Je, Uamuzi wa Russia kuivamia Ukraine ni mbinu au mkakati ulioshindwa (Strategic Failures)? hili ni swali linahitaji majibu.
Sababu mojawapo iliyotolewa na Russia kwa kuhalalisha uvamizi wake nchini Ukraine ilikuwa ni Ukraine kuwa na mpango wa kujiunga EU na baadae NATO.
Russia/Putin alitaka Ukraine iendelee kuwa Neutral country huku ikiendelea kuwa koloni la Russia kama ilivyo kwa jilani yake Belarus ya Lukashenko.
Putin/Russia alikuwa hataki Ukraine ijiunge EU na NATO kwa hoja ya kwamba alikuwa hataki EU na NATO wajitanue na kuisogelea mipaka ya Russia eti kwa hofu ya kuhatarisha usalama wa Russia.
Lakini baada ya kuivamia Ukraine tumeshuhudia nchi kama Sweden na Finland kujitoa kwenye uamuzi wa kuwa Neutral state na kuchukua hatua zaidi za kujiunga na NATO ili kujihakikisha ulinzi wa nchi zao dhidi ya Russia.
Matokea ya maamuzi ya Finland ukazaa matunda na kuruhusiwa kwa kasi ya mwendokasi kujiunga NATO. Sweden naye muda si mrefu ataruhusiwa kuwa mwanachama wa NATO.
Baada ya Finland kujiunga NATO sasa NATO iko ubavuni mwa Russia kwa eneo kubwa kuliko hata kabla hajaivamia Ukraine. NATO imejitanua maradufu na Russia hana cha kuifanya Finland na Sweden pamoja na vitisho vyake vya awali. Mbaya zaidi Ukraine naye mwisho wa siku atajiunga NATO baada ya vita kuisha. Hii itaifanya NATO kujitanua maradufu kwa muda mfupi na Russia asiwe na la kufanya.
Ukraine akiruhusiwa kujiunga na NATO baada ya vita huenda nchi zingine kama Moldova, Georgia, Azerbaijan, Armenia na zingine nazo zikaruhusiwa kujiunga na NATO.
Hivyo basi uamuzi wa Russia kuivamia Ukraine ni mkakati ulioshindwa (strategic Failure), ambapo Russia amepata hasara kuliko faida. Kama sababu ilikuwa ni kuogopa kusogelewa na NATO kwa kisingizio kuwa usalama wa Russia utakuwa hatarini sasa kasogelewa na hana la kufanya.
Hebu tutafakari hoja hizi;
1. Kwa kuwa Finland ni mwanachama wa NATO. Je, Russia atadhubutu kurusha hata bomu la mkono nchini Finland kwa sasa?
2. Russia ana ubavu wa kuizuia Sweden isijiunge na NATO kama ambavyo tuliaminishwa mwanzo na Russia?
3. Je, kitendo cha Russia kuivamia Ukraine ndo kajipalia mkaa zaidi na kujiweka kwenye hatari kuliko alivyofikiria kabla?
4. Je, Russia ataweza kuizuia NATO kutojitanua zaidi kama anavyojigamba au ni kelele za chura kwa ng'ombe kumzuia asinywe maji?
5. Kama Russia atashindwa hii vita na Ukraine kujiunga na NATO atakuwa amepata faida kwa kuanzisha vita dhidi ya Ukraine au hasara.
6. Kama Sweden na Finland wameomba kujiunga na NATO na kukubaliwa katikati ya vita. Je, Russia kapata faida gani?
7. Je, nchi zingine zikiomba kujiunga na NATO atakuwa na ubavu wa kuzizuia kama alivyojaribu kufanya kwa Ukraine na kushindwa?