Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,952
Nimekuwa nikisoma "comments" nyingi sana humu JF zinazohusu kutekwa kwa Roma Mkatoliki na nyingi kati ya hizo comments zinamlaumu Rais Magufuli na Serikali yake. Hata alipopotea Ben Saanane, watu walikuwa wanaishutumu Serikali ya Rais Magufuli.
Mimi ningependa kuhoji; hivi ninyi mnaoishutumu Serikali mna uhakika gani kuwa Serikali ndiyo inahusika na mambo haya?
Binafsi naamini na ninatambua wazi kuwa hakuna uthibitisho wowote ule unaoonyesha kuwa Serikali ndiyo inahusika.
Serikali yoyote ile duniani huwa na maadui. Hakuna Serikali isiyokuwa na maadui hapa duniani. Hata Serikali yetu inayoongozwa na Rais Magufuli pia ina maadui. Maadui hawa hawapendi kuona Rais wetu Magufuli anaendesha nchi hii kwa amani na mafanikio. Maadui hawa watafanya kila wawezalo ili kumchafua Rais na Serikali yake mbele ya macho ya Watanzania na mbele ya jamii ya kimataifa pia.
Inavyoonekana sasa hivi, maadui hawa wanatumia nafasi iliyojitokeza sasa hivi hapa nchini au mwanya uliojitokeza kufanya uhalifu kwa kisingizio kuwa Serikali ndiyo inahusika. Kuna watu wako tayari hata kutoa roho za wenzao ili mradi tu malengo yao yafanikiwe.
Mimi nina mashaka sana tena sana na baadhi ya vyama vya upinzani hapa Tanzania. Vyama hivi vikiongozwa na chama fulani hivi, vinaendesha siasa chafu sana hapa nchini ili tu kuhakikisha taswira safi ya Serikali ya Rais Magufuli inachafuliwa kwa gharama yoyote ile.
Kuna baadhi ya waliokuwa viongozi wakubwa tu hapa nchini waliokuwa kwenye madaraka nyeti, sasa hivi wako kwenye upande wa upinzani na viongozi hawa siyo "MALAIKA". Ni watu wenye uchu wa madaraka, ni watu wenye mbinu chafu sana za kutafuta madaraka, ni watu wa kufanya siasa za "matukio" na "maigizo". Watu hawa ni hatari sana kuliko tunavyofikiria, ni hatari sana tena sana.
Nafahamu kuna baadhi yenu mtatukana sana hapa, lakini amini nawaambieni, ukweli utafahamika na mtabaki midomo wazi.
Kila serikali hapa duniani ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha uwepo wa serikali husika. Hata Serikali yetu pia ina namna ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha usalama wa nchi hii, lakini siyo Roma wala siyo Ben saanane. By the way who is Roma Mkatoliki to the government? Roma is no body.
Kama ni kuwashughulikia watu, basi mimi nafikiri Lissu angekuwa wa kwanza, tena siku nyingi sana na siyo Ben Saanane au Roma. Kama ni kuwafunga midomo watu, basi Lema angeshapotezwa siku nyingi sana na siyo Roma. Msijidanganye, kati ya hao niliowataja hakuna mwenye uwezo wa kujificha ama kujilinda iwapo Serikali itaamua kwa dhati kumshughulikia na kumpoteza mazima! Hakuna mwenye uwezo wa kujilinda hata awe nani.
Watanzania kuweni makini sana na mambo yanayofanyika sasa hivi hapa nchini. Msikimbilie kumtukana na kumlaumu Rais Magufuli kumbe chawa anayewatafuna mmembeba wenyewe kwenye nguo zenu.
Serikali inalitambua hili na inajua ni nani anayehusika na mchezo huu mchafu na It's just a matter of time, kila kitu kitajulikana. Serikali ina mkono mrefu sana na mbinu hii inayotumiwa na "MAADUI" imeshajulikana na sasa hivi kuna kazi maalumu "inaendelea". Kazi maalumu ambayo wewe au mimi hatutatangaziwa au kujulishwa ni namna gani inafanyika.
Rais Magufuli, wewe piga kazi na wala usiyumbishwe na mbinu chafu za hawa wahuni wachache wanaotaka kukumaliza. Tuko pamoja na wewe Rais wetu mpendwa.
By Son of Gamba.