kwa kuongezea...
...aliahidi kuwa wanafunzi wote wa shule za sekondari mjini mbeya watagaiwa laptop pindi atakapochaguliwa, kwa msisitizo alisisitiza kuwa habahatishi na ana historia ya kufanikisha miradi ya aina hiyo akitolea mfano alivyofanikisha mradi wa malaria-no-more.
...aliahidi kupambana na ufisadi wa ugawaji viwanja vya iwambi,na kuwa akiingia atahakikisha uhakiki unafanyika na waliofisadi wanachukuliwa hatua,mara baada ya kupata ubunge,yeye na madiwani wapya walizawadiwa na jiji viwanja,na hajaongelea tena jambo hilo.
Sugu ni failure kwa jiji la mbeya, japo chadema bado ina nguvu kubwa mbeya, lakini ccm inaweza ikashinda ubunge kwa sababu sugu ni "mbunge kivuli", jiji la mbeya limelidhibitishia taifa kuwa inawezekana jimbo kujiendesha bila ya "uwepo wa mbunge".
Naomba niweke angalizo hatumsemi kwa ubaya joseph mbilinyi lakini unapoongelea nafasi aliyonayo ni muhimu sana kwa maendeleo yetu,ameshindwa lazima tuwe wawazi na tusiposema vizazi vijavyo vitauliza mana sehemu zingine zitakuwa na maendeleo ubunge akiwa ni mtu wa hoja hata kama akiwa upinzani jimbo lake litapata maendeleo tu leo hii kigoma ni mkoa wenye waendeleo ila angalia sehemu kubwa ya wabunge wake ni wa upinzani tukipata mtu mzuri wenye hoja maendeleo yatakuja tu,tuache ushabiki usio na mana tupate mbunge mwenye kujua tumemtuma nini