Mbinu chafu za maadui wa Rais Magufuli

Mbinu chafu za maadui wa Rais Magufuli

Ili suala lipo kisiasa tu, Roma si tishio lolote kwa serikali hadi atekwe, kama kuondolewa wangedondoshwa kina Lowasa 2015 waliokuwa wana uwezo wa kuidondosha serikali nzima, tena Lowasa alikuwa mgonjwa wangeweza kumuondoa vizuri tu kwa kupandikiza "ugonjwa" mwingine.

Serikali ihakikishe inaingia chini kabisa kujua nani anahusika na huu upuuzi, kuna wahuni wamechukua fursa ya hali ya kisiasa, hawa si wakuwachekea, Roma hajawahi kuwa tishio na wala si tishio kwa serikali, waliomteka nia yao ni kutengeneza chuki na si kingine.
2015 ulisikia kituo au radio imevamiwa na mitutu?
2015 ulisikia waziri katishiwa kwa bastola,
2015 ulisikia msanii kakamatwa kwa kutoa wimbo?
2015 ulisikia mwanasiasa amekamatwa mara 7 kwa mwaka mmoja mtu huyo huyo?
2015 ulisikia kiongozi anaomba malaika washuke wafunge mitandao?
 
Zamani tulipokuwae kulikuwa na somo la URAI na syllabus ya somo hili ilihakikisha wanafunzi wanafundishwa majukumu ya serikali kwa raia wake. Jukumu moja la serikali kwa raia wake ni kuwalinda wao na mali zao!! Iwapo raia wanatekwa kutoka majumbani mwao na muda mrefu unapita bila ndugu na jamaa kujua waliko[ Ben Saanane na sasa Roma] ni nani wa kulaumiwa?

Sio siri tena kuwa hapa nchini kwetu kwa sasa usalama hakuna tena kwani uhalifu mitaami umetamalaki; watu wanatekwa na kuibiwa majumbani mwao mchana kweupe na wakienda kutoa taarifa vituo vya polisi hawapati msaada wowote na mara nyingine hawa hawa polisi wanashirikiana na hawa wahalifu!!! Jeshi la polisi halisaidii kabisa kulinda usalama wa raia na mali zao na wakati mwingine wanakuwa kero zaidi kwa walioathirika na wizi wa mali zao kwani huomba rushwa ili wafanye upelelezi wa uhalifu. Raia lazima tumlalamike Ngosha kwa sababu kuwepo kwa nani awe IGP kunatokana na utashi wake; THE BUCK STOPS WITH HIM!!!

Ndio maanaa..kila nikija humu nakutana na utumbo.

Wewe ulisoma Uraia, well, somo la URAIA ulilosoma lilikua mbadala ya somo la SIASA tulio soma sisi.

Wengi wenu mngejikita kwenye kilimo cha VIAZI na njegere.
 
Mkuu Son of Gamba kuna points muhimu sana umezigusia, hongera kwa hilo kwan wachache tutaokuelewa mantiki yako kwa Uzi huu. Ila mimi binafsi kuna mambo kadhaa ya maana nimejifunza . Big up sana.
 
Nimekuwa nikisoma "comments" nyingi sana humu JF zinazohusu kutekwa kwa Roma Mkatoliki na nyingi kati ya hizo comments zinamlaumu Rais Magufuli na Serikali yake. Hata alipopotea Ben Saanane, watu walikuwa wanaishutumu Serikali ya Rais Magufuli.

Mimi ningependa kuhoji; hivi ninyi mnaoishutumu Serikali mna uhakika gani kuwa Serikali ndiyo inahusika na mambo haya?
Binafsi naamini na ninatambua wazi kuwa hakuna uthibitisho wowote ule unaoonyesha kuwa Serikali ndiyo inahusika.

Serikali yoyote ile duniani huwa na maadui. Hakuna Serikali isiyokuwa na maadui hapa duniani. Hata Serikali yetu inayoongozwa na Rais Magufuli pia ina maadui. Maadui hawa hawapendi kuona Rais wetu Magufuli anaendesha nchi hii kwa amani na mafanikio. Maadui hawa watafanya kila wawezalo ili kumchafua Rais na Serikali yake mbele ya macho ya Watanzania na mbele ya jamii ya kimataifa pia.

Inavyoonekana sasa hivi, maadui hawa wanatumia nafasi iliyojitokeza sasa hivi hapa nchini au mwanya uliojitokeza kufanya uhalifu kwa kisingizio kuwa Serikali ndiyo inahusika. Kuna watu wako tayari hata kutoa roho za wenzao ili mradi tu malengo yao yafanikiwe.

Mimi nina mashaka sana tena sana na baadhi ya vyama vya upinzani hapa Tanzania. Vyama hivi vikiongozwa na chama fulani hivi, vinaendesha siasa chafu sana hapa nchini ili tu kuhakikisha taswira safi ya Serikali ya Rais Magufuli inachafuliwa kwa gharama yoyote ile.

Kuna baadhi ya waliokuwa viongozi wakubwa tu hapa nchini waliokuwa kwenye madaraka nyeti, sasa hivi wako kwenye upande wa upinzani na viongozi hawa siyo "MALAIKA". Ni watu wenye uchu wa madaraka, ni watu wenye mbinu chafu sana za kutafuta madaraka, ni watu wa kufanya siasa za "matukio" na "maigizo". Watu hawa ni hatari sana kuliko tunavyofikiria, ni hatari sana tena sana.

Nafahamu kuna baadhi yenu mtatukana sana hapa, lakini amini nawaambieni, ukweli utafahamika na mtabaki midomo wazi.

Kila serikali hapa duniani ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha uwepo wa serikali husika. Hata Serikali yetu pia ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha usalama wa nchi hii, lakini siyo Roma wala siyo Ben saanane. By the way who is Roma Mkatoliki to the government? Roma is no body.

Kama ni kuwashughulikia watu, basi mimi nafikiri Lissu angekuwa wa kwanza, tena siku nyingi sana na siyo Ben Saanane au Roma. Kama ni kuwafunga midomo watu, basi Lema angeshapotezwa siku nyingi sana na siyo Roma. Msijidanganye, kati ya hao niliowataja hakuna mwenye uwezo wa kujificha ama kujilinda iwapo Serikali itaamua kwa dhati kumshughulikia na kumpoteza mazima! Hakuna mwenye uwezo wa kujilinda hata awe nani.

Watanzania kuweni makini sana na mambo yanayofanyika sasa hivi hapa nchini. Msikimbilie kumtukana na kumlaumu Rais Magufuli kumbe chawa anayewatafuna mmembeba wenyewe kwenye nguo zenu.

Serikali inalitambua hili na inajua ni nani anayehusika na mchezo huu mchafu na It's just a matter of time, kila kitu kitajulikana. Serikali ina mkono mrefu sana na mbinu hii inayotumiwa na "MAADUI" imeshajulikana na sasa hivi kuna kazi maalumu "inaendelea". Kazi maalumu ambayo wewe au mimi hatutatangaziwa au kujulishwa ni namna gani inafanyika.

Rais Magufuli, wewe piga kazi na wala usiyumbishwe na mbinu chafu za hawa wahuni wachache wanaotaka kukumaliza. Tuko pamoja na wewe Rais wetu mpendwa.

By Son of Gamba.
Tuseme pana hypothesis mbili hapa tuzitafakari kwa kina:
1. Kwamba serekali inateka watu, tena wapinzani kwa kutafuta kiki kwa umma.
Yawezekana matatizo ya wananchi ni makubwa mno kiasi kwamba serekali imeanza kushindwa, na sasa wameanza kutafuta kiki za kupotezea mwelekeo wa watanzania, kutokana na shida nyingi za kiuchumi na maendeleo na hali ngumu kwa ujumla ya watanzania. Kwahio, inajaribu kua potezea wananchi mtazamo, ili wasiwe wanaongelea jambo moja la bashite, na maisha magumu.
2. Kwamba wapinzani wamezidiwa na kasi ya rais nakuanza kuteka watu ili nao kutafuta kiki.
Kwa upande wa wapinzani, yawezekana nao wameanza kuteka watu kwa kutafuta kiki na airtime. Yawezekana hoja zao mpaka hapa tulipofikia, rais amewapiku na wapotea kabisa kwa kasi ya mwendo wa maendeleo. Kwahio kuapoteza munkari wananchi wanaanza kuingia kwenye ujangili wakuteka watu ili wananchi wasione mazuri ya awamu hii kwasababu hawana ajenda.

Kwahio kwa ufupi, hypothesis hizi mbili, lazima zifanyiwe tafiti kwa kina ili kubaini chazo cha haya yote. Tumechoka kuokota ndugu zenu kwenye masafeti. Hii nchi ni ya democracy. Mbona watu waliandamana Africa ya kusini bila tatizo. Mbona huku maandamano, na mikutano yaki siasa ni shida. Kenya wanafanya sababu ndio kazi ya vyama.
Ombi, sio serekali wala vyama vingine, tusitafute kiki kwa kuteka atu. Leteni maendeleo, na kuweni na ajenda za kitaifa.
 
Nimekuwa nikisoma "comments" nyingi sana humu JF zinazohusu kutekwa kwa Roma Mkatoliki na nyingi kati ya hizo comments zinamlaumu Rais Magufuli na Serikali yake. Hata alipopotea Ben Saanane, watu walikuwa wanaishutumu Serikali ya Rais Magufuli.

Mimi ningependa kuhoji; hivi ninyi mnaoishutumu Serikali mna uhakika gani kuwa Serikali ndiyo inahusika na mambo haya?
Binafsi naamini na ninatambua wazi kuwa hakuna uthibitisho wowote ule unaoonyesha kuwa Serikali ndiyo inahusika.

Serikali yoyote ile duniani huwa na maadui. Hakuna Serikali isiyokuwa na maadui hapa duniani. Hata Serikali yetu inayoongozwa na Rais Magufuli pia ina maadui. Maadui hawa hawapendi kuona Rais wetu Magufuli anaendesha nchi hii kwa amani na mafanikio. Maadui hawa watafanya kila wawezalo ili kumchafua Rais na Serikali yake mbele ya macho ya Watanzania na mbele ya jamii ya kimataifa pia.

Inavyoonekana sasa hivi, maadui hawa wanatumia nafasi iliyojitokeza sasa hivi hapa nchini au mwanya uliojitokeza kufanya uhalifu kwa kisingizio kuwa Serikali ndiyo inahusika. Kuna watu wako tayari hata kutoa roho za wenzao ili mradi tu malengo yao yafanikiwe.

Mimi nina mashaka sana tena sana na baadhi ya vyama vya upinzani hapa Tanzania. Vyama hivi vikiongozwa na chama fulani hivi, vinaendesha siasa chafu sana hapa nchini ili tu kuhakikisha taswira safi ya Serikali ya Rais Magufuli inachafuliwa kwa gharama yoyote ile.

Kuna baadhi ya waliokuwa viongozi wakubwa tu hapa nchini waliokuwa kwenye madaraka nyeti, sasa hivi wako kwenye upande wa upinzani na viongozi hawa siyo "MALAIKA". Ni watu wenye uchu wa madaraka, ni watu wenye mbinu chafu sana za kutafuta madaraka, ni watu wa kufanya siasa za "matukio" na "maigizo". Watu hawa ni hatari sana kuliko tunavyofikiria, ni hatari sana tena sana.

Nafahamu kuna baadhi yenu mtatukana sana hapa, lakini amini nawaambieni, ukweli utafahamika na mtabaki midomo wazi.

Kila serikali hapa duniani ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha uwepo wa serikali husika. Hata Serikali yetu pia ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha usalama wa nchi hii, lakini siyo Roma wala siyo Ben saanane. By the way who is Roma Mkatoliki to the government? Roma is no body.

Kama ni kuwashughulikia watu, basi mimi nafikiri Lissu angekuwa wa kwanza, tena siku nyingi sana na siyo Ben Saanane au Roma. Kama ni kuwafunga midomo watu, basi Lema angeshapotezwa siku nyingi sana na siyo Roma. Msijidanganye, kati ya hao niliowataja hakuna mwenye uwezo wa kujificha ama kujilinda iwapo Serikali itaamua kwa dhati kumshughulikia na kumpoteza mazima! Hakuna mwenye uwezo wa kujilinda hata awe nani.

Watanzania kuweni makini sana na mambo yanayofanyika sasa hivi hapa nchini. Msikimbilie kumtukana na kumlaumu Rais Magufuli kumbe chawa anayewatafuna mmembeba wenyewe kwenye nguo zenu.

Serikali inalitambua hili na inajua ni nani anayehusika na mchezo huu mchafu na It's just a matter of time, kila kitu kitajulikana. Serikali ina mkono mrefu sana na mbinu hii inayotumiwa na "MAADUI" imeshajulikana na sasa hivi kuna kazi maalumu "inaendelea". Kazi maalumu ambayo wewe au mimi hatutatangaziwa au kujulishwa ni namna gani inafanyika.

Rais Magufuli, wewe piga kazi na wala usiyumbishwe na mbinu chafu za hawa wahuni wachache wanaotaka kukumaliza. Tuko pamoja na wewe Rais wetu mpendwa.

By Son of Gamba.
ujinga nipale inapozani lisu na Lema ni hatali kwa selikali kukiko roma(wasanii)..wimbo mmoja unaoikashifu serilkali una impact kubwa mmno kuliko mikutano 200 ya lema na lisu....by theway kukosoa serikali ni jambo la kawaida isichukuliwe kama ni uadui ...kama hakuna jira uchumi ni mbaya nk tunapasa kusema na tusikilizwe
 
Wewe ulisoma Uraia, well, somo la URAIA ulilosoma lilikua mbadala ya somo la SIASA tulio soma sisi

Tofauti yenu na sisi inaonekana wazi pale mnapoangalia kila kitu kisiasa siasa tu na ndio maana mnakwama!! Mnaweka mbele vyama vya siasa badala ya TAIFA lenu na short comings ndio hizo kuchagua vilaza vilaza kwa misingi ya kisiasa kuliwakilisha Taifa lenye wasomi waliotukuka huko EALA !!! Ndio maana wenzenu wanawacheka huko EALA kuwa kitu mnachokifamu ni porojo nyingi substance ZERO!!!

Sasa hudhani kuwa nyie ndio mnatakiwa muwe mnalima njegele na viazi?
 
Vyombo vya ulinzi na usalama viko chini ya nani mkuu? Jukumu la ulinzi na usalama wa raia ni dhamana ya nani? Umesema kuna maadui wa serikali, kwanini msiwakamate kama mna uhakika uli raia wasiendelee kutekwa? Hatuwalipi mishahara? Hatujawanunulia silaha? Au mnapungukiwa nini hata mzidiwe na maadui mnaokiri kuwa wapo? Jaribu kuweka itikadi pembeni, fikiria ni mtoto wako katekwa au wewe mwenyewe. Kuwa na utu ndugu
Asante sana mkuu! Umemweleza vizuri sana. Hawa ni watu hawajui serikali ni nini? Na wajibu wa serikali na kwanini wanalipa kodi, kwanini wanaenda kwenye box la kura kila baada ya 5years. Hawa watu hawajui hata wajibu wa rais, hawajui kuwa Rais ni Amiri Jeshi Mkuu...!! Hawa watu hawajui kuwa Mkuu wa Mkoa ni nani na wajibu wake! Kwa kifupi yaan hawajui chochote! Yaan wapo tu ili waijaze dunia!
 
Zamani tulipokuwa shule kulikuwa na somo la URAI na syllabus ya somo hili ilihakikisha wanafunzi wanafundishwa majukumu ya serikali kwa raia wake. Jukumu moja la serikali kwa raia wake ni kuwalinda wao na mali zao!! Iwapo raia wanatekwa kutoka majumbani mwao na muda mrefu unapita bila ndugu na jamaa kujua waliko[ Ben Saanane na sasa Roma] ni nani wa kulaumiwa?

Sio siri tena kuwa hapa nchini kwetu kwa sasa usalama hakuna tena kwani uhalifu mitaami umetamalaki; watu wanatekwa na kuibiwa majumbani mwao mchana kweupe na wakienda kutoa taarifa vituo vya polisi hawapati msaada wowote na mara nyingine hawa hawa polisi wanashirikiana na hawa wahalifu!!! Jeshi la polisi halisaidii kabisa kulinda usalama wa raia na mali zao na wakati mwingine wanakuwa kero zaidi kwa walioathirika na wizi wa mali zao kwani huomba rushwa ili wafanye upelelezi wa uhalifu. Raia lazima tumlalamike Ngosha kwa sababu kuwepo kwa nani awe IGP kunatokana na utashi wake; THE BUCK STOPS WITH HIM!!!
Nchi kubwa zenye technologia ya hali ya juu ya ulinzi na usalama kama Marekani watu wanatekwa na wengine huwa hawapatikani kabisa, itakuwa Tanzania nchi ya dunia ya tatu?

Tatizo lenu wengi wenu mnaishi kwa mihemuko ya kisiasa na uhalisia wa mambo hamjui. Fungukeni akili zenu mtajua nini kinaendelea.
 
Kwahiyo unataka kutuambia kuwa serikali imeshindwa kulinda RAIA wake?
 
Mimi ningependa kuhoji; hivi ninyi mnaoishutumu Serikali mna uhakika gani kuwa Serikali ndiyo inahusika na mambo haya?
Na mimi naomba nikuhoji; je ni nani anayelilinda jambazi lililovamia kituo cha Clouds FM? Kama si ushahidi wa picha ya video kuliumbua hilo jambazi nadhani leo ungekuwa unaongea mengine lakini pamoja na kuanikwa hadharani serikali imelishughulikia vipi hilo jambazi jizi la jina?
Kuna watu wako tayari hata kutoa roho za wenzao ili mradi tu malengo yao yafanikiwe.
Usiwe masikini wa akili; serikali unayoisifia kuwa ina uwezo mkubwa iko wapi mpaka watu unaodai wako tayari kutoa roho za watu watambe bila woga? Serikali gani inaweza kufanya ujinga wa kuweka mwakilishi wa wananchi ndani kwa tuhuma za kijinga kama tunavyoishuhudia hii ya Magufuli?
Mimi nina mashaka sana tena sana na baadhi ya vyama vya upinzani hapa Tanzania. Vyama hivi vikiongozwa na chama fulani hivi, vinaendesha siasa chafu sana hapa nchini ili tu kuhakikisha taswira safi ya Serikali ya Rais Magufuli inachafuliwa kwa gharama yoyote ile.
Taswira chafu ya serikali inaletwa na kiongozi mkuu wa nchi na serikali anayeamua kutofuata sheria kufikia kuvunja katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea. Toka lini uchafu ukachafuliwa?
Ni watu wenye uchu wa madaraka, ni watu wenye mbinu chafu sana za kutafuta madaraka, ni watu wa kufanya siasa za "matukio" na "maigizo". Watu hawa ni hatari sana kuliko tunavyofikiria, ni hatari sana tena sana.
Wenye uchu wa madaraka wako madarakani kwa zaidi ya nusu karne toka tupate uhuru na bado wanang'ang'ania hayo madaraka hata kama uwezo hawana. hivi ni watu gani wameapa kutochia madaraka hata kwa miaka mia ijayo? Je ni wapinzani?
Nafahamu kuna baadhi yenu mtatukana sana hapa, lakini amini nawaambieni, ukweli utafahamika na mtabaki midomo wazi.
Maneno uliyoyaandika ndiyo yanakuumbua ulivyojaa ujinga...wewe unadhani serikali ya Adolf Hiler haikuwa na watetezi kama wewe? Walikuwepo hata waliokuwa wakijitoa mhanga kulinda utawala wa kidikteta hata kuwa kutoa roho zao sembuse huu wa hovyo wa kidikteta uchwara. Hivyo ndivyo binadamu walivyo hasa pale wanapokuwa wanafiki na wabinafsi kama wewe.
Kila serikali hapa duniani ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha uwepo wa serikali husika. Hata Serikali yetu pia ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha usalama wa nchi hii, lakini siyo Roma wala siyo Ben saanane. By the way who is Roma Mkatoliki to the government? Roma is no body.
Sasa hapa ndipo unapojianika na kuonesha ulivyo mtupu kichwani, je unajua kwamba binadamu wote wana haki sawa mbele ya sheria? Ziko serikali zimewahi kufukuru kwa kuwafananisha baadhi ya wananchi wake na panya; kwamba wako wananchi wasio chochote na wapo ambao ni uchafu tu hata wakipotezwa sawa tu. Asante Son of Gamba, hapa umewazindua wengi kuhusu serikali ya Magufuli inavyowachukulia baadhi ya wananchi wake.
Kama ni kuwashughulikia watu, basi mimi nafikiri Lissu angekuwa wa kwanza, tena siku nyingi sana na siyo Ben Saanane au Roma.
Na mimi nasema kama ni kushughulikia wahalifu serikali ingewashughulikia wezi na majambazi kama Bashite na sio wananchi wasio na hatia kama Ben Saanane au Roma. Kushindwa kuwashughulikia wanaowatolea wananchi bunduki mchana kweupe kunaonesha tunayo genge tu la kihuni na si serikali.
Msikimbilie kumtukana na kumlaumu Rais Magufuli kumbe chawa anayewatafuna mmembeba wenyewe kwenye nguo zenu.
Nafikiri hata kumbukumbu huna wewe limbukeni...ni huyo huyo Magufuli anayewatukana Watanzania kila leo tena anawatukana hadharani. Amewahi kuwaita watoto wa wananchi vilaza kumbe vilaza anawafuga hadi nyumbani kwake. Anamlinda hadi kilaza wa kutupwa kwa kumpachika mavyeo asivyostahili ili azidi kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wananchi.
Rais Magufuli, wewe piga kazi na wala usiyumbishwe na mbinu chafu za hawa wahuni wachache wanaotaka kukumaliza. Tuko pamoja na wewe Rais wetu mpendwa.
Masikini Son of Gamba...pole sana!
 
Kama Nape aliyelala porini siku kadhaa alitaka kupigwa risasi mbele ya waandishi wa habari na mkulu badala ya kukemea tukio hilo yeye kachukizwa na magazeti yaliyotoa picha za huyo mtu. Halafu unakuja kuandika utumbo mreeeefu. Tatizo nini lakini, hii miaka 60-70 ya hapa duniani ndio inayowadanganya?
Wamelewa madaraka, huwezi kushabikia yanayoendelea nchini kwa sasa labda uwe mnufafaika.

Watu wanadhani wataishi milele wakiwa madarakani
 
umeeleza vizur tatizo umeegemea upande mmoja sana.

kama roma is no body sawa.

swalii ney wa mitego je?

Walivyotumia nguvu kubwa kwa ney wamitego mpaka rais kuingilia kati. lazima wanainchi tuwe na mashaka na serekali.

angalia logic usiendeshwe na hisia kama mtoto wa kike.
Point mkuu Kuna watu wanakulupuka sana
 
Tuna uhakika kwasababu uvamizi wa studio kama huu ulifanyika Clouds Media na walinzi wa rais wakaonekana kwenye CCTV camera wakiwa na silaha za vita na rais wa nchi akasisitiza "Bashite chapa kaaazi"
 
Nimekuwa nikisoma "comments" nyingi sana humu JF zinazohusu kutekwa kwa Roma Mkatoliki na nyingi kati ya hizo comments zinamlaumu Rais Magufuli na Serikali yake. Hata alipopotea Ben Saanane, watu walikuwa wanaishutumu Serikali ya Rais Magufuli.

Mimi ningependa kuhoji; hivi ninyi mnaoishutumu Serikali mna uhakika gani kuwa Serikali ndiyo inahusika na mambo haya?
Binafsi naamini na ninatambua wazi kuwa hakuna uthibitisho wowote ule unaoonyesha kuwa Serikali ndiyo inahusika.

Serikali yoyote ile duniani huwa na maadui. Hakuna Serikali isiyokuwa na maadui hapa duniani. Hata Serikali yetu inayoongozwa na Rais Magufuli pia ina maadui. Maadui hawa hawapendi kuona Rais wetu Magufuli anaendesha nchi hii kwa amani na mafanikio. Maadui hawa watafanya kila wawezalo ili kumchafua Rais na Serikali yake mbele ya macho ya Watanzania na mbele ya jamii ya kimataifa pia.

Inavyoonekana sasa hivi, maadui hawa wanatumia nafasi iliyojitokeza sasa hivi hapa nchini au mwanya uliojitokeza kufanya uhalifu kwa kisingizio kuwa Serikali ndiyo inahusika. Kuna watu wako tayari hata kutoa roho za wenzao ili mradi tu malengo yao yafanikiwe.

Mimi nina mashaka sana tena sana na baadhi ya vyama vya upinzani hapa Tanzania. Vyama hivi vikiongozwa na chama fulani hivi, vinaendesha siasa chafu sana hapa nchini ili tu kuhakikisha taswira safi ya Serikali ya Rais Magufuli inachafuliwa kwa gharama yoyote ile.

Kuna baadhi ya waliokuwa viongozi wakubwa tu hapa nchini waliokuwa kwenye madaraka nyeti, sasa hivi wako kwenye upande wa upinzani na viongozi hawa siyo "MALAIKA". Ni watu wenye uchu wa madaraka, ni watu wenye mbinu chafu sana za kutafuta madaraka, ni watu wa kufanya siasa za "matukio" na "maigizo". Watu hawa ni hatari sana kuliko tunavyofikiria, ni hatari sana tena sana.

Nafahamu kuna baadhi yenu mtatukana sana hapa, lakini amini nawaambieni, ukweli utafahamika na mtabaki midomo wazi.

Kila serikali hapa duniani ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha uwepo wa serikali husika. Hata Serikali yetu pia ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha usalama wa nchi hii, lakini siyo Roma wala siyo Ben saanane. By the way who is Roma Mkatoliki to the government? Roma is no body.

Kama ni kuwashughulikia watu, basi mimi nafikiri Lissu angekuwa wa kwanza, tena siku nyingi sana na siyo Ben Saanane au Roma. Kama ni kuwafunga midomo watu, basi Lema angeshapotezwa siku nyingi sana na siyo Roma. Msijidanganye, kati ya hao niliowataja hakuna mwenye uwezo wa kujificha ama kujilinda iwapo Serikali itaamua kwa dhati kumshughulikia na kumpoteza mazima! Hakuna mwenye uwezo wa kujilinda hata awe nani.

Watanzania kuweni makini sana na mambo yanayofanyika sasa hivi hapa nchini. Msikimbilie kumtukana na kumlaumu Rais Magufuli kumbe chawa anayewatafuna mmembeba wenyewe kwenye nguo zenu.

Serikali inalitambua hili na inajua ni nani anayehusika na mchezo huu mchafu na It's just a matter of time, kila kitu kitajulikana. Serikali ina mkono mrefu sana na mbinu hii inayotumiwa na "MAADUI" imeshajulikana na sasa hivi kuna kazi maalumu "inaendelea". Kazi maalumu ambayo wewe au mimi hatutatangaziwa au kujulishwa ni namna gani inafanyika.

Rais Magufuli, wewe piga kazi na wala usiyumbishwe na mbinu chafu za hawa wahuni wachache wanaotaka kukumaliza. Tuko pamoja na wewe Rais wetu mpendwa.

By Son of Gamba.

Kazo ya serikali ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao,mpaka sasa serikali imefeli.
Alipotea Ben mpaka leo serikali haijasema lolote,Clouds ikavamiwa mpaka sasa serikali imekaa kimya,Nape alitishiwa bastola mchana na wandishi na wananchi wakiwepo mpaka sasa yule kijana ajachukuliwa hatua,Nay wa Mitego alishikwa kama jambazi na kama asingepost kuwa kakamatwa basi tusingemuona tena. Juzi Roma na wenzake wametekwa na mpaka sasa serikali inajikanyaga tu.
Serikali ya Magufuli imefeli kutunza usalama wa raia na mali zao.
 
Huu mda wakuandka hyo hewa si ungelima hata mchicha kwenye kopo.?
 
Wewe kichwa maji ina maana hukuona kilichofanywa na mkuu wa mkoa clouds na alichofanyiwa nape?

Tatizo la watanzania wengi ni kama wewe, huwa hampendi ukweli hata ukianikwa wazi lazima mtabisha tu kwa kuwa akili zenu zimeganda.
 
Back
Top Bottom