Mbona hatukumuona Chongolo akifanya ziara ya kulaani ufisadi wa CAG? Kwanini anatetea Mkataba tu wa DP World?

Shakari

Senior Member
Jul 6, 2022
157
440
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo anasema ni wajinga wanaokosoa mkataba wa IGA kauli hii ni kinyume cha Katiba na Sheria za nchi na Miiko ya Viongozi wa CCM kuhusu kuheshimu utu na uhuru
wa kutoa maoni.

Kauli yake nyingine ni ile aliyoitoa kwenye Mkutano wa hadhara wa mikoa ya nyanda za juu kusini, uliofanyika jijini Mbeya tarehe 15.7.2023 ambapo alisema Serikali isihangaike kutoa Ufafanuzi juu ya mkataba huo
bali waachiwe wao Chama cha Mapinduzi kutoa Ufafanuzi na akaiagiza Serikali iharakishe kwenda hatua ya pili ya mchakato wa kuingia Mikataba ya utekelezaji.

Nataka nimkumbushe kwamba, Serikali inashauriwa kupitia vikao vya kikanuni na sio mtu binafsi, lakini pia Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichofanyika Dodoma Tarehe 9/7/2023 kiliagiza Serikali itoe elimu na isikilize Maoni ya wananchi kuhusu mkataba wa Bandari. Maagizo yake ni kinyume na maagizo ya vikao halali vya Chama na pia sio kazi ya Chama Kuridhia Mikataba wala kuzunguka nchi nzima kutoa elimu ya mikabata iliyoingiwa na Serikali.

Mbona hatukumuona Katibu Mkuu huyu akifanya ziara nchi nzima kuhusu kupanda kwa gharama za chakula na bidhaa nchini, tatizo la kukatika kwa umeme kwa zaidi ya miaka 2 na ugumu wa maisha nchini? Mbona hatukumuona akifanya ziara nchi kulaani wizi na ufisadi mkubwa uliotajwa kwenye Ripoti ya CAG ambapo matrilioni ya fedha yamepotea, dhuluma wanazofanyiwa wafugaji wa nchi hii, matatizo ya kuhamisha
wananchi wa Ngorongoro, kuanguka kwa bei za mazao kama Pamba na Alizeti na mengineyo.

Leo hii Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima kutetea mkataba wa ovyo wa Bandari, Je ana maslahi gani binafsi katika Mkataba huu? Kiufupi Viongozi hawa niliowataja wameshindwa kujibu hoja zinazoibuliwa na
wananchi katika mkataba wa IGA na badala yake wanaishia kutukana na kujipata kuhusu elimu zao.
 
Back
Top Bottom