Mbona Shule za Kidini hazina ada kubwa?

Mbona Shule za Kidini hazina ada kubwa?

Shule za dini zina ada kubwa tu mazinde juu st.joseph msolwa na nyingine kibao ada zao kubwa sana
 
Kwa nini shule za binafsi zinazoongozwa na taasisi za kidini hazina ada kubwa? Ni lipi wanalofanya tofauti na hizi nyingine za bianafsi zinazotoza mamilioni ya ada kwa Wazazi na walezi?

Kama wamiliki wa shule binafsi hawawezi kutoza Ada inayoelekezwa na Serikali basi wafunge shule zao, kuna wadau wengi sana zikiwemo taasisi za kidini ambao wako tayari kutoa huduma ya Elimu kwa WatanZania kwa ada elekezi ya Serikali, kumbukeni kwamba nchini TanZania Elimu ni huduma kwa Jamii na siyo Biashara ya kupata faida, hivyo kama mlitaka kupata faida kuna biashara nyingine nyingi mnaweza kuwekeza mamilioni yenu badala ya kwenye shule kama kujenga viwanda vidogo vya uzalishaji, kufungua super market, au hata kujenga bwawa la kuogelea na kutoza waogeleaji lkn siyo kwenye Elimu, nchi yetu hairuhusu huwo mfumo!

hizo zinatoa huduma na hupokea ruzuku kutoka sehemu mbali mbali ikiwamo serikali. Pia hazipo katika kupata faida.
hizi za binafsi ni huduma na biashara , wamiliki wanahitaji faida kiduchu
 
Nashangaa sana watu wamepeleka wenyewe watoto wao shule za ada kubwa tena mwingine anatoka Mbweni anaruka shule zooote njiani ampeleke Segerea.
Kama ada kubwa si angempeleka ya ada ndogo? Wazazi wengine kusomesha mtoto shule ya ada kubwa ni sifa.
Wananchi hawajashindwa kulipa ada ila wanapenda ada kubwa ili kuheshimika kwa wanaowazunguka.
 
wote mmeishia kulalamika tu... toeni ushahidi unaoonyesha shule zinazo milikiwa na taasisi za kidini zinatoza sh kadhaa tofauti na shule zinazomilikiwa na watu binafsi kwa kutoza kiasi kadhaa.. lkn wote mna luka luka tu... alafu kuna jamaa anasema kubatiza mtoto kanisa la Roma mpka uwe na laki moja.. nasema ckweli.. unajaza form kwa sh 5000 tu

Krist Mfalme Tabata ilikua 960,000Tsh wakati Tusiime ilikua 2.8m
Sijui kwa sasa.
Ushahidi huo unatosha?
 
Mtoa post fanya uchunguzi kwanza.
Na unaposema wanatoza kidogo unamaana kidogo kipi?maana unaweza kusema kidogo ukimaanisha 1m so kuwa wazi kidogo kama kiasi gani?
 
Jimboni kwetu Kuna seminari Ada yake mwaka jana Ilikuwa around laki saba. Haina michango yeyote kwa mwanafunzi. Lakini kila mkristo lazima kwa mwaka aichangie. Kila parokia inatengewa kiwango chake cha changia Seminari na waseminari. Sasa shule kama hii Hata Ada ikiwa laki moja haiwezi athirika maana ina msaada kutoka kwa wakristo. Sasa mtu binafsi Nani ataichangia shule yako. Kwa 380,000 lazima ushindwe tu kuendesha shule.
 
SH. 380,000/ hazitoshi kuendesha Shule ya private.hata ya Serikali ni majanga tu. kwa nini isifanye evaluation kwa vitendo? mmm na huu mfumuko wa bei.!!!
 
Sasa ni kwanini walianzisha shule kama walijua hawana juwezo wa kuziendesha?
Elimu TanZania siyo Biashara, bali ni Huduma kwa Jamii hivyo ndivyo sheria yetu ya Elimu inavyosema na wenye shule wote wanaijua kwani hauwezi kupata kibali cha kuanzisha shule bila ya kuipewa hii sheria na kuiridhia!

Kwani hiyo dhana unayoleta ilianza lini si tangu nchi hii imekuwepo? Kwani huduma za jamii hazihitaji fedha? Mbona hata shule za serikali zinagharamiwa na ukiondoa ada ndiyo kusema kodi ambayo inalipwa inasimamiwa vizuri ili mwanachi asichangishwe tena maana tayari ameshalipa kodi inayotakiwa kukidhi gharama za elimu. Kwa shule binafsi ni tofauti. Hata hawa wanatoa huduma kwa mujibu wa sheria na kwa vile zile kodi wanachi wanazotoa hazipelekwi kwao ili ziingizwe kwenye mfumo wa kugharamia elimu ndiyo maana wale wanaochagua kwenda shule binafsi wanatakiwa wachangie gharama kwa ajili ya kuenendeshea shule na mahitaji mengine muhimu yatakayowezesha upatikanaji wa elimu bora.
 
Kwa nini shule za binafsi zinazoongozwa na taasisi za kidini hazina ada kubwa? Ni lipi wanalofanya tofauti na hizi nyingine za bianafsi zinazotoza mamilioni ya ada kwa Wazazi na walezi?

Kama wamiliki wa shule binafsi hawawezi kutoza Ada inayoelekezwa na Serikali basi wafunge shule zao, kuna wadau wengi sana zikiwemo taasisi za kidini ambao wako tayari kutoa huduma ya Elimu kwa WatanZania kwa ada elekezi ya Serikali, kumbukeni kwamba nchini TanZania Elimu ni huduma kwa Jamii na siyo Biashara ya kupata faida, hivyo kama mlitaka kupata faida kuna biashara nyingine nyingi mnaweza kuwekeza mamilioni yenu badala ya kwenye shule kama kujenga viwanda vidogo vya uzalishaji, kufungua super market, au hata kujenga bwawa la kuogelea na kutoza waogeleaji lkn siyo kwenye Elimu, nchi yetu hairuhusu huwo mfumo!

Shule za dini zinaendeshwa kwa sadaka za waumini na wafadhili mbalimbali kutoka nje hivyo hawategemei ada pekee kujiendesha tofauti na zile za binafsi halafu hizo taasis zina msamaha wa kodi unless kama wamefutiwa.Hakuna shule yoyote inayoeleweka iwe ya dini au binafsi inayotoza 150k day kwa mwaka au 350k bweni nchi hii.Hata afya ni huduma vilevile lakini gharama ya kipimo cha MRI pale Aghakan ni mara tano ya bei ya Muhimbili so wapeleke hizi siasa na huko tuone basi kama kutakuwepo na hospitali ya binafsi ama taasis ya kidini nchi hii.Hizo shule zikifungwa wazazi watapeleka watoto Kenya kama ilivyokuwa zamani so it's up to them kupima nani ataumia zaidi.Wanaoshabikia huu upuuzi hata hawatumii common sense maanake zikifungwa kuna maelfu wanaenda kukosa ajira walimu,wapishi,madereva,wahasibu,manesi,walinzi,wafagizi etc huu wote mzigo kwa serikali halafu juzi tu rais alidai serikali yake itakuwa rafiki kwa private sector sasa itawezekanaje kwa upuuzi huu.Hata Nyerere alikurupuka akazitaifisha zikamshinda akawapigia magoti wakamuwekea masharti MOU ikazaliwa so wapambe jipageni siyo kusifia tu hata upuuzi.BTW:Kuna mtu alilazimishwa kumpeleka mwanae huko? Kama huzimudu mfundishie kwako akafanye kama private candidate.Ujamaa alikufa nao Julius otherwise serikali iseme kama tumerudi huko tena.

Uko sawa mkuu.
 
Back
Top Bottom