Mbona Mnazidi kunichanganya?? Nani mmiliki?

Hii ndii historia ya Israel kwa ufupi. Wayahudi Asili yao ni Iraq kutoka kabila linaitwa Huru ya wakaldayo. Ibrahimu ndiye aliyesafari na kuhama Iraq kwenda Nchi ya palestina kwa wakati huo ilifahamika kama nchi ya Kanani Pia Mungu alimhadi atampa nchi ya kanani yeye na uzao wake milele. Neno Israel ni Mungu mwenyewe Alimuita Mjukuu wa Ibrahimu Yakobo.Alimwambia hitaitwa tena yakobo bali Israel maana yake Taifa kubwa. Historia inaonyesha Baadae taifa La Babeli kwa sasa ni Iraq Lilitawala dunia kiuchumi kipindi hicho lilishambulia Israel na kuuteka Mji mkuu Yerusalemu kwa kipindi cha miaka 70. Baada ya hapo taifa la uajemi na waamedi Wakiongozwa na mfalme Koresh wa pili wakaipiku Babeli Iraq ya leo kiuchumu. Waajami kwa kwa sasa Ni taifa la (Iran) Wakawasaidi wayahudi kupata uhuru wao na kuwarejesha mateka wa Israel Yerusalemu. Wayahudi walikaa katika Ardhi ya Yao ya Yerusalemu zaidi ya miaka 470 Ndipo lijatokea shambulio la kutoka Dola ya Rumi ikiongozwa na Kamanda Tito ikaipiga Nchi ya Israel na kuharibu vikali hekalu la Sulemani Yerusalemu. Wayahudi waliosalia ambao hawakuuwawa walikombilia nchi za ulaya Magharibi na Taifa la Siberia ambalo kwa sasa Ni Urusi. Kabla Ya vita ya pili ya dunia Adolfu Hitler Akiongoza chama Cha wanazi na kukua kwa siasa sa Kifashist Alitengeneza Sera moja ya Sera zake ni kutaifisha Viwanda na makampuni yote yaliokua yanamilikiwa na Wayahudi baada ya kuchukua Hitla baada ya kuchaguliwa kuwa Cansela wa Ujerumani ndipo akaanza kutekeleza Sera zake kuwafilisi wayahudi na kuwafungu kwenye makambi ya mateso Inakadiriwa ujerumani kulikua na wayahudi zaidi ya Milioni 10 Sera za chuki za Fashism na Nashism kutoka Italia zilitengeneza chuki ndio ikapelekea mauaji Holcut walikufa wayahudi milioni 7.Mara baada ya Vita ya dunia na kuundwa Kwa Umoja wa mataifa (UNO) William james mwakilishi kutoka Uingereza alipeleka hoja ya wayahudi kupewa nchi yao wenyewe Kura ikapigwa kwa Kwa mataifa yaliokua wanachama na ikapelekea kugawanywa kwa Nchi ya palestina Israel apewe eneo Kaskazin mwa Yerusalem na Magharibi Tel Aviv ndio uwe mji mkuu Na Palestina Akapewa Upande wa kusini na Mashariki mwa Yersalemu. kimsingi Palestina alipewa eneo kubwa Zaidi ya asilimia 75 na Israel aslimi 25 ya ardhi. Jambo hili lilikua chukizo kwa nchi za kiarabu zote 1948-1950 vilikua vita vlivopewa jina (Israel Arab war) Mwaka 1956 Lilisukwa jaribia la kuishambulia Israel likashindwa. Mwaka 1967 mwezi juni Ndio vita ya kihistoria kwa Israel inafahamika Kama (Six day war). Kabla ya vita hii Dunia nzima iliingia kwenye hofu kubwa maana yalikua ndani ta vita hii mataifa mawili makubwa kiuchumi Marekani akishirikiana na Ulaya magharibi Uingereza na Ufaransa walikua upande wa Israel. Urusi ambayo kipindi hicho ndio dola lililokua linatwala dunia kiuchumi Na Muungano wa mataifa ya Ulaya Mashariki (USSR) Yalikua upande wa Waarabu. Waarabu wote wakiongozwa na Rais wa Misri Yasin Gamal Walinunua ndege nyingi na Rada za kisasa kutoka Urusi Bado Mfereji wa Suez Canal Ulibeba Manuwari za kivita nyingi. Waarabu Waliizingara Israel kila idara Kwa upande wa Kaskazini mwa Sirya walitegemea Milima Ya Golan na upande wa Kusini walitegemea milima Ya Sinai na ya Jagwa la Araba Lkn mbinu Israel Aliyotumia ni Kumshambulia adui yako kabla hajakushambuli. Israel Alifanya mashambulizi ya Anga masaa mawili mfulizo na kupelekea kuimiliki na kutawala anga lote kwa kuzipiga ndege za Misri, Sirya, Lebanon, Jordani. Na ndio vita iliyopelekea Palestinina kupoteza Eneo lote la Yerusalem Sirya kupoteza Mabonde na milima ya Golani na Misri kupoteza Mlima sinai Ila Misri alirudishiwa Mlima sinai mwa 1978 Baada ya kukubali maazimio ya Mkataba unaofahamika (Camp Devid Agreement) Moja ya makubaliano ni Misri kutojousisha kijeshi Katika Jangwa la Sinai pili Misri kutoingilia Mgogoro wowote wa Israel. Mwaka 1972 Nch za kiarabu zilipigana na Israel ili kukomboa maeneo yao zikashidwa. Mwaka 1982 Israel ilitangaza Yerusalemu ndio mji wake mkuu. Swali la kujiuliza Je! Israel kwa sasa ataachia Eneo la Palestina Jibu ni Hapana. Kwasababu tangia mwaka 1973 Israel anajijenge kijeshi na kumiliki lundo la Silaha za Maangamizi mpaka sasa Israel Haijakaguliwa ina milikiki silaha za nyuklia kiasi gani. Pili kwa sasa nchi za kiarabu zimegawanyika mfano mzuri ni huu mgogoro wa Irani na Isrel. Saudi Arabia, Baharin, Pakistani, Kazakastani, Jordani, Misri wako upande wa Israel na Saudia Arabia ameshasema Yuko taari kutoa anga yake muirani Apigwe.
Tatu sasa hivi yale mataifa ya kikomunisti yalioyokuwa adui na Israel sasa ni Marafiki mfano ni China Urusi na hata Tanzania.
Nne Kila siku mataifa ya kiarabu yakosa nguvu na kupoteza ushawishi duniani mfano Libya, Iraq, Sirya, Afganistani, Kuwet,
Tano Mataifa ya Magharibi kukua kiuchumi na kiteknolojia Yanazidi kuipa nguvu Israel kwa kutoikemea au kuiwekea vikwazo kwa pindi inapoua wapalestina.
Mkuu
Umenifanya nikenue meno ulipoitaja tanzania
 
Mleta mada kanichosha na uzi usio na vituo wala mpangilio nikapiga moyo konde labda chini nitakutana na summary!.
Ukauquote uzi wote na wewe halafu ukaandika na mengine ya kwako!.
Nimechoka kuisoma hii nyuzi kwakweli!.
Na mie nawachosha wanaokuja sasa!.
Ukisoma huu uzi wangu najua utachoka wewe unayefata!.
Lakini jamani tujifunze kuandika kwa vituo na aya.
Halafu tuache kupenda quote uzi mzima, tunaotumia cm tunahangaika.
Poleni
Uzi wako tunaweza kuusoma sababu ni mfupi.

Uzi wa mleta mada mrefu with no paragraphs. Hata kama ana Point vipi lakini bado ataonekana sio tu
 
Uzi wako hatuwezi kuusoma sababu ni mfupi.

Uzi wa mleta mada mrefu with no paragraphs. Hata kama ana Point vipi lakini bado ataonekana sio tu
Ngoja nirudie kuandika halafu nauquote na wenyewe tena!.:D
 
Kisheria na kihaki kabisa lile eneo lote ni la palestina
Wayahudi wao walivamia ardhi ile tangu kipindi inaitwa kanaani wakitumia kigezo cha kwamba wamepewa na mungu wao wa vita.

Wanaotetea eneo lile kidini/wakristo hivi niwaulize ikitokea huyo mungu akiwaambia wayahudi leo hii kuwa amewapa tanzania nao wakaja kwa lengo la kuichukua tanzania mtawaelewa? mtamuonaje huyo mungu?
Kumbuka kama wakipewa tanzania leo hii watakuja na kuanza kutuua na kutufukuza tukawe wakimbizi kwenye nchi za watu ili wao wachukue tanzania waliyopewa na mungu wao! mnakubali kuna mungu mpumbavu kiasi hicho?
Hebu tumieni akili bwana
Nilikuwa mkristo lakini kwa vitu vya kipumbavu kama hivi nikauvua na sasa sina dini.

Wayahudi ndio wanapaswa kuondoka pale na kuwaachia wazawa/wakanaani/wapalestina wa pale ardhi yao yote!
Haiwezekani kuwe na mungu mwenye upendo na wa haki afanye mambo ya kipuuzi namna hii
Mnaoitetea israel jitafakarini hivi kesho wayahudi wakaja na madege ya kivita, vifaru, bunduki alafu waanze kutushambulia waseme wameagizwa na mungu kuja kuikalia tanzania kimabavu mtawaelewa?

ACHENI UPUMBAVU
Mungu hayupo, dhana ya Mungu inatumiwa kisiasa na kiuchumi tu kwa kutimiza matakwa ya watu.

Ukielewa hili, utajua mzozo mzima unaanzia wapi.
 
Hizi kelele hazitasaidia kitu, Palestinians wabanane tu Gaza pale ndio kwao lkn sio Jerusalem.

Historically, hakuna jamii inayoweza kudai hati miliki ya eneo lolote, mfano eneo la Gaza lilikaliwa na Wakanaani miaka 4000 iliyopita baadaye tena ikatwaliwa na Wamisri kwa miaka 350 kisha ikatwaaliwa na Wapalestina na kwenye mwaka 1000 BCE ilitwaliwa na Waisrael.

Miji au nchi zimekuwa na historia ya ku-change hands toka enzi na enzi hivyo Palestinians kama walienda Jerusalem nao walienda tu kama wahamiaji hasa baada ya Waisrael, (The original inhabitants of Jerusalem) kwenda uhamishoni.

Isingekuwa swala la Waisrael kwenda uhamishoni, then Palestinians wasingeweza kuhamia Jerusalem mainly from Gaza. NB: history can't be corrected nor altered to make the Palestinians appear to be the original inhabitants of Judea hence Jerusalem. The Truth will never sink in water nor burn in fire, but it will always prevail.
 
ww wakanaan unawajua?? Unaweza kunieleza wakanaan kwasasa wanaishi nchi gani mkuu??
 
Mungu hayupo, dhana ya Mungu inatumiwa kisiasa na kiuchumi tu kwa kutimiza matakwa ya watu.

Ukielewa hili, utajua mzozo mzima unaanzia wapi.

Nimejaribu kuwatafakarisha tu mkuu maana hawa watu nikiwaambia moja kwa moja sio rahisi wanielewe
 
Hao ni dini gani mzee baba?
Kitu kingine watu wanaoverlook,
tukifuata maandiko,jehova aliwabariki waisrael na sio wayahudi,

ufalme wa israel wenye mji mkuu uitwao Samaria,uliangushwa na waasyria,na yale makabila 10 yakachukuliwa utumwani na waliobaki walikuja kuitwa wasamaria,lakini kiuhalisia ndo hasa waisrael,
wayahudi waliwatenga hawa na kuwa demonise,eti makabila hayo yamepotea na hayatopatikana tena,
it was a propaganda.
Wasamaria wanafuata vitabu vitano tu katika torati mpaka leo,
vitabu kama vya kina samweli,daniel,amos etc ni vya nationalists wa kiyahudi ambao walikuwa wanaandika kwa manufaa ya jamii yao ya kiyahudi.

Hawa chini ni baadhi ya hao wasamalia na hawatambui lolote kuhusu mji mtakatifu wa Daud.

250px-Samaritans_marking_Sukkot_on_Mount_Gerizim%2C_West_Bank_-_20051017.jpg
 
Hivi unajua kuwa Jews ni subst ya Israel?
 
Kisheria na kihaki kabisa lile eneo lote ni la palestina
Wayahudi wao walivamia ardhi ile tangu kipindi inaitwa kanaani wakitumia kigezo cha kwamba wamepewa na mungu wao wa vita.

Wanaotetea eneo lile kidini/wakristo hivi niwaulize ikitokea huyo mungu akiwaambia wayahudi leo hii kuwa amewapa tanzania nao wakaja kwa lengo la kuichukua tanzania mtawaelewa? mtamuonaje huyo mungu?
Kumbuka kama wakipewa tanzania leo hii watakuja na kuanza kutuua na kutufukuza tukawe wakimbizi kwenye nchi za watu ili wao wachukue tanzania waliyopewa na mungu wao! mnakubali kuna mungu mpumbavu kiasi hicho?
Hebu tumieni akili bwana
Nilikuwa mkristo lakini kwa vitu vya kipumbavu kama hivi nikauvua na sasa sina dini.

Wayahudi ndio wanapaswa kuondoka pale na kuwaachia wazawa/wakanaani/wapalestina wa pale ardhi yao yote!
Haiwezekani kuwe na mungu mwenye upendo na wa haki afanye mambo ya kipuuzi namna hii
Mnaoitetea israel jitafakarini hivi kesho wayahudi wakaja na madege ya kivita, vifaru, bunduki alafu waanze kutushambulia waseme wameagizwa na mungu kuja kuikalia tanzania kimabavu mtawaelewa?

ACHENI UPUMBAVU
Mkuu umedhihirisha upumbavu pia (SIYO TUSI)...! Kama ulikuwa Mkristo ukaishia kukasirishwa tu na maamuzi ambayo Mungu aliyafanya endelea kuamini kuwa uko sahihi.
Kiimani, taifa linapopatwa na mambo mabaya kama njaa, vita, au kuvamiwa na kutawaliwa na taifa jingine kanuni za ulimwengu wa roho zinaonesha kwamba taifa hilo ama litakuwa limemkosea Mungu sehemu fulani. Na hata hao unaowatetea kwa mtazamo wa mambo ya kale ni kwamba waliondolewa pale au nchi yao iligawiwa kwa Israel kwa sababu ya machukizo yao mbele za Mungu.
Hivi vita vya leo ni matokeo tu ya makosa ya pande zote mbili. Israel aliambiwa awaangamize kabisa wenyeji wa nchi hiyo (Kanaani) ila kwa sababu ya huruma na upendo wa kibinadamu wafalme wa Israel waliwahurumia baadhi ya watu hasa wanawake wazuri na watoto wakawabakiza na kiapo cha Mungu kikibadilika kwamba hao wenyeji wataendelea kuwasumbua Israel maisha yao yote na watakuwa mwiba kwao.
Endelea kuchukia na kukasirika, ila amini tu hata Tanzania ikileta ujinga mbele za Mungu nayo inaingia utumwani kwa njia moja au nyingine...
 
Kisheria na kihaki kabisa lile eneo lote ni la palestina
Wayahudi wao walivamia ardhi ile tangu kipindi inaitwa kanaani wakitumia kigezo cha kwamba wamepewa na mungu wao wa vita.

Wanaotetea eneo lile kidini/wakristo hivi niwaulize ikitokea huyo mungu akiwaambia wayahudi leo hii kuwa amewapa tanzania nao wakaja kwa lengo la kuichukua tanzania mtawaelewa? mtamuonaje huyo mungu?
Kumbuka kama wakipewa tanzania leo hii watakuja na kuanza kutuua na kutufukuza tukawe wakimbizi kwenye nchi za watu ili wao wachukue tanzania waliyopewa na mungu wao! mnakubali kuna mungu mpumbavu kiasi hicho?
Hebu tumieni akili bwana
Nilikuwa mkristo lakini kwa vitu vya kipumbavu kama hivi nikauvua na sasa sina dini.

Wayahudi ndio wanapaswa kuondoka pale na kuwaachia wazawa/wakanaani/wapalestina wa pale ardhi yao yote!
Haiwezekani kuwe na mungu mwenye upendo na wa haki afanye mambo ya kipuuzi namna hii
Mnaoitetea israel jitafakarini hivi kesho wayahudi wakaja na madege ya kivita, vifaru, bunduki alafu waanze kutushambulia waseme wameagizwa na mungu kuja kuikalia tanzania kimabavu mtawaelewa?

ACHENI UPUMBAVU
Km Israeli wataambiwa na mungu waje waichukue Tanzania hatutakubali kamwe!Lakini Israeli akitumwa na Mungu JEHOVAH kuja kuimiliki Tanzania tutashindwa kuzuia,kumbuka "Mungu akisema ndiyo,hakuna mwanadamu awezaye kumpinga"
 
Kweli mkuu! sio kwamba wapalestina wana haki tu ya kudai ardhi yao! Kama sheria zikitumika wayahudi wanatakiwa waondoke upesi eneo lile tena wawalipe wapalestina fidia kubwa kwa kuwasumbua miaka yote na kuua watu wao.

Kila nwenye kusimamia haki lazima asimame na wapalestina
Hakika mkuu.
 
Uzi wako tunaweza kuusoma sababu ni mfupi.

Uzi wa mleta mada mrefu with no paragraphs. Hata kama ana Point vipi lakini bado ataonekana sio tu
Kwani ulilazimishwa kusoma kiongozi au shida ni nini? Kama kiswahili ulikisoma mbona unatengeza tu hapo paragraphs.
 
Siku zote mi sitaki kubishana na Mungu
Alishasema wapalestina ni watumwa tu kwa israel na itaendelea kuwa hivyo mpaka mwisho wa dahari
Mungu sasa anaitumia marekani kuilinda israel na mji wake mkuu wa jerusalemu
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom