Mbona Shule za Kidini hazina ada kubwa?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Kwa nini shule za binafsi zinazoongozwa na taasisi za kidini hazina ada kubwa? Ni lipi wanalofanya tofauti na hizi nyingine za bianafsi zinazotoza mamilioni ya ada kwa Wazazi na walezi?

Kama wamiliki wa shule binafsi hawawezi kutoza Ada inayoelekezwa na Serikali basi wafunge shule zao, kuna wadau wengi sana zikiwemo taasisi za kidini ambao wako tayari kutoa huduma ya Elimu kwa WatanZania kwa ada elekezi ya Serikali, kumbukeni kwamba nchini TanZania Elimu ni huduma kwa Jamii na siyo Biashara ya kupata faida, hivyo kama mlitaka kupata faida kuna biashara nyingine nyingi mnaweza kuwekeza mamilioni yenu badala ya kwenye shule kama kujenga viwanda vidogo vya uzalishaji, kufungua super market, au hata kujenga bwawa la kuogelea na kutoza waogeleaji lkn siyo kwenye Elimu, nchi yetu hairuhusu huwo mfumo!
 
Zipi hizo,mimi.ninazozijua zinaada kubwa.Kwani ada kubwa ni shs ngapi kwanza
 
Hii nchi IPO kwenye mfumo gani wa kiuchumi?? Ubepari au ujamaa?? I'm still perplexed guys...Any clarification please....
 
Tofautisha kati ya Biashara, Msaada, na Service

Serikali hata ikitoa Elimu bure hio ni service kwa wananchi wake na Kodi yako na yangu ndio inalipia hio Service (kwahio in short sio bure..)

Shule za Dini zinatoa Misaada kwa Jamii (hivyo hata zikitoa Elimu Bure kuna sponsorship nyuma ya pazia)

Shule za Binafsi zipo pale kutengeneza Profit (kwahio zitaendelea kuongeza ADA mpaka pale Demand itakapokuwa ndogo kuliko Supply) hapo automatically ushindani utapelekea bei kushuka.

Cha Maana ni Shule za Serikali zikiwa bora kama hizo za Binafsi watu wanapokimbilia basi hio za Mapesa Mengi zitakufa kifo cha kawaida.., (unless kama kutabakia Market ya watu wanaotaka watoto wao waende kwenye exclusive schools, yaani za wachache, na kigezo cha kuwa pale ni lazima mzazi awe na mapesa)
 
Lakini mfumo wetu wa Elimu hauruhusu hilo la kutengenza faida kupitia Elimu na liko wazi kwenye Sheria ya Elimu ambayo wamiliki wote wa shule wanaijua na wameikubali!
 
Shule za kidini ninazozifahamu mmi ada zake ni kubwa sana,
Ukianzia na shule yangu Pandahill nilikosoma kipindi hicho,
 
Lakini mfumo wetu wa Elimu hauruhusu hilo la kutengenza faida kupitia Elimu na liko wazi kwenye Sheria ya Elimu ambayo wamiliki wote wa shule wanaijua na wameikubali!

kwani serikali inatumia shs ngapi kusomesha motto mmoja kwa mwaka labda tuanzie hapo
 
Duh ada ya shule za dini ni balaa kubwa Marian,Mariagoreti,Henrygogate......ada zake kwa mwaka ni bei ya kununulia gari.
 
Lakini mfumo wetu wa Elimu hauruhusu hilo la kutengenza faida kupitia Elimu na liko wazi kwenye Sheria ya Elimu ambayo wamiliki wote wa shule wanaijua na wameikubali!
Hivi unadhani kuna mfanyabiashara binafsi ataanzisha shule ili kutoa huduma ?, Hio ni Kazi ya Kanisa / Dini au NGOs..

Kama soko lipo na fursa ipo sioni shida ni nini mfanyabiashara kuchuma pesa za watu ambao uwezo wanao, kuna watu wanaona fahari na uwezo wanao kusomesha watoto wao kwenye shule exclusive, kwanini hawa watu wasipewe fursa ya kupata huduma hio hapa na sio kuitafuta nje ?
 
Shule gani za kidini zinazotoza ada kidogo?au mleta uzi unaogelea madrasa nini?siku hizi hakuna cha dini, ni watoza ushuru hao,peleka mtoto akabatizwe kanisa katoriki bila laki moja habatizwi.
 
Shule za dini zinaendeshwa kwa sadaka za waumini na wafadhili mbalimbali kutoka nje hivyo hawategemei ada pekee kujiendesha tofauti na zile za binafsi halafu hizo taasis zina msamaha wa kodi unless kama wamefutiwa.Hakuna shule yoyote inayoeleweka iwe ya dini au binafsi inayotoza 150k day kwa mwaka au 350k bweni nchi hii.Hata afya ni huduma vilevile lakini gharama ya kipimo cha MRI pale Aghakan ni mara tano ya bei ya Muhimbili so wapeleke hizi siasa na huko tuone basi kama kutakuwepo na hospitali ya binafsi ama taasis ya kidini nchi hii.Hizo shule zikifungwa wazazi watapeleka watoto Kenya kama ilivyokuwa zamani so it's up to them kupima nani ataumia zaidi.Wanaoshabikia huu upuuzi hata hawatumii common sense maanake zikifungwa kuna maelfu wanaenda kukosa ajira walimu,wapishi,madereva,wahasibu,manesi,walinzi,wafagizi etc huu wote mzigo kwa serikali halafu juzi tu rais alidai serikali yake itakuwa rafiki kwa private sector sasa itawezekanaje kwa upuuzi huu.Hata Nyerere alikurupuka akazitaifisha zikamshinda akawapigia magoti wakamuwekea masharti MOU ikazaliwa so wapambe jipageni siyo kusifia tu hata upuuzi.BTW:Kuna mtu alilazimishwa kumpeleka mwanae huko? Kama huzimudu mfundishie kwako akafanye kama private candidate.Ujamaa alikufa nao Julius otherwise serikali iseme kama tumerudi huko tena.
 
Jengeni na nyie shule ili muone gharama ya uwekezaji wake! Siyo tu kuwa mnalalamika ada kuwa kubwa! Kama huwezi kulipa hiyo ada mpeleke akasome kwenye shule za serikali! Watu mnapeleka watoto wenu kwenye shule binafsi 'kwa nyodo' halafu mnaanza kulalamika lalamika!
 
Safi sana
 
Ni vema mtu akisema Shule binafsi za Dini zina Ada ndogo ataje jina la Shule hizo na kiwango cha Ada bila kusahau michango ya lazima kwa mwanafunzi.
 
Kwa nini shule za binafsi zinazoongozwa na taasisi za kidini hazina ada kubwa? Ni lipi wanalofanya tofauti na hizi nyingine za bianafsi zinazotoza mamilioni ya ada kwa Wazazi na walezi?

Kama wamiliki wa shule binafsi hawawezi kutoza Ada inayoelekezwa na Serikali basi wafunge shule zao, kuna wadau wengi sana zikiwemo taasisi za kidini ambao wako tayari kutoa huduma ya Elimu kwa WatanZania kwa ada elekezi ya Serikali, kumbukeni kwamba nchini TanZania Elimu ni huduma kwa Jamii na siyo Biashara ya kupata faida, hivyo kama mlitaka kupata faida kuna biashara nyingine nyingi mnaweza kuwekeza mamilioni yenu badala ya kwenye shule kama kujenga viwanda vidogo vya uzalishaji, kufungua super market, au hata kujenga bwawa la kuogelea na kutoza waogeleaji lkn siyo kwenye Elimu, nchi yetu hairuhusu huwo mfumo!

Shule za kidini hazina ada kubwa kwa sababu zinapokea msaada kutoka kwa wafadhili wakati shule binafsi zinategemea tu ada za wanafunzi.
 
Shule za kidini hazina ada kubwa kwa sababu zinapokea msaada kutoka kwa wafadhili wakati shule binafsi zinategemea tu ada za wanafunzi.

Sasa ni kwanini walianzisha shule kama walijua hawana juwezo wa kuziendesha?
Elimu TanZania siyo Biashara, bali ni Huduma kwa Jamii hivyo ndivyo sheria yetu ya Elimu inavyosema na wenye shule wote wanaijua kwani hauwezi kupata kibali cha kuanzisha shule bila ya kuipewa hii sheria na kuiridhia!
 
wote mmeishia kulalamika tu... toeni ushahidi unaoonyesha shule zinazo milikiwa na taasisi za kidini zinatoza sh kadhaa tofauti na shule zinazomilikiwa na watu binafsi kwa kutoza kiasi kadhaa.. lkn wote mna luka luka tu... alafu kuna jamaa anasema kubatiza mtoto kanisa la Roma mpka uwe na laki moja.. nasema ckweli.. unajaza form kwa sh 5000 tu
 
Back
Top Bottom