WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
re: Mbona watu hawahoji kuhusu cv ya huyu?
mkuu, kwanza kama ulivyosema kuwa hauna chembe ya udini wala hidden agenda, swali lako nami nitarijibu bila chembe ya udini, upenzi wala hidden agenda. Mimi ni mpentecost na kwa bahati najua elimu za kikatoliki.
Miaka ya karibuni kumezuka wakatoliki wengi walio seminary kutaka elimu yao ibadilishwe na kufanana na standard za kidunia kwa sababu au hofu uliyoionyesha.
Ukweli ni kuwa seminary hawafundishwi dini tu..masomo mengi wanayofundishwa ni ya dunia hii, philosophy, geography, uraia, science courses, mathematics, .....name it wanayasoma vizuri tena kwa uwanja mpana sana.
Kumbuka kuwa neno certificate au degree au diploma are not universal, maneno haya yanabadilika kutoka nchi moja na nyingine. Kwa mfano ufaransa mpaka phd wanaita certificate, degree ya ujerumani hawaita bsc wanaiti diploma in engineering. Leo hii kwa mfano unapo-apply shule usa,canada kuna agents za ku-angalia vyet vyako kama vina meet standard za kwao, kwa hiyo neno certificate kwa kirumi inaweza ni equivalent na degree fulani au masters fulani ila wanatumia 'certificate'.
Ikumbukwe hata kihistoria japo haipo kwenye biblia mussa alikuwa mwanasheria na alisoma chuo kikuu kinaitwa elimopolice, ambako watoto wa matajiri walikuwa wanasoma wakati yeye akiwa jumba la farao, alisoma masomo mengi zikiwemo tamaduni za ki-misri, sheria, lugha n.k na equaivalent ya elimu yake ya wakati ule ni sawa na degree za sasa.
Hesabu kwa mfano za trigonomoteric zimevumbuliwa miaka 600 b.c lakini ni aghalabu kipindi hicho ukakuta watu wanaitwa professors, drs, degree holders n.k
hivyo basi kitamaduni za shule za seminary bado wanashikiria tamaduni za vyuo vyao vya mwanzo ambavyo havijabadilishwa kulingana na elimu za au standard za 'wababe' wa dunia hii british ambao wamedumaza ubongo wa watu wengi kuwa ili uonekane umesoma basi lazima uwe na first degree, masters, phd...... Leo tunaweza tukaita same level of education with other names...hakuna kulazimishana, kwa mfano first degree tunaweza tukaita ngumbaro, masters tukaita dudusa, phd tukaita pozi....japo kwa kiswahili yana majina yao uzamili, uzamivu....problem is that we think british standard is universal is not true.
Italy kwa mfano degree za engineering ni miaka 3 au 4, ukiongeza mmoja unaondoka na masters, ujerumani wanafanya hivyo. Tunaye professor mwandosya ambaye hana masters alivyosoma first degree akafanya research na akawa awarded phd! Canada wana utaratibu huo pia ambao mimi mwenyewe nime-uexperience ukiwa unafanya masters ukafanya vizuri au ukaextend wanakupa phd! So jumping from certificate which equated as degree to phd is normal!
Wanaseminary wengi ni wasomi, wako deep na wengi huwezi kuwapambanisha na sisi tunaofundisha vyuo vikuu...wako mbali.
Ukiangalia uongozi wa catholic churches uko kwenye mifumo ya kipekee sana, very stable sasa hii haitokani na kusoma biblia tu ni masomo meengi sana ambayo mnayasomoa kwenye poltical science, medicines, sociology, history, journalism, social sciences, uchumi, etc., this knowledge have made this institution to be stable ever.
Smile!
last edited by waberoya; today at 02:45 pm.
mlaizer,
hii inafanana na ya waberoya mbona!?
?