Tafadhali wewe unayeripoti uko wapi na kama mambo ndio hayo basi wajue peoples power iko kazini. umesikia au umeambiwa
tafadhali tuambie sisi tunasubiri.
habari wana JF Kwa sasa nipo uyole hapa nashindwa kwenda mjini kifupi hali toka asubuhi ni mbaya kuliko hata mnavofikiri hadi sasa ni mwendo wa mabomu hakuna kupumzika na raia nao wapo hi hadi sasa kuna mauaji yameshafanyika .
[h=3]Breaking Nuuz Liveee!! Kutoka Mbeya muda huu : Bara bara za Mbeya zafungwa hakuna pa kupita Jeshi laingilia kati lamwaga wanajeshi Risasi zalindima sasa[/h]
Picha hazipo Clear sana kutokana na Mabomu kuwa Mengi wananchi wanaziba barabara kuzuia Magari yasipite Maeneo ya Ilomba wananchi Bado wanafunga Barabara Wananchi wamechoma matairi kuzuia usafiri wa aina yoyote usiwepo Hapa ni Mamajoni ambapo Bara bara zimefungwa.mia
Haya huwa yanaanza kido dogo hivi hivi!! Mwisho wake ulikuwa mbaya sana kwa Mubarak!! Yule kijana alivyochoka tu kunyanyaswa na polisi akajilipua moto, mambo yakawa mambo!! Hizi risasi mwishowe si mzuri!!
Poleni wana wa Mbeya, Mungu mkubwa kama hakuna maafa yaliyotokea, jamani damu ya binadamu si sawa na damu ya mnyama mwingine, wenye mamlaka waangalie hivi si viashiria vizuri kwa mstakabali wa nchi, watu wana shida na hawaoni mwanga wa matumaini.
arusha tulikuwa tuna msubiri dr dr dr dr dr dr kikwete kachomoa dakika za mwisho..sijui ataogoa arusha mpaka lini..safi sana wana-mbeya tuko pamoja kwenye kutafuta ukombozi zidi ya mafisadi
hii ni hali ya wananchi waliokata tamaa baada ya kuonewa kudanganywa kuzulumiwa hawaoni shida kupoteza lolote kwani katika hali halisi wameshapotezewa kila kitu. si walaumu kwa wanachofanya laiti wangekuwa wana misingi mizuri ya maisha ajira biashara na kutoonewa kamwe hawawezi kufanya vurugu za namna hii.
Polisi hao hao na mgambo ndio wa kwanza kuwaibia hao wamachinga wenye mitaji midogo wasio na hatia na kujifanya wanakiuka sheria ndio maana wanachukua bidhaa zao uongo mtupo na uonevu huku matajiri wakubwa wakitafutiwa maoneo mazuri na wakati mwingine hata kuwafukuza wazawa na kuwapa matajiri wawekeze kwa hakli hii watu hawachoki na wataacha kufanya vurugu?
nyie mnaotaka source subirini taarifa ya habari..kwa tanzania haijawai tokea mabomu kuanza kupigwa asubui mpaka mda huu huo mziki sio wa mchezo ndugu zangu kama una ndugu au rafiki muulize akupe habari hali ni mbaya huko
Huyo Kandoro alifikiri hili jambo litakuwa jepesi kabisa, JWTZ imekuwa vita sasa! Kuna kipindi polisi wanapiga mabomu ya machozi mpaka wanaishiwa inabidi wakaombe JW sijui kama hili hlaitatukia Mbeya.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.