Mbeya na Kilimanjaro: Siri ya mafanikio yao ni nini?

Hawa watu wana akili sana....sijui walitumia akili gani hadi wakazaliwa kwenye kanda hizo.....
 
Sasa hakuna kabila lilobaki nyuma kwa maendeleo na kusoma. Ngoja nawaulize wachaga ambao mnajisifia sana kwenye huu uzi kwa nini sasa mnabaguana na kudharauliana, Mkibosho anamuona Mkishimundu mjinga, Mrombo anamuona Mmachame mshenzi.

ukiona ndugu wawili wanagombana chukua jembe ukalime .... hizo ni vita za hisia zinazochochea maendeleo yao
 
Mkuu Joka Kuu,
Labda nikumbushe kuwa mkoa wa Tanga ndio wa kwanza kuwa na gazeti wakati wa Wajerumani 1905.
Mkonge ulikuwepo miaka mingi sana kabla ya uhuru na ndilo chimbuko la miundo mbinu kama bandari na reli.

Katika shule za zamani sana mojawapo ni Tanga Tech school iliyokuwepo kabla ya Uhuru.
Athari zitokanazo na wageni kama Waarabu zilikuwepo, ikiwa ni pamoja na wamishenari waliofika mapema.
Tanga imekuwa manisapaa tangu mwaka 1966. Umetoa takwimu nzuri tu kuwa wasomi walikuwepo tangu zama hizo.
Kwahiyo factor zote zimekamilika! Je, kwanini Tanga imefika hapo ilipo?

Tuangalie mikoa ya Kanda ya Ziwa. Ukiacha Kagera uliokuwa na cash crop kama Kilimanjaro, Mwanza na Shinyanga zilikuwa na Pamba pamoja na madini (Williamson Diamond 1948). Hata kama wazawa hawakuchimba lakini ukweli unabaki kuwa hicho ni kitu muhimu sana katika maendeleo.

Katika miaka ya 70 na 80 Pamba ilikuwa hot cake na moja kati ya Cash crop kubwa sana nchini.
Tofauti na matarajio athari za Kahawa Kagera zinaonekana katika maendeleo hadi leo, kwanini basi Mwanza na Shinyanga zisiwe kama Kagera achilia mbali Mbeya au Kilimanajaro?

Uwepo wa Bandari ya Mtwara ulitokana na kilimo cha Korosho na mengine ya cash crop. Hata kama Korosho ilianguka kama kahawa ilivyoanguka katika soko la dunia, kwanini hatuoni effect yake hata kama si kwa kiwango cha Mbeya na Kilimanjaro?

Zakumi, kama kipimo kimojawapo cha maendeleo ni net immigration, huwezi kuishia hapo ni lazima uende mbele zaidi.
Kilimanjaro, mathalani, watu hawahamii kwasababu ya uhaba wa ardhi. Kesi nyingi za Kilimanjaro ni kuhusu migogoro ya ardhi. Lakini pia lazima ufahamu kuwa ili mtu aweze kuhamia Kilimanjaro ni lazima awe contender na si pretender. Hilo linawazuia wengi kuhamia kule. Matokeo yake ni kinyume, Wakazi wengi wa Kilimanjaro, Mbeya na Kagera wanazidi kuteka maeneo mengine kwasababu wanahimili competition.

Nicholas, nadhani unawahukumu Wapare bila kuwa na inside out zao. Sidhani kuwa wewe kufanya kazi na Mpare mmoja kitakwimu inakidhi haja ya kujenga hoja achilia mbali ukweli wa takwimu hizo. Unasahau kuwa katika mkoa wa Kilimanjaro ni wilaya mbili tu ndizo zenye wenyeji wakaazi wapare yaani Same na Mwanga. Na kuna ukweli kuwa watu wanashindwa kutofautisha hata kwa majina. Njau ni Mpare na Mchagga, Mberesero ni Mchaga na ni Mpare, Minja anaweza kuwa Mchaga au Mpare. Kwahiyo ukijenga hoja kuna 'thin line' unayotakiwa kuiangalia.

Ningeomba unsome vizuri Bagusule ana hoja za msingi sana si kutaka kushinda majadiliano ni kuweka sawa kumbu kumbu.
Mfano, nimeona mifereji ya umwagiliaji iliyotumika vizazi 4 vilivyopita. Endapo kizazi kimoja kina life expectancy ya miaka 40 tu, hapo tunazungumzia umwagiliaji kuanza kutumika miaka 160 iliyopita.

Ni wapare waliowahi kusimama toe to toe na Mkoloni kupinga kodi kwa kuelewa kuwa haikuwa sahihi na wala haikuwasaidia kwa matarajio yao( MBIRU). Unapodai ni waoga na hivyo CCM itawatawala unakosea sana.
Ninachojua ni kuwa utiifu wao upo kwa viongozi wao na si chama! wamejenga shule na zahanati baada ya kuweka tofauti za kisiasa pembeni. Wakati watu wanazungumzia shule za kata wao walimaliza siku nyingi sana na Msuya.
Walivunja miamba, wakachangishana majogoo kwa kutumia mbunge wao.

Ubahili wao unawasaidia sana na ingekuwa ni majuu tungesema 'financial discipline yao ni excellent na ni fiscal conservatives. Kwa vile ni Wapare wanaitwa Mabahili.Ubahili wa kupeleka mtoto shule nadhani ni mzuri kuliko kuwa Frugal (Arusha wanasema Fogo) kusikosaidia.
Sipendi kujadili watu napenda tujadili issue, hivyo hilo sitaendelea nalo.

Tujiulize, Je, wale ndugu zangu za Malinyi, kidogo basi, Zignali na viwanja sitini wanaotumia mpunga wa msimu katika hafla za kila siku ikiwa ni pamoja na pombe wamlaumu nani?

Ninachosema hapa ni kuwa maendeleo yana vichocheo lakini kubwa zaidi ni hulka na tabia zilizojengwa na tamaduni.

Nguruvi

Hiyo theory yangu ya net migration is well proven. Chaggas, Hayas, Kyusas depend on the same primitive methods of survival like the rest of the country.
 
Naomba kuuliza Mbeya na Kilimanjaro kuna viwanda vingapi vya uzalishaji, naona kila mtu anaongelea maeneo alipotoka na kujipa sifa nyingi. Kuna makabila yalikuwa yanabanwa na mazingira tu lakini ni watu wa kazi sana. Nenda Mwanza saizi utakuta wafanyabiashara wakubwa ni watu kutoka mkoa wa Mara na wenyeji Mwanza, saizi wamefika mpaka Dar, kuna Wapemba hawa mmewasahau wamejaa mikoani wapo Dar, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, saizi wamefika mpaka Malawi, Angola, Zimbabwe, Zambia, wanafanya biashara zao.
 
Naomba kuuliza Mbeya na Kilimanjaro kuna viwanda vingapi, naona kila mtu anaongelea maeneo alipotoka na kujipa sifa nyingi. Kuna makabila yalikuwa yanabanwa na mazingira tu lakini ni watu wa kazi sana. Nenda Mwanza saizi utakuta wafanyabiashara wakubwa ni watu kutoka mkoa wa Mara na wenyeji Mwanza, saizi wamefika mapaka Dar, kuna Wapemba hawa mmewasahau wamejaa mikoani wapo Dar, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, saizi wamefika mpaka Malawi, Angola, Zimbabwe, Zambia, wanafanya biashara zao.
Nadhani tunaongelea maeneo si makabila. Hilo la makabila si jema. Hoja ni kuwa katika umasikini wetu kuna sehemu zina nafuu kuliko zingine.
Nimezunguka Tanzania, nakuhakikishia kuna sehemu unaweza kufika na kujiuliza kama ni Tanzania hii au nyingine.

Hoja si kuwa kwanini Wapemba wamefanikiwa kibiashara n.k Hoja ni kuwa kwanini Pemba ni masikini sana kuliko ABCD.
That's a point
 
Nguruvi:

Eneo lolote lenye mafanikio litakuwa na inward migration. Niambie mmchinga gani anakwenda kupiga debe Mbeya au Kagera au Mmasai gani anakwenda kuwa mlinzi Kagera?
 
Nguruvi:

Eneo lolote lenye mafanikio litakuwa na inward migration. Niambie mmchinga gani anakwenda kupiga debe Mbeya au Kagera au Mmasai gani anakwenda kuwa mlinzi Kagera?
Nimeleta hoja kuwa, eneo kama Kilimnjaro lina tatizo la ardhi kwa kiasi kikubwa sana. Je, unataraji nani aende huko?

Pili, nikasema ili uweze ku-survive Kilimanjaro unatakiwa uwe ''contender na si pretender'' Sasa unatarajia Machinga afanye biashara gani wakati huko umachinga ulishafanywa miaka 40 iliyopita. Liangalie hili jambo kwa upana!
Huko Mbeya na Kilimanjaro wanahitaji wawekezaji ! ushanfahamu?
 
Nadhani tunaongelea maeneo si makabila. Hilo la makabila si jema. Hoja ni kuwa katika umasikini wetu kuna sehemu zina nafuu kuliko zingine.
Nimezunguka Tanzania, nakuhakikishia kuna sehemu unaweza kufika na kujiuliza kama ni Tanzania hii au nyingine.

Hoja si kuwa kwanini Wapemba wamefanikiwa kibiashara n.k Hoja ni kuwa kwanini Pemba ni masikini sana kuliko ABCD.
That's a point

Mkuu mbona unakuwa double standard! Muanzisha huu uzi kaelezea watu kutoka Mbeya na Kilimanjaro wana mafanikio akiwalenga wachanga na wanyakyiusa, Nicholas, kaongelea makabila mengi sana na kujisifia wachaga na kuwaponda wapare lakini ukumwambia hivyo kuwa mnaongelea maeneo sio makabila, cha kushangaza wewe mwenyewe ukaanza kuongelea makabila na kujenga hoja ya kuwatetea wapare. Mie kutaja wapemba naona umekuwa mkali sana sijui kwa nini mkuu, mie sio mpemba lakini hawa jamaa nawakubali sana kwa kuangaika kutafuta maisha...Mkuu siasa za muungano weka pembeni tujadili hoja ukifuatilia huu uzi toka mwanzo umejaa ukabila tu.
 
Nimeleta hoja kuwa, eneo kama Kilimnjaro lina tatizo la ardhi kwa kiasi kikubwa sana. Je, unataraji nani aende huko?

Pili, nikasema ili uweze ku-survive Kilimanjaro unatakiwa uwe ''contender na si pretender'' Sasa unatarajia Machinga afanye biashara gani wakati huko umachinga ulishafanywa miaka 40 iliyopita. Liangalie hili jambo kwa upana!
Huko Mbeya na Kilimanjaro wanahitaji wawekezaji ! ushanfahamu?

Eneo siyo tatizo la kufanya watu wasiende kama kungekuwa na viwanda vya uzalishaji, lazima wangeitaji nguvu kazi, Dubai, Hong Kong zote zina maeneo madogo sana lakini watu wanakimbilia huko kwa nini.
 
Nadhani nimevutika na hoja ya joka kuu kuhusu uwepo wa cash crop kama kichocheo cha maendeleo katika maeneno fulani. Ima kama nilitoka nje na kutozungumzia makabila kwa kina basi niwie radhi na wengine.
Ninaamini kuwa huwezi kuwa Mnyakyusa kama hutoki Mbeya au Mbondei kama hutoke Nyumbani Muheza.

Pili, niliposema Wapemba nili chukua katika mstari wako na nilielezea vema bila chembe ya husuda. Ndio maana nimesema hoja si Wapemba waliofanikiwa katika biashara niki-acknowlege aggressiveness yao katika biashara. Lakini pia nafahamu kuwa Pemba ni sehemu Masikini na nikaunganisha hilo.
Sikuwa na maana ya kuleta politics za muungano! nadhani umenielewa tofauti, nimekuwia radhi hata hivyo!

Kuhusu Wapare nimenukuu Bangusule kwa majibu yake kwa Nicholas kwa kukubali hoja zake kama ninavyozijua kijiografia, kihistoria n.k.

Lakini pia hiyo hainizuii kuchangia kile ninachokijua kama nilivyofanya kwa Wapogoro na Warugu.
Nadhani kusimama katika ukweli ni jambo zuri hata kama unauma.

All in all niwie radhi kama kuna mahali nimekukwaza.
 
Eneo siyo tatizo la kufanya watu wasiende kama kungekuwa na viwanda vya uzalishaji, lazima wangeitaji nguvu kazi, Dubai, Hong Kong zote zina maeneo madogo sana lakini watu wanakimbilia huko kwa nini.
Tena hapa naona mnanisadia kujenga hoja. Watumishi wakipangwa Lindi, Mtwara Sumbawanga hawataki, wakiambiwa Kilimanjaro, Arusha,, Mbeya wanakwenda. Je hakuna attractiveness hapo.
Si mnakumbuka mikoa fulani iliwahi kufanywa kama mikoa ya adhabu! ni kwanini?

Kwa Machinga hawawezi kwasababu tayari kule kuna machinga ambao ni more advance ndio maana hawaendi. Kule kuna nguvu kazi tayari kwahiyo anayekwenda ajiandae.

Na vipi kuhusu ukweli kuwa ukienda kule unatakiwa uwe mshindani haswa! Hilo mbona hamlijibu. Hamuoni ni sababu ya kuzuia uhamiaji hasa kwa wasioweza kuhimili ushindani?
 
Nguruvi3, Galileo Galilei, Zakumi,

..mimi nadhani katika hoja hii tunaweza kuzungumzia maeneo pamoja na makabila bila kuonyesha dharau.

..pia sidhani kama tunazungumzia maendeleo per se, bali ile hali ya unafuu wa kiuchumi kwa jamii au eneo fulani.

..bado sielewi ni kitu gani kimetokea Tanga. haswa katika suala la elimu ambapo kama nilivyoeleza ndugu zetu wabondei walikuwa wako mbali kulinganisha na wenzao wa maeneo mengine.

..pia kuna ndugu zetu Wakinga na Wapemba ambao nadhani mwanzoni walikuwa hawavumi, lakini miaka ya hivi karibuni wameibuka ktk shughuli za biashara. factors gani mnadhani zimewezesha mafanikio ya jamii hizi?

..kuhusu dhana ya inward migration, sijui Zakumi anaielezea vipi hali ya wenyeji wa miji mbalimbali kuhamishwa ktk maeneo yao na wahamiaji wanaotokea maeneo mengine.
 
Last edited by a moderator:
Nimeleta hoja kuwa, eneo kama Kilimnjaro lina tatizo la ardhi kwa kiasi kikubwa sana. Je, unataraji nani aende huko?

Pili, nikasema ili uweze ku-survive Kilimanjaro unatakiwa uwe ''contender na si pretender'' Sasa unatarajia Machinga afanye biashara gani wakati huko umachinga ulishafanywa miaka 40 iliyopita. Liangalie hili jambo kwa upana!
Huko Mbeya na Kilimanjaro wanahitaji wawekezaji ! ushanfahamu?

Hakuna upana wowote. Eneo la watu linapoendelea, idadi ya watoto wanaozaliwa katika familia inapungua. Hivyo suala la tatizo la ardhi linakuwa halipo.

Pili kuna kuwa na diversification ya investments. Hizo investments zinafanya kutokee na ajira ambazo zitavutia watu kutoka sehemu zingine kwenda huko na vilevile kuzuia wazawa wa maeneo hayo kutoka nje ya maeneo yao.

Vitu hivi havijatokea katika mikoa au maeneo hayo husika. Hivyo kwa ujumla wao hawana maendeleo bali unafuu wa shida.
 
Nadhani nimevutika na hoja ya joka kuu kuhusu uwepo wa cash crop kama kichocheo cha maendeleo katika maeneno fulani. Ima kama nilitoka nje na kutozungumzia makabila kwa kina basi niwie radhi na wengine.
Ninaamini kuwa huwezi kuwa Mnyakyusa kama hutoki Mbeya au Mbondei kama hutoke Nyumbani Muheza.

Pili, niliposema Wapemba nili chukua katika mstari wako na nilielezea vema bila chembe ya husuda. Ndio maana nimesema hoja si Wapemba waliofanikiwa katika biashara niki-acknowlege aggressiveness yao katika biashara. Lakini pia nafahamu kuwa Pemba ni sehemu Masikini na nikaunganisha hilo.
Sikuwa na maana ya kuleta politics za muungano! nadhani umenielewa tofauti, nimekuwia radhi hata hivyo!

Kuhusu Wapare nimenukuu Bangusule kwa majibu yake kwa Nicholas kwa kukubali hoja zake kama ninavyozijua kijiografia, kihistoria n.k.

Lakini pia hiyo hainizuii kuchangia kile ninachokijua kama nilivyofanya kwa Wapogoro na Warugu.
Nadhani kusimama katika ukweli ni jambo zuri hata kama unauma.

All in all niwie radhi kama kuna mahali nimekukwaza.

Wala ujanikwanza mkuu ni majadiliano tu tupo pamoja. Tuendelee na mjadala.
 
Tatizo linajionyesha pale effect za waliopata opportunity kuwa bonyeza mizani ya mabadiliko wa wenzao na hata wao wenyewe kuweza grab opportunity kama si kujitengenezea opportunity.

Kuna wavivu kila mahlai ila kwa wachaga kujaa vibarazania asubuhi wakiwa wamevaa khanga mbili, na misuli hadi siku inaisha kila mtu atakushangaa.Akina mama wa kichaga arusha,moshi saa 11 wapo njiani na ndoo,vikapu etc wanawahi masokoni kununu bidhaa bora,saa moja wamshapanga ktk megenge au sokoni na tayari wanakwenda kufany abishara nyingine kama kununua na kuuaza mitumba,kutafuta nyasi za ngombe ambao pia wakiuzwa mtoto anakwenda shule au kwenda mashambani.

Cha kushangaza hawa akina mama wa apwani wanaoshinda vibarazani na nyumba zao zinathibitisha jinsi zilivyojengwa,wana miguu iliyopasuka pasuka vibaya ,huku wakiwa wachafua wa mwili na nyumba zao.

Mkuu Nico, mimi nimesoma Minaki nilikuwa na kawaida ya kutembelea vijiji vya pwani na kushiriki kwenye harusi zao, sikuwahi kukutana na wanawake wanao kaa barazani bila shughuli yoyote au kuona miguu yao imejaaa masagamba (would you believe IT) au wamejifunga sijuhi kanga moja!! Hivi umewahi kutembelea vijiji vya pwani kuingia nyumba wanazo ishi na kuangalia mazingira yanayo wazunguka? - ni watu wanao jali usafi wa mwili na mazingira hawakati miti ovyo!!

Sina hakika unazungumzia wanawake wa vijijini au mijini, wewe umekili kwamba kuna wavivu kila kabila - kama kuna mahali walikuwa wanalega lega kidogo watajifunza na kujirekebisha mbona wapo wengi wanao chakalika - cha muhimu hapa nikuwa-encourage na siyo kuwa-condem WHOLESALE hii haipendezi haka kidogo.
 
Nguruvi3, Galileo Galilei, Zakumi,

..mimi nadhani katika hoja hii tunaweza kuzungumzia maeneo pamoja na makabila bila kuonyesha dharau.

..pia sidhani kama tunazungumzia maendeleo per se, bali ile hali ya unafuu wa kiuchumi kwa jamii au eneo fulani.

..bado sielewi ni kitu gani kimetokea Tanga. haswa katika suala la elimu ambapo kama nilivyoeleza ndugu zetu wabondei walikuwa wako mbali kulinganisha na wenzao wa maeneo mengine.

..pia kuna ndugu zetu Wakinga na Wapemba ambao nadhani mwanzoni walikuwa hawavumi, lakini miaka ya hivi karibuni wameibuka ktk shughuli za biashara. factors gani mnadhani zimewezesha mafanikio ya jamii hizi?

..kuhusu dhana ya inward migration, sijui Zakumi anaielezea vipi hali ya wenyeji wa miji mbalimbali kuhamishwa ktk maeneo yao na wahamiaji wanaotokea maeneo mengine.

Jokakuu:

Sources zangu zinasema in 40s and 50s miji miwili tu Africa ilikuwa ina-over 1 Million population, one of the two is Cairo. Hivyo kusini mwa jangwa la sahara ni mmoja.

Migration hii ya kwenda kwenye miji mikubwa hiko katika bara zima la Africa na imeongeza property values. Watu wanaouza property zao hawahamishwi. They just take advantage of the market price. There's a boom and they are cashing in.
 
Back
Top Bottom