Mbona Lazaro Nyalandu amekuwa kimya sana tangu ahamie CHADEMA?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,239
113,612
Namzungumzia aliyekuwa mbunge wa CCM jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

Tokea atangaze kuhamia CHADEMA akitoka CCM amekuwa kimya sana.

Nawaza ni kulikoni huo ukimya wake? Je, labda anajutia huo uamuzi wake?

Au labda huo ukimya wake mwingi una mshindo na hivyo makamanda wavute subira?

Mimi binafsi bado naamini huyo bwana atarejea tu alikotoka kwa sababu siamini kama anayo DNA ya kuwa mpinzani kwenye nchi hii.

Alishazoea mema na istihaki za kuwa kwenye chama tawala na sidhani anaweza akakaa bila nazo kwa muda mrefu.

Muda utatueleza, hata hivyo.....
 
Mwenye hekima lazima anyamaze kwanza aangalie upepo unaendaje sio afike tu aanze kubwabwaja maneno, akianza ongea ongea itaonekana dhahiri alikihama chama Cha ccm kwa chuki na hasira au labda ya kutoelewana, ni vyema akae kimya kwanza maana akiongea ongea atapotezwa.
 
Ungependa asemee wapi wakati mmekataza siasa kwao?

Sijui huwa mnawaza kwa njia gani sijui. Mmesema wanaotakiwa kuseme na kusikika ni wabunge tena majimboni mwao tu, yeye sio mbunge tena na mmemnyang'anya uhuru wake wa kusema kama mwananchi wa kawaida bado unauliza mbona kimya!
 
Mwenye hekima lazima anyamaze kwanza aangalie upepo unaendaje sio afike tu aanze kubwabwaja maneno, akianza ongea ongea itaonekana dhahiri alikihama chama Cha ccm kwa chuki na hasira au labda ya kutoelewana, ni vyema akae kimya kwanza maana akiongea ongea atapotezwa.

Mimi nahisi alikihama CCM kwa hasira tu na hasira zikimuisha atarudi tu alikotoka.

Ni suala la muda tu.
 
Namzungumzia aliyekuwa mbunge wa CCM jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

Tokea atangaze kuhamia CHADEMA akitoka CCM amekuwa kimya sana.

Nawaza ni kulikoni huo ukimya wake? Je, labda anajutia huo uamuzi wake?

Au labda huo ukimya wake mwingi una mshindo na hivyo makamanda wavute subira?

Mimi binafsi bado naamini huyo bwana atarejea tu alikotoka kwa sababu siamini kama anayo DNA ya kuwa mpinzani kwenye nchi hii.

Alishazoea mema na istihaki za kuwa kwenye chama tawala na sidhani anaweza akakaa bila nazo kwa muda mrefu.

Muda utatueleza, hata hivyo.....
Hata Mr wako tangu aingie hapo Supermarket amekuwa kimya sana!
 
Back
Top Bottom