Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Polisi mkoani humo inamshikilia mtu mmoja, Ally Mwakila (32), Mkazi wa Mwambene kwa tuhuma za kupatikana na laini za simu 141 zenye usajili wa majina ya Watu wengine
Mtuhumiwa ambaye pia ni fundi Umeme alikamatwa mnamo Julai 12, 2019 majira ya saa 7 mchana katika Mtaa wa Itongo, Kata ya Mwambete, Tarafa ya Iyunga na baada ya kuhojiwa alikiri kumiliki laini hizo
Alikutwa na laini za Halotel 13, laini za Tigo 29, laini moja ya TTCL, laini 78 za VodaCom na laini 20 za Airtel, pia alikutwa na vocha zilizotumika 5 za VodaCom, 4 za Tigo, 48 za Airtel na 3 za Halotel pamoja na simu Itel (3), Oking (1) na Hotwave (1)
Mtuhumiwa alikuwa na vitu hivyo ili kujipatia kipato kwa udanganyifu na atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika