Mbiu ya Maskini: - Iachieni nchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbiu ya Maskini: - Iachieni nchi!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mzee Mwanakijiji, May 6, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,387
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji (MwanaHalisi)


  Sasa najua kwanini waliliua Azimio la Arusha kule Zanzibar na kulizika bila kuliswalia dua za mwisho wala kulifanyia ibada ya mazishi. Sasa najua kwanini jina lake azimio hilo limefutwa milele kwenye vinywa vyao. Mwenzenu sasa nimetambua ni kwanini kabla ya kuanzisha wizi wao mkubwa wa mali na utajiri wa nchi yetu na kugawana wao kwa wao na watoto wao ilibidi kwanza kabisa wakiondoe kizuizi pekee kilichokuwa kati yao na urithi wa wana na mabinti wa taifa hili. Sasa najua, kwanini vita hii dhidi ya ufisadi ni vita ya kugombania hatima ya taifa letu!

  Azimio la Arusha lilipotangazwa lilikuwa na lengo la kuhakikisha kuwa utajiri wa nchi yetu unagawanywa kwa wananchi wa taifa hili. Lengo la Azimio halikuwa kugawana umaskini bali kugawana utajiri. Leo hii, wao wanagawana utajiri sisi tunatakiwa kugawana umaskini. Na wakati wowote tutakapojaribu kutaka kugawana utajiri wetu wao (wetu) ndivyo hivyo hivyo mapambano haya yatakuwa magumu zaidi.

  Kinyume na watu wengine wanavyoona, ninaliona sakata la Mengi na wale aliowaita kuwa ni “mapapa wa ufisadi” kuwa ni mapambano ya kugombania urithi wetu. Alichofanya Mengi na Mwakyembe kabla yake na wale waliochapisha ile taarifa ya “Tanzania’s Mafia” iliyoanzisha sakata hili la kwenye mtandao wa Jamiiforums.com ni kutukumbusha kuwa hatuwezi kamwe kuuachia urithi wa nchi yetu mikononi mwa kikundi cha watu wachache.

  Ni kile kile kilichofanywa na Dr. Slaa na kundi la wapinzani pale Mwembe Yanga walipotangaza ile Orodha ya Aibu ya mafisadi. Ni kile kile kilichopigiwa kelele Bungeni na kina mama Kilango na kina Mkumba. Ndiyo, ni sehemu ile ile ya mapambano ya kugombania urithi wetu. Kama watu wanafikiria hili ni suala la Mengi na Manji au Mengi na Rostam basi wanakosa kuiangalia picha nzima. Wanaona sehemu sehemu tu.

  Kwani, Mengi akikaa kimya, mama Kilango akifunga kinywa chake na kina Mwakyembe wakisalimu amri, haitakuwa mwisho wa mapambano. Watakuwa wamekubali kama walivyokubali wabunge wengine na watumishi wengine wa serikali kuwa sehemu ya utawala wa himaya ya kifisadi inayoongozwa na watu wanaokula kwa mikono miwili bila kunawa, na wanakula siyo minofu tu ya kuku, bali wanakula miguu na firigisi pia, tena wanakula bila kutaka waulizwe! Tukiwauliza wanatuelekeza kwenye kula utumbo!

  Ndugu zangu, yawezekana kuna mgongano wa kibiashara, yawezekana kuna chuki au kinyongo cha mambo fulani lakini hayo yote hayaondoi ukweli kuwa hatima ya taifa letu inashikiliwa na kundi la watu wachache; kundi ambalo halitaki kuulizwa, halitaki kuhojiwa na kwa hakika halitojitolea hata siku moja kutoa majibu zaidi ya kutisha watu na kutufanya tuishi kwa wasiwasi.

  Wapo watu wengi na wenye nguvu ambao majina yao yanajulikana, uwezo wao unazidi makisio na nafasi yao katika jamii ni sawa na wana wa mfalme fulani. Watu hawa wamechukulia kuvunjwa kwa Azimio la Arusha kama kibali cha wao kutunyonya kama wana akili fyatu. Na wanatufyonza kama mtu anayefyonza ganda la muwa na kuliacha kapi.

  Katika watu ambao wanaunda kundi hilo, kundi ambalo naamini lina nguvu kuliko inavyofikirika wapo wengi. Watu hawa hawana rangi, kabila au dini, ni wanyonyaji wa hali ya juu (nafahamu neno “mnyonyaji” kwa wengine ni geni). Wamejikita katika siasa na utendaji wa nchi yetu na katika kufanya hivyo wamejitengenezea himaya yao ya ufisadi. Chini yao wana watu ambao nimewaita makuwadi wa ufisadi na hivi karibuni tumeona siyo makuwadi tu wa ufisadi waliopo bali pia wametengeneza vikaragosi vya mafisadi!

  Miongoni mwa watu hao ambao wamechota utajiri wetu kama kutoka kisimani huku wakiturishia vimifupa kama mwizi anavyomrushia mbwa nyama ili asibweke sana wapo watumishi wa umma, wanasiasa na wafanyabiashara. Watu hao wana mtandao unaotisha, mtandao ambao ni imetengeneza pembetatu ya ufisadi (the triangle of corruption). Pembetatu hiyo inahusisha wafanyabiashara, wanasiasa na watendaji serikalini.

  Katika pembetatu hiyo kuna watu watatu ambao ni lazima niwataje hapa, yupo Sir. Andy Chande, yupo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na yupo Mbunge na mfanyabiashara maarufu Mhe. Rostam Abdulrassul Aziz (Igunga – CCM). Hawa watatu ndio naamini wanaunda mhimili wa ufisadi Tanzania (the axis of corruption). Chini yao kuna makumi na mamia ya watu ambao wanatekeleza majukumu yao mbalimbali kuhakikisha kuwa pembetatu hiyo ya ufisadi haivunjiki.

  Chini ya hawa watatu wapo ambao tunaweza kuwaita makuwadi wa ufisadi. Hawa ni watendaji serikalini ambao wamekubali kuuza haki yao na utu wao na uhuru wa Taifa letu kwa bei. Hawa ni wasomi waliokubuhu na watu “wazito” tu lakini kutokana na ahadi ya utajiri wa haraka haraka wamekubali kupinda sheria, kuvunja sheria na wakati mwingine kuiharibu sheria ili kurahisisha uporwaji wa mali za taifa letu. Ndiyo hawa waliorahisisha wizi wa Benki Kuu, ndiyo hawa waliofumba macho wakati nchi inabakwa na ndiyo hawa hawa ambao leo hii wengine wamefikishwa kizimbani. Lakini wengi bado wapo katika maofisi na taasisi mbalimbali.

  Hawa si watu wenye vyeo vya chini bali ni Wakurugenzi, Wenyeviti wa Bodi na watu wazito kwenye baadhi ya taasisi zetu nyeti. Wengi wa hawa waliteuliwa na kupewa nafasi zao za juu kutokana na maamuzi au mapendekezo ya mhimili wa ufisadi. Hawa sasa hivi wameshibishwa neema ya nchi yetu.

  Pamoja na hawa serikalini kuna makuwadi wengine kwenye siasa ambapo baadhi ya Watanzania wenzetu walikubali kununuliwa kwa bei ya chini ili waweze kupewa nafasi ya kushinda uchaguzi. Wengi wa hawa ni wanasiasa walionufaika kwa namna moja au nyingine na fedha za Mhimili.

  Katika kuwafikia watu hawa hakuna mtu mwenye nguvu kubwa kama Rostam. Rostam ametoa ufadhili kwa wanasiasa mbalimbali na kuwasaidia kushika nafasi zao walizonazo sasa. Katika kufanya hivyo amejihakikishia kundi kubwa la watu watiifu kwake. Watu hawa ambao amewasaidia wengi wamesainishwa misaada hiyo (kama alivyomfanyia Mtikila) na hivyo kujikuta hawana uwezo wala ubavu wa kusema kitu chochote dhidi ya Rostam.

  Katika kufanya hivyo utaona kuwa Rostam amepanga mojawapo ya safu ya makuwadi wake ambao siyo tu wana nafasi lakini pia wana nguvu kubwa mno. Tukumbuke kuwa aliyekuwa Meneja wa kampeni ya Urais wa Rais Kikwete ni Bw. Rostam Aziz (wakati huo akiwa pia mweka hazina wa CCM).

  Kwa nafasi yake hiyo Rostam alijua kila senti iliyokuwa inaingia na kutoka kwenye kampeni ya Kikwete. Ni yeye ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa katika kuchangisha fedha za kampeni hiyo. Tunapojiuliza fedha za kampeni za Urais wa Rais Kikwete zilizotoka wapi jibu analo Rostam!

  Kwa watu wanaokumbuka (kama mzee wenu hapa) Rostam alihusishwa na kutajwa na gazeti maarufu la Africa Confidential kuwa alipokea kiasi cha dola milioni 2 kutoka Oman kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi. Kiasi hicho ni kingine ya kila kilichotajwa na Christopher Mtikila kuwa kilitoka Iran (kupitia kwa Rostam) na ambacho kilitumiwa katika mchakato wa kumtafuta mgombea wa CCM.

  Vyanzo vyangu vya karibu kabisa vimenidokeza kuwa kiasi kilichotoka Oman kilitolewa na mfanyabiashara maarufu aitwaye Gen. Suleiman Al-Adawi ambaye alikuwa ni kigogo na msaidizi wa karibu wa Sultani wa Oman. Gen. Al-Adawi ni mzaliwa wa Zanzibar ingawa si raia wa Tanzania.

  Wakati huo Kikwete alitishia kulifungulia mashtaka gazeti hilo lakini hakufanya hivyo. Ukweli ni kuwa Kikwete hakujua fedha zimetoka wapi kwani alimuamini Rostam na hivyo hakukuwa na kesi siyo dhidi ya hilo gazeti tu bali hata Mtikila hakushtakiwa na hivyo kuwapa nguvu kuwa madai yao ni ya kweli.

  Hata baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani tunawaona watu mbalimbali waliohusiana na Rostam wakishika nafasi mbalimbali za utendaji na tena kwenye sehemu nyeti. Aliyetaka kugombea jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM ambaye alikuwa ni mtumishi wa Wizara ya Nishati na Madini Dr. Peter Kafumu aliyekuwa anaonesha kutoa ushindani mkubwa kwa Rostam alijikuta anakaa pembeni na kumpisha Rostam kwenye kiti hicho. Inadokezwa kuwa kwa kufanya hivyo atakumbukwa katika awamu mpya. Rostam akawa hana mpinzani kwenye kura za maoni!

  Baada ya kuchaguliwa Rais, Kikwete alimkumbuka Bw. Kafumu kwa kumteua kuwa Kamishna wa Madini. Hili inadaiwa lilikumbushwa na Rostam.

  Barua iliyotoka kwa Salva Rweyemamu (alikuwa mhariri wa Habari Corporation) kwenda kwa Rostam ilivujishwa karibu wiki mbili zilizopita. Katika barua hiyo ambayo imewafungua watu wengi macho inaonesha ni jinsi gani Rostam (RA kwa kifupi) amekuwa na nguvu mno. Katika barua hiyo ambayo sehemu kubwa ni jinsi gani Rostam aliacha kampuni aliyoinunua kufanya kazi kinyume cha sheria (bila kusajiliwa)) ilikuwa na sehemu ya mambo binafsi pia ambapo kimsingi Salva anaonekana akimkumbusha Rostam juu ya ahadi yake/zake kwake.

  Inaonekana katika barua hiyo Salva alikuwa hajakumbukwa na awamu hiyo mpya na akawa anashangaa inakuwaje baada ya jitihada zote (kwenye vyombo vya habari wakati wa kampeni) yeye hajakumbukwa. Akamhoji Rostam kama ndivyo wanasiasa wanawatenda wale watu walio karibu nao na waliowasaidia kushika madaraka. Wiki chache baadaye Salva Rweyemamu akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Rostam alimkumbuka tena.

  Aliyekuwa Wakili wa Vodacom (Mkuu wa kitengo cha sheria) na ambaye alisaidiwa na Rostam kuingia kampeni ya uchaguzi wa Ubunge kule Sengerema ni Bw. William Ngeleja. Wakati akiwa Vodacom mmoja wana hisa wa kubwa alikuwa (bado ni) Bw. Rostam Aziz. Baada ya uchaguzi wa 2005 ambapo Ngeleja alishinda Sengerema, Kikwete hakumsahau kwani alikumbushwa na Rostam. Kwanza kama Naibu Waziri na baada ya matukio ya mwaka jana kuupata Uwaziri kamili.

  (Hadi hapa tunawaona watu wawili wanaohusiana na Rostam wakiwa wizara moja).

  Mtu mwingine ambaye tunamkuta ni Bi. Badra Masoud ambaye aliwahi kuwa mhariri wa Habari Corporation (pamoja na kina Salva). Huyu alitoka Habari na kupata ajira kule DAWASCO na baadaye Tanesco kama Afisa Mawasiliano. Akiwa DAWASCO wengi watakumbuka ndiye aliyetangaza kukatiwa maji kwa wadeni sugu akiwemo Dr. Mwakyembe. Habari hizo zilikuja wiki chache tu baada ya ripoti ya Richmond Bungeni. Lengo lilikuwa kumchafua Dr. Mwakyembe kitu ambacho kilishindwa baada ya kuonekana kuwa jaribio hilo limeshindwa.

  Siyo yeye tu pale Tanesco bali pia Mkurugenzi wa Tanesco Dr. Idris Rashid ambaye naye ametoka huko Vodacom. Tukumbuke kuwa huko Vodacom Rostam ana hisa kubwa tu na hivyo kuwa na mtu kule Tanesco pia ni jambo la kuangalia sana kwa karibu.

  Katika sakata la Richmond na Dowans jina la Rostam linatajwa. Kinyume na taarifa yake ya juzi kuwa ripoti hiyo haikumtaja kwa jina. Tukumbuke vizuri kuwa katika mkutano wake wa waandishi wa habari mwaka jana Bw. Rostam alizungumza kana kwamba haijui kabisa kampuni ya Dowans na kuwa aliacha tu kadi yake tu na kuwa alienda tu kuomba kazi.

  Alinukuliwa kusema “Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi.. Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani” Maneno yake ya wakati ule yaliwaaminisha watu wengine kuwa Rostam haijui Dowans!

  Ukweli (ambao sasa tunaujua zaidi) ni kuwa Rostam ndiye aliyefanikisha ujio wa mmiliki wa Dowans na kumsaidia kuweza kuanzisha kampuni hewa ya Dowans Holdings SA ya Costa Rica. Mmiliki huyo ambaye nyaraka za BRELA zinamuonesha si mwingine bali ni rafiki wa karibu na mshirika wa karibu wa Rostam Gen. Suleiman Al-Adawi ambaye ana undugu na mahusiano ya karibu ya kifamilia na Watawala wa Falme za Kiarabu. Rostam hakuwa mkweli wakati ule na kama angetaka kuwa mkweli angesema wazi mapema mahusiano yake na watu wa Dowans!

  Naweza kuendelea kuandika mifano mingine mingi na watu wengine ambao Rostam amewasaidia katika kampeni za uchaguzi (nina majina karibu ya wabunge 40 ambao “wako mfukoni” mwake). Wabunge ambao ninawaita kuwa ni makuwadi wa ufisadi. Hawa msitegemee hata siku moja kuwaona wanapiga vita ufisadi au kupiga kelele juu ya uporaji wa mali zetu.

  Jinsi ya kuwagundua wabunge hawa ni pale wanapozungumzia ufisadi. Wao wanasikika wakisema “vita ya ufisadi ni vita yetu sote”. Utawasikia wakisema “mtu asitumie vita ya ufisadi kujinufaisha kisiasa”. Kamwe hata hivyo hutawasikia wakipigia kelele Kagoda, EPA au kutaja majina ya watu ambao wanahusika na ufisadi. Watasikika kwa haraka kumlaani Mzee Mengi kwa jina lake lakini hawatasika kumtuhumu Rostam au vigogo wengine kwa majina yao.

  Chini ya hao (makuwadi wa ufisadi) utawakuta vikaragosi vya ufisadi. Hili ni kundi kubwa la waandishi wa habari, na watendaji wa ngazi za chini wa CCM na wapambe wengine au mashabiki ambao kila mabwana zao wanapoguswa hufanya haraka kuwasafisha na kuwatetea. Wengine hufunga safari toka mikoa ya mbali ili waje wasikike. Vikaragosi hawa wapo hadi kwenye timu zetu za mpira na ambao “mfadhili” wao akiguswa wanakuja na kelele kuwa anaonewa ingawa wengine tunajua yaliyotokea Mbagala wiki iliyopita yawezekana kabisa kuhusishwa na biashara za mfadhili huyo!

  Vikaragosi hawa wa ufisadi ni wale ambao bila haya wala soni wako tayari kuuza utu wao, hadhi yao na heshima yao ili wafadhiliwe. Ndiyo watu wa hatari pia katika mapambano haya kwani bei yao inajulikana. Ujumbe wetu kwa hawa wote (Pembetatu ya ufisadi, Mhimili wa ufisadi, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vya ufisadi) ni kuwa sasa imetosha iachieni nchi yetu! Mmeishikilia vya kutosha na sasa mnataka kututumikisha milele. Mmeuza urithi wetu na utajiri wetu mmegawana; leo mnataka sisi tugawane umaskini wetu wakati nyinyi mnamegeana utajiri wetu. Sasa yatosha!

  Labda niwakumbushe mbiu ile ya Azimio la Maskini!

  “Tumeonewa kiasi cha kutosha, Tumenyonywa kiasi cha kutosha,
  Na tumepuuzwa kiasi cha kutosha; Unyonge wetu ndio umetufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge wetu ili tusionewa tena, tusinyonywe tena”!

  Ni mimi: Mwanakijiji@mwanakijiji.com
   
 2. D

  Dotori JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  MMJ,
  Nice piece! How does EL fit in this frame?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,387
  Trophy Points: 280
  nadhani atakuwa katika kundi la RA..
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  May 6, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  My dear fellow countrymen,  This is the first of what I hope will be a series of regular letters to the 40 million Good People of this Great Nation. Being my first letter, I would like to deal with an issue of utmost concern to all, something that touches every life in the nation. Corruption is a menace that is posing a great challenge to our development, a torn in the flesh of our national conscience compromising the rule of law and becoming an undesirable way of life and governance that is undermining our democratic values. I would spend much energy and time addressing what I think should be lasting solutions to this somewhat incurable disease that is more dangerous than the notorious Swine flu.  Many have talked passionately and elaborately about this problem with only a few suggesting the ways out. Lamentation will not effect any change unless we get to the root cause, cure it and remove all the signs and symptoms. I would be using this space to do exactly that. We have to come together to end this problem even though we did not create it but we have all contributed to project it to the current level.  Very often, when we talk about corruption, we all tend to look at the other side, it something others do. Someone else is corrupt. It's what the politicians do, it's what the bosses do and all the state and local government houses; and the parliaments. Yes they do but if they are the only corrupt beings, then only an insignificant fraction of our society is corrupt. We are all quick to judge as corrupt, the TRA and all organizations that have T stuck in them such as TPA , TANESCO, TEMESA, TAESA, TANAPA, TANROADS, TBC, …. Yes! You are right. They are all corrupt but corruption is not limited to them. If corruption is only limited to what we see in Lowassa , Mkapa, Rostam , Mengi , and Dowans , I would be the first to thrown stone at them in the open. No! It is far beyond this.  So what is corruption? Nice question! Who is corrupt? Still a good question!! How did we get there? A better question!!! And how do we get out of this mess? Wow! You've just ask the best question!!!! My letter will deal with all these questions.  According to Oxford English dictionary, corruption is dishonest or illegal behaviour or the willingness to act dishonestly in return for money or personal gain. If I have to expand this and bring it home, then corruption is a dysfunctional system or institution in which government officials, political officials and private employers or employees seek illegitimate personal gains through actions such as bribery, extortion, nepotism, graft, embezzlement and abuse of corporate power by managers against the shareholders or consumers. Corruption usually facilitate organized crime and criminal activities such as money laundering, fraud, drug trafficking and all other forms of trafficking.  A government is susceptible to political corruption where access to politics is organized with limited transparency, limited competition and directed towards promoting narrow interests featuring stuffs like kleptocracy – rule by thieves inflating contracts and electoral process manipulation and rigging.  Who is corrupt?  This is a practical question that I would like to answer practically. In answering this question, I would like to ask you a few personal questions based on your past experiences. You'll need to do some personal appraisal. If you answer YES to any of the questions, it can not be said that your are totally immune to corruption. If you answer is NO to all the question, I may have to bring a lie-detector to run the test on you by myself and if you still get a perfect NO, be sure that I'd recommend you to Transparency International (TI) in Berlin, Germany for a special anti-corruption award.  · Have you ever embezzled i.e. wrongfully taken, stolen or misappropriated a fund or office entrusted in your care. This include sending an official employee e.g. your official driver on a private errand? YES/NO  · Have you ever favoured or received favour from relatives, friends and associates in employment, judgement, award of contract or admission? YES/NO  · Have you ever made an illegitimate gain in employing someone or given a contract to a person other than the most competent candidate? YES/NO  · Have you ever been ‘settled', taken a graft or a kickback i.e. a share of misappropriated funds from overpriced purchases or allocated from an organization involved in inflated contract? YES/NO  · Have you ever rigged an election or accepted an elected office through a fraudulent election? YES/NO  · Have you ever inflated the price of an item purchased in your official capacity or inflated the price of a contract?  · Have you ever used your official power illegitimately as means to an end, to punish or promote a person or to trump-up charges against enemies? YES/NO  If your answer is outright NO, congratulation! You have not contributed to corruption in the country but wait! Before you start uncorking the Champagne or giving testimony in your local church of your incorruptibility, let me ask you the last question.  · Have you ever given any form of bribe to any one or taken one. YES/NO  The answer to this may require a real soul-searching. Think of the popular Tshs 20000 at the checkpoint substituting vehicle documents, 30000 at the airport for easy passage, 300000 to the Immigration officer for quick passport, Tshs 20000 at Namanga and Tanga border to make the Custom men blind, 1000000 to have a reduced tariff or duty, 3000000 to the Bunge Committee, Tshs 60000000 to NEC to change the will of the people, Tshs 400000000 to the Presidency for the Mineral block……………. Wow! Everything has a price.  Really, corruption can be graded. Some are more harmful than the others but every bit of it is detrimental to our system. We are where we are today as a result of all the forms of corruption at all level and we are all have to take responsibility and flush it out of our national life.  How did we get this low?  No nation is perfect. No country is 100% protected from corruption. In all great nations, corruption is not visible and acceptable. It goes on underground and perpetrated by only an infinitesimal fraction of the society and who are brought to book whenever they are caught. Tanzania was like this until the mid ‘60 when we had our first shot at electoral corruption.  Ever since the mid ‘60s, corruption has been dwelling with us and all successive governments made the fight against corruption a core point of their policies. We never really had a large scale corruption until the regime of Benjamin Mkapa , A News Maker turned president. The government was viewed as very corrupt and incompetent by virtually all sectors of Tanzanian society. Are News Makers incompetent to put their Making experiences and skills to ruling a nation?  So how do we get out of this mess called corruption?  Whatever has a beginning must definitely have an end. Life always present us with choices. We have two choices in ending this endemic vice that has apparently caused us to live a discounted life with an ever diminishing standard of living. It has eroded our national pride and sense of belongingness leaving us with nothing other than a collapsed system with brain drain and unemployment as main features and now threatening to completely mortgage our future.  Much sooner than later, we will be left with a violent change is we fail to make a peaceful change now! Dodoma should know that those who make peaceful changes impossible, make violent changes inevitable.  Most Tanzanians hope and pray to live in a country that will be free from corruption and many of us believe that a cause worth living for is worth dying for. We will be left with no alternative than this bloody revolution if we fail to act on a peaceful resolution.  The peace resolution will require a collective effort by all and sundry to be spearheaded by the government. Needless to say that with this depth of corruption, no single person or organisation has the moral ability and capability to fight it because when you do a background check, you will find out that those empowered by law to fight corruption are more deeply involved in corruption than those they want to check. The government has to provide an enabling environment by making zero tolerant policies (that must be strictly adhered to) against corruption and by leading through example that will flow down the ladder.  President Kikwete must show that he is serious about fighting this corruption and if he succeeds in just only this, posterity will place him on the right side of history.  Everyone has to give up all corrupt practices or be brought to book and whenever we see something, we have to say something as demanded by TAKUKURU.  Tanzania also need to get back all the stolen money and looted treasures especially considering the present economic situation. We thereby need to set up a recovery commission using the South African model of Truth and Reconciliatory Commission (TRC) in order to get the loots back so that we can have a fresh start.  TRC was a court-like body assembled in South Africa after the abolition of apartheid. Anyone who felt that he or she was a victim of its violence was invited to come forward and be heard. Perpetrators of violence could also give testimony and request amnesty from prosecution. Despite some flaws, it is generally thought to have been successful. It was seen by many as a crucial component of the transition to full and free democracy in South Africa.  A recovery commission will enable people to come out voluntary and return back their loots in exchange for amnesty and only those who refuse to cooperate will be brought to justice.  If we fail to act now, the good people of this great nation are becoming impatient and the forceful change is imminent. A word is enough for the wise and the fact remains that "The future will have no pity for those men who have the exceptional privilege of speaking the word of truth to their own oppressors but who have taken attitude of passivity, mute indifference and sometimes of cold complicity". Frantz Fannon  God Bless Tanzania !  Tanzania Go Better!  Yours Sincerely,
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Weka credit wewe, sio una plagiarize tu

  Corruption: How did we get this low? And which way out? – An open letter to a great Nation - by Rufus Kayode Oteniya - modernghana.com/nigeria news

  Corruption: How did we get this low? And which way out? – An open letter to a great Nation - by Rufus Kayode Oteniya

  My dear fellow countrymen,This is the first of what I hope will be a series of regular letters to the 140 million Good People of this Great Nation. Being my first letter, I would like to deal with an issue of utmost concern to all, something that touches every life in the nation. Corruption is a menace that is posing a great challenge to our development, a torn in the flesh of our national conscience compromising the rule of law and becoming an undesirable way of life and governance that is undermining our democratic values. I would spend much energy and time addressing what I think should be lasting solutions to this somewhat incurable disease that is more dangerous than the notorious Swine flu.

  Many have talked passionately and elaborately about this problem with only a few suggesting the ways out. Lamentation will not effect any change unless we get to the root cause, cure it and remove all the signs and symptoms. I would be using this space to do exactly that. We have to come together to end this problem even though we did not create it but we have all contributed to project it to the current level.

  Very often, when we talk about corruption, we all tend to look at the other side, it something others do. Someone else is corrupt. It's what the politicians do, it's what the bosses do in Aso Rock and all the federal, state and local government houses; and the parliaments. Yes they do but if they are the only corrupt beings, then only an insignificant fraction of our society is corrupt. We are all quick to judge as corrupt, the NNPC and all organizations that have N stuck in them such as PHCN, NERC, NPA, NA, NN, NAF, NPF, NI, NC, NFA, FAAN, CBN, NDIC, NDCC, INEC…. Yes! You are right. They are all corrupt but corruption is not limited to them. If corruption is only limited to what we see in Ibori, Aondoakaa, the hairdresser Etteh, Lucky, Tafa, Alam, Edem, Alaibe, Dariye, Odili, Turaki, Atiku, Yar'Adua, Obasanjo, Abacha, Babangida, Abdulsalam, Siemens, Willbros, Halliburton and African Petroleum, I would be the first to thrown stone at them in the open. No! It is far beyond this.

  So what is corruption? Nice question! Who is corrupt? Still a good question!! How did we get there? A better question!!! And how do we get out of this mess? Wow! You've just ask the best question!!!! My letter will deal with all these questions.

  According to Oxford English dictionary, corruption is dishonest or illegal behaviour or the willingness to act dishonestly in return for money or personal gain. If I have to expand this and bring it home, then corruption is a dysfunctional system or institution in which government officials, political officials and private employers or employees seek illegitimate personal gains through actions such as bribery, extortion, nepotism, graft, embezzlement and abuse of corporate power by managers against the shareholders or consumers. Corruption usually facilitate organized crime and criminal activities such as money laundering, fraud or 419, drug trafficking and all other forms of trafficking.

  A government is susceptible to political corruption where access to politics is organized with limited transparency, limited competition and directed towards promoting narrow interests featuring stuffs like kleptocracy – rule by thieves inflating contracts and electoral process manipulation and rigging.

  Who is corrupt?
  This is a practical question that I would like to answer practically. In answering this question, I would like to ask you a few personal questions based on your past experiences. You'll need to do some personal appraisal. If you answer YES to any of the questions, it can not be said that your are totally immune to corruption. If you answer is NO to all the question, I may have to bring a lie-detector to run the test on you by myself and if you still get a perfect NO, be sure that I'd recommend you to Transparency International (TI) in Berlin, Germany for a special anti-corruption award.

  · Have you ever embezzled i.e. wrongfully taken, stolen or misappropriated a fund or office entrusted in your care. This include sending an official employee e.g. your official driver on a private errand? YES/NO

  · Have you ever favoured or received favour from relatives, friends and associates in employment, judgement, award of contract or admission? YES/NO

  · Have you ever made an illegitimate gain in employing someone or given a contract to a person other than the most competent candidate? YES/NO

  · Have you ever been 'settled', taken a graft or a kickback i.e. a share of misappropriated funds from overpriced purchases or allocated from an organization involved in inflated contract? YES/NO

  · Have you ever rigged an election or accepted an elected office through a fraudulent election? YES/NO

  · Have you ever inflated the price of an item purchased in your official capacity or inflated the price of a contract?

  · Have you ever used your official power illegitimately as means to an end, to punish or promote a person or to trump-up charges against enemies? YES/NO

  If your answer is outright NO, congratulation! You have not contributed to corruption in the country but wait! Before you start uncorking the Champagne or giving testimony in your local church of your incorruptibility, let me ask you the last question.

  · Have you ever given any form of bribe to any one or taken one. YES/NO

  The answer to this may require a real soul-searching. Think of the popular N100 at the checkpoint substituting vehicle documents, N1000 at the airport for easy passage, N10,000 to the Immigration officer for quick passport, N100,000 at Idi-Iroko and Seme border to make the Custom men blind, N1,000,000 at Tin-Can to have a reduced tariff or duty, N10,000,000 to the Senate Committee, N100,000,000 to INEC to change the will of the people, N1,000,000,000 to the Presidency for the Oil block……………. Wow! Everything has a price.

  Really, corruption can be graded. Some are more harmful than the others but every bit of it is detrimental to our system. We are where we are today as a result of all the forms of corruption at all level and we are all have to take responsibility and flush it out of our national life.

  How did we get this low?
  No nation is perfect. No country is 100% protected from corruption. In all great nations, corruption is not visible and acceptable. It goes on underground and perpetrated by only an infinitesimal fraction of the society and who are brought to book whenever they are caught. Nigeria was like this until the mid '60 when we had our first shot at electoral corruption.

  In 1965 elections, the Action Group (AG), a party led by late Chief Obafemi Awolowo was outmanoeuvred for control of Nigeria 's Western Region by the Nigerian National Democratic Party, an amalgamation of conservative Yoruba elements backed heavily by the Federal Government amid dubious electoral circumstances. This perceived corruption of the electoral and political process as well as other forms of corruption were cited as the factors leading in 1966 to back-to-back military coups.

  Ever since the mid '60s, corruption has been dwelling with us and all successive governments made the fight against corruption a core point of their policies. We never really had a large scale corruption until the civilian regime of Alhaji Shehu Shagari, a grade 2 teacher turned president. The Shagari government was viewed as very corrupt and incompetent by virtually all sectors of Nigerian society. Are teachers incompetent to put their teaching experiences and skills to ruling a nation? Yar'Adua is a former teacher.

  Under Shagari's government between 1979 to 1983, politicians like Alhaji Umaru Dikko, the then minister of transport was said to be corruptly making up to a million naira (then a naira was more than a dollar) daily from importation of rice and other commodities; and import duties fraud. The government was also re-elected through a massively fraudulent election that caused a lot of unrest in some south west states.

  Most of the Shagari era's deep corrupt practices were reversed by Mohammadu Buhari/Idi-Agbon's government through the War Against Indiscipline programme (WAI). It was the only government on record apart from the short-lived Murtala Mohammed's government that showed seriousness in fighting corruption. Other governments played only lip service. This high-handed government that came in January 1984 was overthrown in 1985 by Ibrahim Babangida to the relieve of many.

  Most people believe that the Babangida's government should be credited with institutionalizing corruption in our system. Babangida himself was the architect of the present miserable state of the nation and some call him the author and the finisher of corruption in the country. It can be correctly said that "the seed of corruption was planted by Babangida, watered by Abacha, nurtured to maturity by Abdulsalam, consolidated by Obasanjo and harvested by Yar'Adua". The successive governments keep building on the brawny foundation of corruption Babangida laid and this explains why the situation progressively get worse. The zenith of this government's corrupt practices was Babangida's annulment of June 12, 1993 election which was adjudged by most people as the most free and fair election in the history of Nigeria and presumably won by Alhaji Moshood Abiola a philanthropic business mogul and government contractor.

  So how do we get out of this mess called corruption?

  Whatever has a beginning must definitely have an end. Life always present us with choices. We have two choices in ending this endemic vice that has apparently caused us to live a discounted life with an ever diminishing standard of living. It has eroded our national pride and sense of belongingness leaving us with nothing other than a collapsed system with brain drain and unemployment as main features and now threatening to completely mortgage our future.

  Much sooner than later, we will be left with a violent change is we fail to make a peaceful change now! Abuja should know that those who make peaceful changes impossible, make violent changes inevitable.

  Most Nigerians hope and pray to live in a country that will be free from corruption and many of us believe that a cause worth living for is worth dying for. We will be left with no alternative than this bloody revolution if we fail to act on a peaceful resolution.

  The peace resolution will require a collective effort by all and sundry to be spearheaded by the government. Needless to say that with this depth of corruption, no single person or organisation has the moral ability and capability to fight it because when you do a background check, you will find out that those empowered by law to fight corruption are more deeply involved in corruption than those they want to check. The government has to provide an enabling environment by making zero tolerant policies (that must be strictly adhered to) against corruption and by leading through example that will flow down the ladder.

  President Yar'Adua must show that he is serious about fighting this corruption and if he succeeds in just only this, posterity will place him on the right side of history.

  Everyone has to give up all corrupt practices or be brought to book and whenever we see something, we have to say something as demanded by EFCC.

  Nigeria also need to get back all the stolen money and looted treasures especially considering the present economic situation. We thereby need to set up a recovery commission using the South African model of Truth and Reconciliatory Commission (TRC) in order to get the loots back so that we can have a fresh start.

  TRC was a court-like body assembled in South Africa after the abolition of apartheid. Anyone who felt that he or she was a victim of its violence was invited to come forward and be heard. Perpetrators of violence could also give testimony and request amnesty from prosecution. Despite some flaws, it is generally thought to have been successful. It was seen by many as a crucial component of the transition to full and free democracy in South Africa .

  A recovery commission will enable people to come out voluntary and return back their loots in exchange for amnesty and only those who refuse to cooperate will be brought to justice.

  If we fail to act now, the good people of this great nation are becoming impatient and the forceful change is imminent. A word is enough for the wise and the fact remains that "The future will have no pity for those men who have the exceptional privilege of speaking the word of truth to their own oppressors but who have taken attitude of passivity, mute indifference and sometimes of cold complicity". Frantz FannonRufus Kayode Oteniya is a Milan , Italy based businessman and social affairs commentator.
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  1. Tofauti ni ipi kati ya mhimili na pembe tatu? Mgawanyo wa nguvu hakuna?

  2. Pili hao walioitwa pembe tatu? inamaanisha wao ndio matajiri wakuu! sioni tofauti yao na makuwadi, kwani faida ya unyonyaji haibaki mikononi mwao!

  3. Azimio la arusha wameliweka chini ya uvungu, halijafa ila halipaswi kuoneka, ili waweza kuwa makuwadi wazuri - wasio na mipaka wala utaifa-. Wangejaribu basi kuwa pebari wa kitaifa - lahasha hilo wakalikana kwani zinahitaji fikra na msimamo, wakakimbia kirahisi - ukinipa nakata cha juu.

  4. Maskini, bado kupiga mbiu - kwani anamatumaini, inamoyo wa imani, katengwa na mifumo ya kijamii inayoamua elimu ni bora zaidi ya kilimo, waishio vijijini ni duni. Watu wakati wamehamaki, kwa kuwa wanautambuzi, lakini hamaki yao imekitwa na ubinafisi - kiongozi yule hafai kwani elimu yake duni, nilisoma nae alikuwa kilaza, kapendelewa na fulani, ni mshikaji wa fulani, sio kwamba hafai kwa sababu hana maslahi ya umma hafai akilinganishwa na mimi.

  5.Tukiondoka katika umimi, na kufikiria taifa kwa ujumla wake mbiu ya maskini itapigwa na itapigika. Tukibaki katika ukati wetu, nguvu zetu za fikra peke yake hazitangoa wenye fedha. Tukiunganisha nguvu za fikra na nguvu za umma, mbio ya maskini itapigika tu na wateule watacheza dede! Lakini kabla ya hapo tutamiliza soli!
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hakuna chochote hapa ,Sultani CCM amekamata katiba ya Nchi ,mtapanga mkipangua wala hababaiki ,labda wananchi wapewe maelekezo ya kufa kupona lakini wasimupe CCM nafasi ya kukwiba kura ama zao ama zetu ,nchi haitakalika kama kutatokea wizi ,hio ndio dawa ya kupambana na CCM vinginevo kwa kupanga mahesabu itakuwa ni kumpigia mbuzi gitaa.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,508
  Trophy Points: 280
  i miss these guys ! shy and blue ray
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,304
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  Tanzania ya viwanda ndio hii
   
Loading...