Mbeya: Mbaroni kwa kukutwa na laini 141 za simu

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Polisi mkoani humo inamshikilia mtu mmoja, Ally Mwakila (32), Mkazi wa Mwambene kwa tuhuma za kupatikana na laini za simu 141 zenye usajili wa majina ya Watu wengine

Mtuhumiwa ambaye pia ni fundi Umeme alikamatwa mnamo Julai 12, 2019 majira ya saa 7 mchana katika Mtaa wa Itongo, Kata ya Mwambete, Tarafa ya Iyunga na baada ya kuhojiwa alikiri kumiliki laini hizo

Alikutwa na laini za Halotel 13, laini za Tigo 29, laini moja ya TTCL, laini 78 za VodaCom na laini 20 za Airtel, pia alikutwa na vocha zilizotumika 5 za VodaCom, 4 za Tigo, 48 za Airtel na 3 za Halotel pamoja na simu Itel (3), Oking (1) na Hotwave (1)

Mtuhumiwa alikuwa na vitu hivyo ili kujipatia kipato kwa udanganyifu na atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika
 
Wamchunguze isije ikawa 'ile pesa tuma kwenye namba hii'..
 
Kuna Yule wa south Africa alijiajiri kupitia mtandao alisifiwa Sana humu Na huyu naye sijui tumuweke wapi
 
Jingine saa 6 usiku linanitumia "mimi Mwenyenyumba wako nitumie kodi yangu kwa namba hii jina litakuja upupu gan sijui nikamjibu simple tu kafir... Ë !

Hata mm hii sms ya mm mwenye nyumba wako, ile kodi yangu itume kwenye hii namba,

Nikamjibu kuwa “Anakung’utwa na kufakamiwa na popobawa, kama kila mtu anaweza kuwa mpangaji wake”
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom