Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Manzese Dar: Hashim Rungwe(CHAUMA) Azindua Ilani, Kutoa Chakula bure Shuleni na Hospitalini. Kujenga mfereji wa Maji ya Bahari dar-Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
835
1,000
Salaam Wakuu,

Leo chama cha cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) , kinazindua Kampeni zake Manzese Dar Es Salaam.

Leo Asubuhi Mgombea Urais wa CHAUMA aliwalalamikia TAKUKURU kwa kumzua kupika Ubwabwa na kuku kwa kile kinachodaiwa ni Rushwa. Akahoji kwanini Wanaotumia Wasanii hawaambiwi wanatoa Rushwa?

Akahoji ni kosa gani mtu akiamua hela ya kuwapa wasanii akawapikia watu wale Ubwabwa na kuku? Kasema watakutana Mahakamani

Nipo hapa kuwaletea kile kinachojiri.

=====

UPDATES: 1544HRS

=====

1618hrs : Mgombea Mwenza wa Urais Masoud Rashid anasema;
IMG_20200905_162341_430.jpg

Tutashirikiana na Mabeberu kupeleka Maji ya Bahari kwenda dodoma. Tutajenga Mfereji kama mfereji wa Suez kwa miaka 10. Awamu ya kwanza tutajenga Kilometa 100 ndani ya mwaka mmoja na nusu. Mfereji huo utatumiwa na Watalii na Meli. Hata Mchina ni bebeeu, tutashirikiana naye.

=> Tutajenga Daraja kutoka Zanzibar hadi Dar Es Salaam ndani ya Miaka Mitano. Ni KM 65 kutoka Zanzibar hadi Dar. Tunaweza Jenga madaraja hata mia

=> Kupeleka vyakula Mahospitalini sasa basi. Watoto kushinda njaa Mashuleni sasa basi. Kura mpeni Hashim Rungwe. Ubwabwa Mashuleni, Mashuleni Ubwabwa. Asanteni sana.

1640hrs: Hashim Rungwe

=> Watoto wetu Mashuleni wana njaa.

Kwanza nawanadi Madiwani Wangu. Chagueni CHAUMA.
IMG_20200905_164223_443.jpg

Picha ya Madiwani wa CHAUMA Mkoa wa Dar Es Salaam

Mimi nimelazwa Hospitali, nikaondoka. Hakuna chakula kule kule hospitali. Hawa Wamekuta tunapewa Chakula, Mashuleni Madaftari na Kalamu bure.

Mnadanganywa eti Elimu bure. Mna uhakika? Elimu bure lakini Michango mingi.

Mimi nikiingia Madarakani Mashuleni na Hospitalini chakula kitakuwa bure, niingizeni Ikulu.

Nikiingia Madarakani, Nauza Magari yale yote ya Mil 300 hadi 400. Wakuu wa Wilaya na Mikoa watatembelea Land Rover Defender.

1647hrs: Hotuba ya Rais Hashim Rungwe imesimama baada ya Jenereta kuishiwa Mafuta

1645hrs: Hotuba inaendelea

Wangapi hapa mumepanda ndege ya Bombadia?

Miaka 53 tumekaa tunawasikiliza CCM wanatuendesha Hovyo.

Watoto wakienda shule wakapata ubwabwa na kuku anasoma na kuelewa.

Hela zitatoka wapi? Si kuna mfuko wa shule? Wananchi watalima Mashamba chakula watauza Mashuleni.

Madawa bila chakula wagonjwa wanakufa. Tulikuwa tunatoa chakula bure Hospitali hawa CCM Wakaondoa.

Shuleni Watoto wapate Wali, Ubwabwa na nyama.

Mimi nakwenda kwenye Semina za Serikali. Nikifika tu tunapata chai. Sambusa zipo, mayai yapo Soseji. Tunakula pale halafu tunaingia kusikiliza Semina. Ikifika saa sita tunaambiwa tukale. Lakini mtoto wako asubuhi hadi jioni hali chochote. Huko kwenye semina tukimaliza kunywa chai ya jioni tunapewa Mshiko. Hawa watoto wetu tunashindwa kuwalisha? Tunaweza, watoto wote watapata chakula. Na hivi vitu vililuwepo.

Wanahoji eti wakati ule tunatoa chakula shuleni tulikuwa Mil 8 sasa hivi tupo Mil 60. Hii sio hoja, kwani hao watu Mil 60 hawalipi kodi?

Mnajenga Madaraja, barabara mnanunua ndege. Mtu atakula hivyo vitu? Sisi Mkishawapa kula wanakimbia hawarudi hadi Uchaguzi.

Nchi zilizoendelea, hawa Wakina dada wakizaa watoto wanapewa Pesa

Tumekatazwa Ubwabwa, TAKUKURU wamepiga mikwara. Tukienda mikutano ya CCM tunakula, Tukienda kwenye Semina Tunakula. Mbona hawakamatwi? Nmeandaa Chakula, baada ya hapa tunakula.

Tunataka Utawala wa Sheria. Watu wanafungwa miezi sita mwaka halafu unamuomba hela ndo mnamuachia. Mimi wameshanikamata mara tatu bila kosa na hakuna lolote waliloniambia. Nikawatishia napeleka kesi mahakama kuu ndo nikaachiwa.

Watu wanabomolewa nyumba zao halafu hawapewi fidia kisa unajenga barabara, kwanini? CHAUMA tutawalipa wote fidia. Hakikisheni Unamchagua Hashim Rungwe. Mimi ni Wakili, nitaleta Utawala wa Sheria


Watu wananunua ndege, ukiwauliza wamenunua bei gani hawasemi. Tenda hawaoneshi.

Sasa amewaita Wabunge wajitambulishe.

Watu waliopata hitilafu ya akili, wanazunguka barabarani Serikali haiwasaidii. Nani anawapa chakula? Sisi tutatoa chakula. Hospitali

Rufaa zaidi ya 500. Wanasema eti chama hiki hawakijui. Wasimamizi wa Uchaguzi ni Makada wa CCM. Tulienda Mahakamani tukashinda wakakata rufaa. Eti Wanakula kiapo.

Mimi Chama changu Wabunge 15 Wameenguliwa. Wananchi tusaidieni kupiga kelele.. Wenzetu wanachanja mbuga sisi tunaambia Tusubiri rufaa tume itatenda haki.

Tutahakikisha Vijana wanapata ajira ya kilimo. Tutaanzisha Mashamba ya Vijana. Tutashirikiana na Mabeberu kutoka China na Ulaya kuhakikisha Vijana wanapata ajira. Bandari zetu zimejengwa na Mabeberu.

Tanzania tumerudi nyuma kwa Ushirikiano na Mataifa mengine. Tunawapa majina ya ajabu eti MABEBERU. Hayo ni majina kabla ya uhuru.

Sisi tukiandamana tunaambiwa tutapigwa kipigo cha Mbwa koko. Chagueni mtu anayeongea mambo ya maana.

Tutaka nchi huru. Ukimuona Askari unanywea, sisi tunataka ukimuona askari uchangamke.

Nchi yetu haina furaha. Takwimu zinaonesha. Nichagueni mimi.

Wale wanaotaka kunichakachua kama safari ile, safari hii sikubali.

Tumechoka siasa za kutututisha. Watu wanatoa maburungutu ya hela zingine anarusha mbona hawasemi ni rushwa. Lakini mimi chakula changu eti ni Rushwa. Mi natoa chakula kwasababu nawapenda. Kula wali sio Starehe, ni kitu cha kawaida. Wali ni mchele tu. Pesa mfukoni na Mkate unaleta.

Ilani ya chama cha Ukombozi wa umma imesheheni imejaa.

Sisi tukichimba mfereji wa maji kwenda dodoma, wangapi watapata Huduma?

Bandari ya bagamoyo imezimwa. Eti kuna wezi, si muwakamate?

Majumba yake ya kigamboni tumepata hasara.

Majumba ya Morocco na Kawe beach, huyu jamaa kazima. Nyumba hazijengwi tena eti kuna wezi. Kama wezi wakamatwe. Mnatutia hasara sisi wananchi na kodi zetu. Huyu jamaa vipi?

Tunataka mali za wananchi ziwasaidie wenyewe. Ameenda kujenga huko, ndicho tulimtuma?

Kwenye Uongozi wangu hakuna kulipiza kisasi. Sisi wote watu wa kufa. Mimi ni kifa nalala, mtabaki mnalia yule mzee alikuwa mzuri. Eti unaua wewe ndo hufi? Umauti unao. Sio hivyo hivyo tumafanya vibaya.

Kazi kama ngumu si unaaacha? Sasa kila saa kulalamika eti urais mgumu.

Kampeni zao wasanii 300. Wasanii mnawakumbuka leo? Wasanii wanakimbilia kule sababu ya njaa. Hamna Ubwabwa


Mahitaji yangu. Mficha njaa kifo kitamuumbua. Tumepigwa sana tupo hoi.

Sisi tunataka kutembea Tanzania nzima na maneno yetu ndo hayo.

Hospitali na Mashuleni watakula bure. Wanaozurura barabarani wenye Upungufu wa akili watapewa chakula.


Tumepangiwa ratiba tuzunguke nchi nzima. Hali yetu ni mbaya hatuna fedha. Tupeni fedha kwenye account yetu ya benki tuzunguke nchi Nzima. Hii ni kazi ya wananchi

Account namba 10259127100. Hii ya shilingi na akaunti ya dola ni crdb kojitonyama 0250259127100

Ukiwa na njaa huwezi kusoma ukaelewa.

Chama cha CCM hakikujiandikisha kisheria kama vyama vingine. Hakijapita kuomba wadhamini

TAKUKURU wamenikataza kugawa Wali kuku. Nikisema niende na watu nyumbani Polisi watanifuata. Kesho Nitaendelea na Kampeni Temeke

IMG_20200905_162532_580.jpg
IMG_20200905_162341_430.jpg
IMG_20200905_163806_085.jpg
IMG_20200905_163803_510.jpg
IMG_20200905_163808_690.jpg
IMG_20200905_164223_443.jpg
IMG_20200905_173734_726.jpg
IMG_20200905_173732_504.jpg
IMG_20200905_173729_983.jpg
IMG_20200905_173702_628.jpg
IMG_20200905_173659_091.jpg
IMG_20200905_172911_196.jpg
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
26,696
2,000
Tafadhali Sana Kiongozi Ambaye Unatoa Habari Moja Kwa Moja Hapo Manzese
Hitaji Letu Kubwa Tunaloomba Wakianza Kugawa Ubwabwa Weka Update Haraka Tuje, Hatuwezi Kuacha Chakula Leo!!😋😋😋😋😍😘🤩
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,039
2,000
Kwahio anapika au hapiki ?

Ila definition ya Rushwa siielewi..., je wali wanaowaambia wengine wasigombee urais atawapatia kazi nyingine ni nini kama sio rushwa...

Haya maigizo ya nchi hii zaidi ya Bongo Movie
 

mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,721
2,000
Salaam Wakuu,

Leo chama cha CHAUMA, kinazindua Kampeni zake Manzese Dar Es Salaam.

Leo Asubuhi Mgombea Urais wa CHAUMA aliwalalamikia TAKUKURU kwa kumzua kupika Ubwabwa na kuku kwa kile kinachodaiwa ni Rushwa. Akahoji kwanini Wanaotumia Wasanii hawaambiwi wanatoa Rushwa?

Akahoji ni kosa gani mtu akiamua hela ya kuwapa wasanii akawapikia watu wale Ubwabwa na kuku? Kasema watakutana Mahakamani

Nipo hapa kuwaletea kile kinachojiri.

=====

UPDATES: 1544HRS

=====
Sawa nakuja
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
20,247
2,000
Kwa mara ya kwanza maishani nilijua kwanini nimezaliwa. For the first time I had a purpose.

That purpose was to attend this campaign na kufinyanga ubwabwa kwa kuku kwa kadri ninavyoweza.

Takukuru took that away from me.

Sikubali nakuja hivyo hivyo. I was born for this.
 

kelphin kepph

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
2,380
2,000
Kwa mara ya kwanza maishani nilijua kwanini nimezaliwa. For the first time I had a purpose.

That purpose was to attend this campaign na kufinyanga ubwabwa kwa kuku kwa kadri ninavyoweza.

Takukuru took that away from me.

Sikubali nakuja hivyo hivyo. I was born for this.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom