Mbinu chafu za maadui wa Rais Magufuli

Mbinu chafu za maadui wa Rais Magufuli

Nimekuwa nikisoma "comments" nyingi sana humu JF zinazohusu kutekwa kwa Roma Mkatoliki na nyingi kati ya hizo comments zinamlaumu Rais Magufuli na Serikali yake. Hata alipopotea Ben Saanane, watu walikuwa wanaishutumu Serikali ya Rais Magufuli.

Mimi ningependa kuhoji; hivi ninyi mnaoishutumu Serikali mna uhakika gani kuwa Serikali ndiyo inahusika na mambo haya?
Binafsi naamini na ninatambua wazi kuwa hakuna uthibitisho wowote ule unaoonyesha kuwa Serikali ndiyo inahusika.

Serikali yoyote ile duniani huwa na maadui. Hakuna Serikali isiyokuwa na maadui hapa duniani. Hata Serikali yetu inayoongozwa na Rais Magufuli pia ina maadui. Maadui hawa hawapendi kuona Rais wetu Magufuli anaendesha nchi hii kwa amani na mafanikio. Maadui hawa watafanya kila wawezalo ili kumchafua Rais na Serikali yake mbele ya macho ya Watanzania na mbele ya jamii ya kimataifa pia.

Inavyoonekana sasa hivi, maadui hawa wanatumia nafasi iliyojitokeza sasa hivi hapa nchini au mwanya uliojitokeza kufanya uhalifu kwa kisingizio kuwa Serikali ndiyo inahusika. Kuna watu wako tayari hata kutoa roho za wenzao ili mradi tu malengo yao yafanikiwe.

Mimi nina mashaka sana tena sana na baadhi ya vyama vya upinzani hapa Tanzania. Vyama hivi vikiongozwa na chama fulani hivi, vinaendesha siasa chafu sana hapa nchini ili tu kuhakikisha taswira safi ya Serikali ya Rais Magufuli inachafuliwa kwa gharama yoyote ile.

Kuna baadhi ya waliokuwa viongozi wakubwa tu hapa nchini waliokuwa kwenye madaraka nyeti, sasa hivi wako kwenye upande wa upinzani na viongozi hawa siyo "MALAIKA". Ni watu wenye uchu wa madaraka, ni watu wenye mbinu chafu sana za kutafuta madaraka, ni watu wa kufanya siasa za "matukio" na "maigizo". Watu hawa ni hatari sana kuliko tunavyofikiria, ni hatari sana tena sana.

Nafahamu kuna baadhi yenu mtatukana sana hapa, lakini amini nawaambieni, ukweli utafahamika na mtabaki midomo wazi.

Kila serikali hapa duniani ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha uwepo wa serikali husika. Hata Serikali yetu pia ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha usalama wa nchi hii, lakini siyo Roma wala siyo Ben saanane. By the way who is Roma Mkatoliki to the government? Roma is no body.

Kama ni kuwashughulikia watu, basi mimi nafikiri Lissu angekuwa wa kwanza, tena siku nyingi sana na siyo Ben Saanane au Roma. Kama ni kuwafunga midomo watu, basi Lema angeshapotezwa siku nyingi sana na siyo Roma. Msijidanganye, kati ya hao niliowataja hakuna mwenye uwezo wa kujificha ama kujilinda iwapo Serikali itaamua kwa dhati kumshughulikia na kumpoteza mazima! Hakuna mwenye uwezo wa kujilinda hata awe nani.

Watanzania kuweni makini sana na mambo yanayofanyika sasa hivi hapa nchini. Msikimbilie kumtukana na kumlaumu Rais Magufuli kumbe chawa anayewatafuna mmembeba wenyewe kwenye nguo zenu.

Serikali inalitambua hili na inajua ni nani anayehusika na mchezo huu mchafu na It's just a matter of time, kila kitu kitajulikana. Serikali ina mkono mrefu sana na mbinu hii inayotumiwa na "MAADUI" imeshajulikana na sasa hivi kuna kazi maalumu "inaendelea". Kazi maalumu ambayo wewe au mimi hatutatangaziwa au kujulishwa ni namna gani inafanyika.

Rais Magufuli, wewe piga kazi na wala usiyumbishwe na mbinu chafu za hawa wahuni wachache wanaotaka kukumaliza. Tuko pamoja na wewe Rais wetu mpendwa.

By Son of Gamba.
Leo unakuja na maoni gani na kupatikana kwa hawa watu na uhusikaji wa serikali?
 
Naona kuna watu huwa hawataki kuona ukweli unasimama wako tayar kufanya figisufigisu ionekane watawala hawahusishwi na tuhuma hizi iko wazi huwez kuniambia mtoto wako ametekwa na kabla ya j 3 atapatikana akiwa hai hii inatosha kabisa kukushikilia wewe kwakuwa unafaham A-Z kuhusu mtoto wangu,siku nyingine ili ukitaka ku-win game kama hii unapaswa kutoa majibu ya kufuatilia suala hilo bila kutoa uhakika walini atapatikana na siku ukiamua kumleta utaweza kupata sifa kwa ufanikishaji wako kosa alilofanya bashite ni kuahidi atapatikana ndani ya muda flani hili ni kosa la kimkakati ni sawa na yule wa magogoni aliyesema kuwa Kinana amemtuma india kwa matibabu ya siku 14 yaani mtu na babaake ni zero kabisa kimkakati .
Mkuu ujue mwisho wa ubaya ni Aibu. Jana Maliyamungu Bashite alijikuta karopoka bahati mbaya na anajutia kauli yake kwani ni kauli ilitokana na mungu kuwaonyesha watanzania juu ya mabaya yao, ni mungu alifunua bila kujijua pia ameogopa baada ya kusikia mmiliki wa studio kaleta mashehe kuja kusoma Elibadili, pressure ikampanda kaamua kuwaachia hataka japo kikundi chake kinachoongozwa na Le mutuz kinajitahidi kumtetea nina imani wataambulia Aibu tu.
 
umeeleza vizur tatizo umeegemea upande mmoja sana.


kama roma is no body sawa.



swalii ney wa mitego je?


Walivyotumia nguvu kubwa kwa ney wamitego mpaka rais kuingilia kati. lazima wanainchi tuwe na mashaka na serekali.

angalia logic usiendeshwe na hisia kama mtoto wa kike.
Kwann ney si kakamatwa na polisi live kwa ajili ya nyimbo na siri hamna sasa mm nadhan ww ndo unaongozwa na hisia za kidada
 
Le mutuz jiandae kudaiwa pesa na Maliyamungu Daud Bashite makonda kwani kazi aliyowatuma mtandaoni mmefeli watanzania wameamka hawakubali propaganda zenu kamwe.
 
acheni ujuaji, hakuna anaye jua Roma kakamatwa na nani, lawama zinakuja kwa serikali kwa nn ina shindwa ku react kwenye hii ishu!? ila mpaka Roma au walio mteka wapatikane ndio ukweli utajulikana, Polisi na vyombo vya usalama wafanye kazi yao wamtafute
Imeshindwa vip kureact?fafanua labda au futa comment yko mapema ukijua ni pumba
 
ujinga nipale inapozani lisu na Lema ni hatali kwa selikali kukiko roma(wasanii)..wimbo mmoja unaoikashifu serilkali una impact kubwa mmno kuliko mikutano 200 ya lema na lisu....by theway kukosoa serikali ni jambo la kawaida isichukuliwe kama ni uadui ...kama hakuna jira uchumi ni mbaya nk tunapasa kusema na tusikilizwe
Hizi pumba zko dui
 
Nay alitekwa kwa siri au alikamatwa hadharani na kila mtu aliona.

Tumia akili zako kufikiri mambo kwa kina.

Kwa taarifa yako, Roma hajakamatwa na Polisi, ametekwa na "wahuni" wenye nia chafu dhidi ya Rais.
Inabidi uisaidie polisi, uwataje hao wahuni kijana.
 
Nay alitekwa kwa siri au alikamatwa hadharani na kila mtu aliona.

Tumia akili zako kufikiri mambo kwa kina.

Kwa taarifa yako, Roma hajakamatwa na Polisi, ametekwa na "wahuni" wenye nia chafu dhidi ya Rais.
Ni kweli alitekwa na wahuni wakiongozwa na Bashite ambaye kapewa kazi iyo na ********
 
Tunakoenda sasa Maliyamungu Daud Bashite akachukua wake za watu live bila kikwazo na endapo utaleta upinzani utatekwa
 
Kwa akili zako kutekwa kwa ROMA ni crisis? Who is ROMA by the way?

Watu wangapi wamepotea hapa Tanzania? Na siyo Tanzania tu, duniani kote watu wanapotea kila siku.
Inaonekana huna ufahamu na wala huelewi ya masuala ya kiusalama.

Katika masuala ya kiusalama anything threatening human life is a crisis. Crisis haitegemei uwingi wa watu bali ni hatari ya uwezekano wa kupotea maisha ya mtu, watu au kikundi cha watu. Ndiyo maana katika mataifa yanayothamini uhai wa binadamu, kutekwa kwa mwananchi mmoja tu ni crisis. Italazimu vyombo mbalimbali vya kiusalama kukutana na kujadili na kuona uwezekano wa kuyaokoa maisha yaliyopo kwenye hatari ya kupotea.

Mtu au watu wakifa inaweza isiwe crisis kama hakuna hatari ya wengine kupoyeza maisha. Unajua psychological impact inayotokana na mtu kuwa mateka? Ndiyo maana magaidi kuna wakati wanamteka raia mmoja tu na kutoa masharti. Wanajua jinsi tukio hilo linavyoweza kufadhaisha jamii. Tofauti na wakimwua.
 
Ni kweli alitekwa na wahuni wakiongozwa na Bashite ambaye kapewa kazi iyo na ********
Bashite Maliyamungu amekuwa hatari yupo radhi afanye chochote ili mladi awapakazie chochote Wapinzani lolote lakini safari hii atadunda.
 
Watu wataachaje kuwa na mawazo ya kinyume kama yule aliyemnyooshea Nape bastola hajajulikana, waliompoteza Saanane hawajulikani, na watu wanaendelea kutekwa? Mtu yeyote lazima apate mawazo ya kulaumu vyombo vya dola au serikali inayovisimamia.
 
umeeleza vizur tatizo umeegemea upande mmoja sana.


kama roma is no body sawa.



swalii ney wa mitego je?


Walivyotumia nguvu kubwa kwa ney wamitego mpaka rais kuingilia kati. lazima wanainchi tuwe na mashaka na serekali.

angalia logic usiendeshwe na hisia kama mtoto wa kike.
Ahhhhh logic u naelewa kweli we logic Embu tengeneza hixo syllogism zako .ney alikamatwa na polisi. Ney kama roma naye ni msanii
Kumbe roma kwa kuwa kupotea basi kakamatwa na polisi. You are stupid as they come.
 
Huu uzi lazima Kuna mtu Ana ujira kwa kila post anayoijibu sio bure mtu ukose kazi busy kuandika reply gazeti....njaa hii
 
Lazima tuilaumu serikali coz wenye akili zetu, tuna connect dots then tunapata picha kamili.

1.Bashite kwenda wcb studio kufanya nao kikao na kuwaahidi mambo kibao.

2. Dai kumuimba bashite, huku akijipendekeza. Yani katoa wimbo mpya Wa bashite. Na wimbo umeachiwa siku hizi hizi za kutekwa na kina Roma

3. Babutale kuitisha kikao cha wasanii kujua hatima ya kina Roma,akisema kitafanyika Tongwe records kumbe alikuwa na mpango Wa kukifanyia Nyumbani kwa bashite.

4. Bashite kutetemeka kidole akiongea na wasanii, na kuhakikisha EXACTLY siku watakayopatikana kina Roma na kweli imekuwa hivyo.

Etc
 
Mimi naamini kuwa hakuna PANYA atakayemyumbisha Rais Magufuli na serikali yake.
Lakini ikibidi mimi nilidhani kuna haja ya kutumia mbinu alizotumia SADDAM HUSSEIN kumshikisha adabu yeyote aliyeonekana kuhatarisha usalama wa Nchi.
MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI, TUPO PAMOJA.
 
Lazima tuilaumu serikali coz wenye akili zetu, tuna connect dots then tunapata picha kamili.

1.Bashite kwenda wcb studio kufanya nao kikao na kuwaahidi mambo kibao.

2. Dai kumuimba bashite, huku akijipendekeza. Yani katoa wimbo mpya Wa bashite.

3. Babutale kuitisha kikao cha wasanii kujua hatima ya kina Roma,akisema kitafanyika Tongwe records kumbe alikuwa na mpango Wa kukifanyia Nyumbani kwa bashite.

4. Bashite kutetemeka kidole akiongea na wasanii, na kuhakikisha EXACTLY siku watakayopatikana kina Roma na kweli imekuwa hivyo.

Etc
Mungu ndiyo kafunua yote siku zote Mungu huwaonyesha wanadamu kwa njia mbalimbali, akina Babu Tale na Daimond wamepiga pesa za Maliyamungu Bashite lakini wakakosea kutengeneza movie kwa sababu director ana vyeti feki uelewa juu ya sinema upo chini, tunashukuru mungu kusimama kidete na kuonyesha njia zote za ubaya zilipo.
 
Back
Top Bottom