Mkuu umedhihirisha upumbavu pia (SIYO TUSI)...! Kama ulikuwa Mkristo ukaishia kukasirishwa tu na maamuzi ambayo Mungu aliyafanya endelea kuamini kuwa uko sahihi.
Kiimani, taifa linapopatwa na mambo mabaya kama njaa, vita, au kuvamiwa na kutawaliwa na taifa jingine kanuni za ulimwengu wa roho zinaonesha kwamba taifa hilo ama litakuwa limemkosea Mungu sehemu fulani. Na hata hao unaowatetea kwa mtazamo wa mambo ya kale ni kwamba waliondolewa pale au nchi yao iligawiwa kwa Israel kwa sababu ya machukizo yao mbele za Mungu.
Hivi vita vya leo ni matokeo tu ya makosa ya pande zote mbili. Israel aliambiwa awaangamize kabisa wenyeji wa nchi hiyo (Kanaani) ila kwa sababu ya huruma na upendo wa kibinadamu wafalme wa Israel waliwahurumia baadhi ya watu hasa wanawake wazuri na watoto wakawabakiza na kiapo cha Mungu kikibadilika kwamba hao wenyeji wataendelea kuwasumbua Israel maisha yao yote na watakuwa mwiba kwao.
Endelea kuchukia na kukasirika, ila amini tu hata Tanzania ikileta ujinga mbele za Mungu nayo inaingia utumwani kwa njia moja au nyingine...