Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
Wazalendo, Happy New Year 2009!
Katika Kijarida cha Habari za Ukimwi (April - June 2008) Takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya Ukimwi kufuatia Kampeni ya Kitaifa ya Kupima Ukimwi kwa Hiari ni kama Ifuatavyo:
Maambukizi ya Juu:
- Mbeya - 15.2% (Kyela 24%, Chunya 23.7%)
- Iringa - 14.7% (Ludewa 19.7%, Makete 16.8%)
- Dar Es Salaam - 8.3%
- Mwanza - 8.1 %
- Coastal - 6.2%
- Ruvuma - 5.6%
Hakuna sababu zilizoainishwa ni nini vichocheo vikubwa vya maambukizi haya.
Wazalendo, Tunaambiwa Elimu Kuhusu Ukimwi imewafikia Watanzania kwa kiwango cha kutosha ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujikinga na maabukizi.
- Je, ni nini vichocheo vya maambukizi makumbwa yaliyoainishwa hapo juu na ni nini kifanyike?