Mbinu za kuwapata majambazi Rufiji na Mkuranga

m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
979
1,353
1. Lazima ikaguliwe nyumba moja baada ya nyingine kuwabaini wahusika.

2. Kuwepo na vizuizi toka kijiji kimoja kwenda kingine kwa ukaguzi makini.

3. Pia mabalozi wa nyumba 10 waeleze kama wanawafahamu wananchi wao kwenye maeneo yao.

4. Askari waache kulinda kwa mazoea sasa watambuwe kuwa wanawindwa na majambazi hivyo lazima walinde wakipeana hatua kadhaa toka alipo askari mmoja kumfikia mwengine wasirundikane.

5. Askari kanzu wenye silaha za bastola waongezeke kwa wingi maeneo tajwa.

6. Zipigwe kura za kuwabaini wahusika wa mambo haya.
 
kwakweli kuna kitu kimeniudhi sana Juzi, nilikuwa natoka lindi tumefika mkuranga askari kasimamisha gari then anaanza kutafuta mtu kwa kutumia picha iliyo kwenye simu kwa kama 20 minutes, then akaamuru bus liende kituoni nako vile vile askari wanaingia na simu kutafuta mharifu for about 30minutes.... mbinu kama hizi ni rahisi waharifu kuambiana namna ya kuwakwepa polisi.
 
Kwa akili yako wauaji bado wako maeneo hayo,tena nyumbani


!
!
hawa ndio wale wanaofikiri elimu ni ufunguo wa maisha wakati kwa sasa milango haitumii funguo bali password. Achana nae mkuu kachelewa sana huyu mleta mada. Watu waue polisi halafu wabaki hapo hapo wangojee kukamatwa
 
Aah hii Mada bwana, kwaio unadhani wauaji bado wako mkuranga?
 
Hapo safi,lakini kutumia askari waliovaa kanzu? hayo majambazi na yenyewe yatavaa kanzu halafu kanzu ndio zitakuwa target,maustadhi wetu wataacha hata kuzivaa.
Haha "askari kanzu" ni wale wasiovaa uniform wanafuga mindevu nywele na wachafuwachafu sazingine
 
Hapo safi,lakini kutumia askari waliovaa kanzu? hayo majambazi na yenyewe yatavaa kanzu halafu kanzu ndio zitakuwa target,maustadhi wetu wataacha hata kuzivaa.
Mkuu inaelekea kipindi cha nahau uliruka dirisha, Askari kanzu unajua maana yake?
 
Back
Top Bottom