFICATES ghafla inaibuka PH.D! Jee hapa hamana ombwe tunalolifumbia macho?

  Habari ya kuwa (some cerificates) are equivalent to degree, ningeikubali kama angekuwa anafanya Masters!

  Najua kwanini hii ilipita, ni kwasababu kasoma katika vyuo vya kiimani ambavyo haviwi- regulated na any independent credible academic authority! Kwa maneno mengine hii ni kama ile ya akina Dr. Kamala!

  USIACHE IMANI/MAPENZI YAKO YAFUNIKE UKWELI!

 2. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  mtoa mada weka CV yako na wewe hapa tuzichambue sambamba na ya dr vinginevyo tunaangalia uwezo wa mtu katika kudeal na matatizo hata kama angeruka toka darasa la saba mpaka phd, tofauti na hao walio na miphd wasiyoweza kuitumia kutatua matatizo ya nchi
   
 3. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio double-standard mkuu.We ngine mnahoji CV zao,huyu unataka utendaji wake! Basi Mrema ni bora kuliko huyu!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Low....
  Una kazi moja tu humu..kudivert attention ya watu ili wasijadili hotuba ya msanii wenu aliyoitoa jana...
  hUMPATI MTU HAPA!...Nikitoka hapa naendelea kuchambua kule!
  Tumeshakugundua...
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama una amini kwamba watu hawahoji cv ya huyu mtu, mbona wewe umehoji? au wewe si ntu?

  Hata hivyo jaribu kuongeza bidii ya kupitia pitia mabandiko hata kwenye ma-archive kule kama ungepita usingekuja na haya malalmio yako.

  Huyu dakatari alishajadiliwa sana na maswali kama yako yalishaulizwa na kujibiwa.

  Jaribu kufanya kazi yako ya nyumbani vizuri zaidi.
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sioni haja ya kuanza kujadili hii kitu maana inanipotezea muda wa kuangalia mambo mengine ya msingi
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Japo huwa siyo shabiki wa haya mambo ya maprezdaa..nimeisoma hii nikacheka sana maana siamini mtizamo kama huu unaweza kutoka kwa mtu anayesomeka kama msomi na mwenye uelewa!

  nitauliza maswali machache:
  1. Kazi ya elimu ni nini? Ninavyoelewa elimu inamsaidia mtu kuchambua mambo na kuweza kutenda kwa ufanisi zaidi.NB urais siyo profession inayosomewa!

  2. Dr Slaa umewahi kuwa naye karibu au umewahi kumsikiliza ukaona kapwaya kwenye nyanja yoyote?

  3. Kama ni elimu ya Kiseminary - unayo idea kidogo kuhusu elimu itolewayo seminary? Hujiulizi ni kwanini shule za Seminary zinafanya vizuri kuliko shule nyingine? TAFAKARI HILI KWA MAKINI ndio utajua value ya elimu ya seminary ya Dr Slaa.

  Halafu mwaka jana kipindi haya mambo yanachambuliwa humuhumu JF kuhusu Dr Slaa, ulikuwa wapi unaamka saa hizi kuuliza kitu kisicho na maana?
   
 8. P

  Pokola JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo??
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa, Mrema ni bora kuliko huyu!!

  Si unaona hatimaye naye ametunukiwa Phd, kama aliyonayo kiongozi wako mkuu sana.

  Ngoja kwanza tuijadili hotuba ya malalamiko ya rais JK then tutarudi huku.
   
 10. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kunavichwa vikienda Masters vinalejea na PHD Kwa kichwa cha Slaa hiyo inawezekana. Kwahiyo usikalili, kuna Mheshiwa mmoja anaitwa Ndunguru pale Mzumbe, ukitafuta Masters yake hupati ana PHD na nikichwa si mchezo namba zinapanda kuliko. Kama umefika chuo kikuuu najua unajua haya yanatokea ila unataka kupotosha tu.
  Ombwe linaonekana sana pale mtu anapokuwa KIHIYO, ana PHD anafanya mambo ya Form two kama wale wanaolia bungeni kuhusu majimbo yao kwa mawaziri na kuishia kuunga hoja mia kwa mia.
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kwanza kama ulivyosema kuwa hauna chembe ya udini wala hidden agenda, swali lako nami nitarijibu bila chembe ya udini, upenzi wala hidden agenda. Mimi ni Mpentecost na kwa bahati najua elimu za kikatoliki.

  Miaka ya karibuni kumezuka wakatoliki wengi walio seminary kutaka elimu yao ibadilishwe na kufanana na standard za kidunia kwa sababu au hofu uliyoionyesha.

  Ukweli ni kuwa seminary hawafundishwi DINI TU..masomo mengi wanayofundishwa ni ya dunia hii, philosophy, geography, uraia, science courses, mathematics, .....name it wanayasoma vizuri tena kwa uwanja mpana sana.

  Kumbuka kuwa neno certificate au degree au diploma are not universal, maneno haya yanabadilika kutoka nchi moja na nyingine. Kwa mfano ufaransa mpaka PhD wanaita certificate, degree ya ujerumani hawaita Bsc wanaiti diploma in engineering. Leo hii kwa mfano unapo-apply shule USA,Canada kuna agents za ku-angalia vyet vyako kama vina meet standard za kwao, kwa hiyo NENO certificate kwa kirumi inaweza ni equivalent na degree fulani au masters fulani ila wanatumia 'certificate'.

  Ikumbukwe hata kihistoria japo haipo kwenye biblia Mussa alikuwa mwanasheria na alisoma chuo kikuu kinaitwa ELIMOPOLICE, ambako watoto wa matajiri walikuwa wanasoma wakati yeye akiwa jumba la farao, alisoma masomo mengi zikiwemo tamaduni za ki-misri, sheria, lugha n.k na equaivalent ya elimu yake ya wakati ule ni sawa na degree za sasa.

  Hesabu kwa mfano za trigonomoteric zimevumbuliwa miaka 600 B.C lakini ni aghalabu kipindi hicho ukakuta watu wanaitwa professors, Drs, degree holders n.k

  Hivyo basi kitamaduni za shule za seminary bado wanashikiria tamaduni za vyuo vyao vya mwanzo ambavyo havijabadilishwa kulingana na elimu za au standard za 'wababe' wa dunia HII BRITISH ambao wamedumaza ubongo wa watu wengi kuwa ili uonekane umesoma basi lazima uwe na first degree, masters, PhD...... LEO tunaweza tukaita same level of education with other names...hakuna kulazimishana, kwa mfano first degree tunaweza tukaita NGUMBARO, masters tukaita DUDUSA, Phd tukaita POZI....japo kwa kiswahili yana majina yao uzamili, uzamivu....problem is that we think british standard is universal IS NOT TRUE.

  Italy kwa mfano degree za engineering ni miaka 3 au 4, ukiongeza mmoja unaondoka na masters, ujerumani wanafanya hivyo. Tunaye professor Mwandosya ambaye hana masters alivyosoma first degree akafanya research na akawa awarded PhD! Canada wana utaratibu huo pia ambao mimi mwenyewe nime-uexperience ukiwa unafanya masters ukafanya vizuri au ukaextend wanakupa PhD! so jumping from certificate which equated as degree to PhD is NORMAL!

  wanaseminary wengi ni wasomi, wako deep na wengi huwezi kuwapambanisha na sisi tunaofundisha vyuo vikuu...wako mbali.

  Ukiangalia uongozi wa catholic churches uko kwenye mifumo ya kipekee sana, very stable sasa hii HAITOKANI na kusoma biblia tu ni masomo meengi sana ambayo mnayasomoa kwenye poltical science, medicines, sociology, history, journalism, social sciences, UCHUMI, etc., this knowledge have made this institution to be stable ever.

  Smile!
   
 12. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Unafikiri hiyo ni Phd ya mezani (wanaziita Phd za heshima) ......; at least huyu kasomea.

  Halafu kuna wadau kipindi cha nyuma waliwahi kuelezea hiyo Phd kwa undani zaidi, itafute hiyo thread for more information.
   
 13. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ndugu Jesuit, katik vyuo viku vya Kanisa, elimu ya msc wala bsc sio ishu sana kuizumzia. Kwani kwa mfano mdogo tu angalia how many years has been spent in the clas. Ukiangalia mpaka kupat phd frm secondary it takes more than 14yr in the clas plus research. Ndo maana utakuta kanisa katoliki wachungaji wao wanapat upadri baad ya zaid ya miaka 8, exlude sec na primary. Dr Slaa kabobea kwenye canon law. Nimbie wewe na Msc yako umeipat bada ya miaka mingapi ya tafit na darasa.
   
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada lazima ujiulize ni wakati gani Elimu za watu uhojiwa humu Jf? Kwa nfano umeshawahi kusikia watu wakihoji elimu ya Magufuli kabla na baada ya kupata Phd? Kwanini watu wanahoji elimu ya makongoro mahanga? ni kitu gani kinapelekea mtu aanze kwasasa kutaka kujua elimu ya Anna makinda? kwa mtazamo wangu nadhani ni pale mtu anapokuwa kafanya madudu fulani hivyo watu wanakuwa wanataka kujua wasifu wake
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  PhD ya Lyatonga ndio mwisho wa mambo yote.
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Asante Prof.Waberoya!

  NATAMANI NIONGEZEE LAKINI NITAHARIBU UTAMU HUU.
  Jesuit nadhani umeelimika vya kutosha kwa hii lecture nzuri..usitutie tena aibu!
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hivi nikiwa madrasa al sul miaka 16 zaidi ya kuwa brain washed napewa cheti gani ?
   
 18. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Well worded, nadhani kwa maelezo yako kama hataelewa basi hawezi tena, muacheni.
   
 19. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Re: Mbona Watu Hawahoji Kuhusu CV ya Huyu?

  Mkuu, kwanza kama ulivyosema kuwa hauna chembe ya udini wala hidden agenda, swali lako nami nitarijibu bila chembe ya udini, upenzi wala hidden agenda. Mimi ni Mpentecost na kwa bahati najua elimu za kikatoliki.

  Miaka ya karibuni kumezuka wakatoliki wengi walio seminary kutaka elimu yao ibadilishwe na kufanana na standard za kidunia kwa sababu au hofu uliyoionyesha.

  Ukweli ni kuwa seminary hawafundishwi DINI TU..masomo mengi wanayofundishwa ni ya dunia hii, philosophy, geography, uraia, science courses, mathematics, .....name it wanayasoma vizuri tena kwa uwanja mpana sana.

  Kumbuka kuwa neno certificate au degree au diploma are not universal, maneno haya yanabadilika kutoka nchi moja na nyingine. Kwa mfano ufaransa mpaka PhD wanaita certificate, degree ya ujerumani hawaita Bsc wanaiti diploma in engineering. Leo hii kwa mfano unapo-apply shule USA,Canada kuna agents za ku-angalia vyet vyako kama vina meet standard za kwao, kwa hiyo NENO certificate kwa kirumi inaweza ni equivalent na degree fulani au masters fulani ila wanatumia 'certificate'.

  Ikumbukwe hata kihistoria japo haipo kwenye biblia Mussa alikuwa mwanasheria na alisoma chuo kikuu kinaitwa ELIMOPOLICE, ambako watoto wa matajiri walikuwa wanasoma wakati yeye akiwa jumba la farao, alisoma masomo mengi zikiwemo tamaduni za ki-misri, sheria, lugha n.k na equaivalent ya elimu yake ya wakati ule ni sawa na degree za sasa.

  Hesabu kwa mfano za trigonomoteric zimevumbuliwa miaka 600 B.C lakini ni aghalabu kipindi hicho ukakuta watu wanaitwa professors, Drs, degree holders n.k

  Hivyo basi kitamaduni za shule za seminary bado wanashikiria tamaduni za vyuo vyao vya mwanzo ambavyo havijabadilishwa kulingana na elimu za au standard za 'wababe' wa dunia HII BRITISH ambao wamedumaza ubongo wa watu wengi kuwa ili uonekane umesoma basi lazima uwe na first degree, masters, PhD...... LEO tunaweza tukaita same level of education with other names...hakuna kulazimishana, kwa mfano first degree tunaweza tukaita NGUMBARO, masters tukaita DUDUSA, Phd tukaita POZI....japo kwa kiswahili yana majina yao uzamili, uzamivu....problem is that we think british standard is universal IS NOT TRUE.

  Italy kwa mfano degree za engineering ni miaka 3 au 4, ukiongeza mmoja unaondoka na masters, ujerumani wanafanya hivyo. Tunaye professor Mwandosya ambaye hana masters alivyosoma first degree akafanya research na akawa awarded PhD! Canada wana utaratibu huo pia ambao mimi mwenyewe nime-uexperience ukiwa unafanya masters ukafanya vizuri au ukaextend wanakupa PhD! so jumping from certificate which equated as degree to PhD is NORMAL!

  wanaseminary wengi ni wasomi, wako deep na wengi huwezi kuwapambanisha na sisi tunaofundisha vyuo vikuu...wako mbali.

  Ukiangalia uongozi wa catholic churches uko kwenye mifumo ya kipekee sana, very stable sasa hii HAITOKANI na kusoma biblia tu ni masomo meengi sana ambayo mnayasomoa kwenye poltical science, medicines, sociology, history, journalism, social sciences, UCHUMI, etc., this knowledge have made this institution to be stable ever.

  Smile! ​

  Last edited by Waberoya; Today at 02:45 PM. ​
   
 20. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hesabu miaka hapo kwenye read - utakuta ni sita: O leve-High School

  Kwenye Blue - seminary don't issue titles za degree -count kwenye blue utakuta:

  Kibosho seminary - 2 years: Uliwahi kuona certificate ya miaka miwili baada ya kumaliza form six katika secular education?

  Kipalapala - 4 years; Uliwahi kuona certificate ya miaka minne duniani baada ya kumaliza certificate nyingine for two years katika secular education?

  Kwa secular education - the first two years baada ya form six could have been a Diploma, the following four Years is an LLB or any other four years degree.

  Baada ya hapo ikiwa you have First Class you can join Phd Program katika University yoyote duniani.

  Kwa nchi zenye mfumo wa Juris Doctorate unahitaji kuwa na Degree ya Law or any speciality.
  study hata bio ya Obama - he has a BA then a Juris Doctorate.
   
Loading...