Mbezi Beach wamekosaje lami? Mbona Mbweni, Manzese na Yombo kuna lami?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,905
Kuna kitu kinanishangaza Sana...ukienda Manzese Hadi vichochoroni kuna lami...ukienda Yombo kuna lami mitaani tu huko Buza Hadi vibarazani kuna lami...

Ukifika Mbezi Beach ukishatoka Bagamoyo road Tu ni vumbi juu ya vumbi...majumba makali ...eneo planned lakini barabara vumbi....wakati ukienda Mbweni JKT angalau kuna lami za mtaani kiasi lakini Mbezi beach vumbi vumbi.....yaani Manzese Hadi mto umepigwa zege.....

Kuna mtu anajua why???
 
Sasa watu wenye kipato cha chini wanahitaji lami au kuongezewa kipato??

Hapa chini ni moja ya vigezo vya miradi ya DMDP ambapo ukitazama maeneo tajwa, utaona ni zile sehemu ambazo zilisahaulika...

iii) Kupandisha hadhi makazi yaliyopangwa kiholela katika Kata 14 za Tandale, Mburahati, Mwananyamala, Gongo la Mboto, Kiwalani, Ukonga, Keko, Kilakala, Mbagalakuu, Mbagala, Mtoni, Yombo Vituka, Kijichi na Makangarawe kwa kujenga kilometa 145 kwa kiwango cha lami, kuweka nyenzo za ukusanyaji wa taka ngumu, kujenga mitaro ya kutiririsha maji ya mvua, kuweka taa za barabarani, kujenga njia za watembea kwa miguu, ujenzi wa maeneo ya mapumziko na vituo vya mabasi, ujenzi wa vyoo vya umma na ujenzi wa maeneo ya michezo.
 
Kuna kitu kinanishangaza Sana...ukienda Manzese Hadi vichochoroni kuna lami..ukienda Yombo kuna lami mitaani Tu .huko Buza Hadi vibarazani kuna lami...Ukifika mbezi beach ukishatoka Bagamoyo road Tu ni vumbi juu ya vumbi...majumba makali ...eneo planned lakini barabara vumbi....wakati ukienda Mbweni JKT angalau kuna lami za mtaani kiasi lakini mbezi beach vumbi vumbi.....yaani Manzese Hadi mto umepigwa zege.....
Kuna mtu anajua why???
mahali wanakokaa wahaya ni shida watata sanaaa
 
Dah ilinipita hii ..
Sasa mbona Masaki kuna lami
Mbweni kuna lami?..
Why mbezi beach ndo kama imerukwa
 
Dah ilinipita hii ..
Sasa mbona Masaki kuna lami
Mbweni kuna lami?..
Why mbezi beach ndo kama imerukwa

Masaki ina lami miaka mingi mkuu kutokana na hadhi yake...

Mbweni nayo lami haipo kila mahali bali barabara muhimu tu kama ilivyo kwa Mbezi Beach...

Pia kwa Dar kuna maeneo lami zinapelekwa kutokana na uwepo wa kiongozi au viongozi fulani...reference zipo nyingi tu
 
Kuna kitu kinanishangaza Sana...ukienda Manzese Hadi vichochoroni kuna lami..ukienda Yombo kuna lami mitaani Tu .huko Buza Hadi vibarazani kuna lami...Ukifika mbezi beach ukishatoka Bagamoyo road Tu ni vumbi juu ya vumbi...majumba makali ...eneo planned lakini barabara vumbi....wakati ukienda Mbweni JKT angalau kuna lami za mtaani kiasi lakini mbezi beach vumbi vumbi.....yaani Manzese Hadi mto umepigwa zege.....
Kuna mtu anajua why???
Siyo hivyo tu The Boss. Mbezi beach, Kunduchi beach, Kawe, Bahari beach na ununio hadi tegeta ni majanga sana hasa wakati wa mvua. Barabara za mitaa zote hopeless.
 
Back
Top Bottom