Mnyika: Nyalandu na mwenzake ni wasaliti, wameshindwa kuvumilia baada ya mateso ya kuporwa ushindi wa ubunge mwaka 2020

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,099
10,145
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho kilifahamu kuwa Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew, ambao wote walikuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, wangeondoka kutokana na mienendo yao waliyokuwa wakiionyesha kwa hivi karibuni.

“Hawa ni wasaliti, wamejiongeza wameshindwa kuvumilia baada ya mateso ya kuporwa ushindi wa ubunge mwaka 2020. Chadema itasonga mbele hadi mabadiliko, uhuru na haki na demokrasia vipatikane nchini.

“Mapengo yao yatazibwa na makamanda wengine na mapambano yanaendelea,” alisema Mnyika bila kutaka kufafanua kwa kina.

Juzi CCM iliwapokea Nyalandu na Mathew ambao ni makada wake wa zamani waliokihama chama hicho kati ya mwaka 2015 na 2017 na kwenda Chadema ambako hivi karibuni Nyalandu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kati na Mathew kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini.

Wawili hao walitangaza uamuzi huo katika mkutano mkuu maalumu wa CCM jijini Dodoma mbele ya Mwenyekiti mpya wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, huku wakiweka bayana masaibu waliyopitia na uamuzi wao huo wa kurejea kwenye chama tawala.

Nyalandu, aliyekuwa wa pili kutambulishwa na Rais Samia aliikana ahadi yake kutoihama Chadema ikiwa zimepita siku 1,278 tangu alipojiondoa CCM.

Kwa nyakati tofauti, Nyalandu amekuwa akijinasibu kuwa hawezi kuihama Chadema, kwa mara ya kwanza alimtaka Machi mwaka 2019 akisema yeye hakwenda Chadema kwa mafuriko. Msingi wa kauli ulitokana na kitendo cha Edward Lowassa kurejea CCM akitokea Chadema.

Kama hiyo haitoshi, Nyalandu alirejea kauli hiyo Agosti 2020 kwa staili tofauti katika mkutano mkuu wa Chadema wa kuchagua jina moja la mgombea urais aliyepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita.

Katika mkutano huo, Nyalandu alishindwa na mpinzani wake, Tundu Lissu na baada ya matokeo kutangazwa aliwaondoa hofu wanachama wa Chadema kuhusu mapenzi yake ndani ya chama hicho, akisisitiza yupo pamoja nao.

Lakini, jana katika mkutano mkuu wa CCM akitumia staili ya kunukuu baadhi ya vifungu vya biblia Nyalandu alisema: “Hakuna furaha izidiyo furaha ya mtoto arejeapo nyumbani.

“Wimbo wa bwana hauimbiki katika nchi ya ugenini, Mzee Sumaye (Frederick), Lowassa (Edward) na Dk Slaa (Wilbroad) ni mashuhuda wachache kati ya wengi kwa nini wimbo wa bwana hauimbiki katika nchi ya ugenini. Nakupongeza Rais kwa uongozi wako shupavu, nakushukuru kwa kukubali kunipokea na kunisamehe pamoja na kuniruhusu kurejea chamani,” alisema Nyalandu ambaye ni wazari wa zamani wa Maliasili na Utalii.

Kwa upande wake, Mathew alisema: ‘‘Nimekuja hapa kusema neno moja, nimeamua kurudi nyumbani. Nilikuwa ndani ya CCM na niliondoka CCM. Lakini, kadri unavyoendelea kuwa nje ya Chama cha Mapinduzi basi unajihisi una upungufu, leo (jana) nina furaha kubwa ya kuja mbele yenu wajumbe wa mkutano mkuu na kamati kuu,” alisema Mathew, maarufu ‘Messi’ aliyewahi kuingia kwenye mikwaruzano na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020.

Sio katika uchaguzi mkuu tu, bali hata kwenye kura za maoni ndani ya CCM za mwaka 2015 ambazo Nape pia alimshinda Messi. Hatua hiyo ilizua sintofahamu na kuamua kutoka CCM kuhamia Chadema.
 
Hakuna chochote cha ajabu hapo ktk siasa za kibongo.kuna mmoja wa cuf hezi ya kikwete alimnyari weee mwisho akasema yeye akienda ccm basi amlale mama yake.Ajabu ni kuwa alienda huko.
 
Hili suala la mtu kuhama chama mpaka lini litaendelea kutolewa maelezo marefu? hivi washamba ni sisi wapenzi, mashabiki, na wanachama wa vyama vya siasa au washamba ni viongozi wetu, au wote tu washamba?

Katiba mbovu tuliyonayo inatamka wazi kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa akipendacho, sasa maelezo mengi ya nini kumuelezea aliehama? au hufanywa hivyo ili kujibu mipasho ya wanaohama? I see no sense.

Hili jambo ni la kawaida, hebu sasa tuwekeze kwenye kuijenga Tanzania iliyo bora kwa kujiletea Katiba Mpya, ili kuwazuia hawa wanaohangaika kuhama kutoka chama kimoja na kwenda kingine kutafuta malisho mema watulie na kufanya mambo mengine ya maana.
 
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho kilifahamu kuwa Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew, ambao wote walikuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, wangeondoka kutokana na mienendo yao waliyokuwa wakiionyesha kwa hivi karibuni...
Huyo ni demokrasia huwezi ukakaa sehemu ambayo hujisikii kuwa huru ni Bora ukatafuta sehemu ambayo utakuwa na uhuru ndani ya moyo wako.
 
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho kilifahamu kuwa Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew, ambao wote walikuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, wangeondoka kutokana na mienendo yao waliyokuwa wakiionyesha kwa hivi karibuni...
Katibu piga kazi na sisi wana chama watiifu wa CHADEMA tupo pamoja.

Tumepita kwenye tanuru la moto mkali hadi sasa tulipo fikia bado tunapumua naamini hakuna atakaye katishwa tamaa na hao virus waliotumwa na ccm.
 
Hamkomagi nyinyi,mkiambiwa mnajitia wajuaji sana. Bado NAPE naye anakula jalamba anataka aingie sub
 
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho kilifahamu kuwa Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew, ambao wote walikuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, wangeondoka kutokana na mienendo yao waliyokuwa wakiionyesha kwa hivi karibuni....
Hakuna cha uzalendo wala mapenzi kwa chama chochote hapo, bali ni kuganga njaa. Aliyezoea kula bila kunawa hawezi kuishi upinzani. Kuna ushujaa, njaa na mateso.
 
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho kilifahamu kuwa Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew, ambao wote walikuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, wangeondoka kutokana na mienendo yao waliyokuwa wakiionyesha kwa hivi karibuni...
Mungu ibariki Chadema
 
Hata kesho ukisikia Nape kahamia upinzani,pasi na shaka atapewa na uongozi wa juu wa chama na vigeregere atapigiwa.
Siku akiamua kurudi CCM ataimbiwa nyimbo za umamluki na usaliti.
Hawa ndo wapinzani wa CCM hapa Tanzania.
Vp kuhusu kina Gekul, Silinde, Waitara na wengineo??

Chadema siyo Chama cha mapambio. Ukihamia Chadema unafundishwa ukakamavu uvumilivu na ujasiri hakuna pambio. Sasa wale waimbaji wa mapambio lazima wakimbilie chama cha kusifu kuabudu ili waweze kuimba mapambio yao.
 
Back
Top Bottom