MBEYA: Kanisa kutoa orodha ya wauza unga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MBEYA: Kanisa kutoa orodha ya wauza unga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Jun 9, 2011.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  na Betty Kangonga

  MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Pentecost Church (TEC) la mjini Mbeya, William Mwamalanga, amesema wanatarajia kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kutaja hadharani orodha ya vigogo wanaoshiriki katika biashara ya dawa za kulevya.

  Kauli ya mchungaji huyo imekuja siku moja baada ya Ofisi ya Rais (Ikulu) kuwataka maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kuacha kutoa saa 48 kwa Rais Jakaya Kikwete kutaja majina ya viongozi wanaouza dawa za kulevya bali yeyote anayejishuku ajisamilishe au atajwe.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mwamalanga alisema kundi la viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali wamepanga kukutana kwa ajili ya kutaja majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo.

  Alisema wanatarajia kutaja majina yote, si ya viongozi wa dini ya Kikristo pekee, bali hata wale waliopo nje ya Ukristo, ambao taarifa zao zimefika hadi kwa Rais Kikwete.

  "Si kwamba tutataja majina ya maaskofu na wachungaji pekee, bali tutataja hadi wale waliomo ndani ya Ofisi ya Rais, ambao wanafanya biashara hiyo, wabunge pamoja na mawaziri," alidai mchungaji huyo.

  Alisema wana taarifa kamili ya viongozi wa dini ambao wanatumia makanisa kama vivuli na kujificha, kumbe wanaendesha biashara hiyo haramu inayoangamiza taifa.

  Mchungaji Mwamalanga alisema lengo ya kutaja majina hayo hadharani ni kutaka kumsaidia Rais Kikwete na kuisafisha nchi iondokane na uingizaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

  "Kwa sasa tupo Dodoma na leo tunatarajia kutaja majina hayo ambayo Rais Kikwete anashindwa kuyataja, ili kumsaidia …maana taarifa za orodha hiyo tuliwahi kumfikishia katika ofisi yake mwaka 2006," alisema.

  Alisema viongozi wa dini wanaotumia makanisa kama vivuli huku wakiendesha biashara hiyo wanafahamika wazi, lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua.

  Aliongeza kuwa wanategemea kuwa orodha hiyo ikiwekwa hadharani wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachunguza.

  Alibainisha kuwa kama vyombo vya dola vitapuuzia orodha hiyo watakayoitaja, kamwe mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayawezi kuzaa matunda.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Rais Kikwete akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Killian katika sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo, kuwa askofu wa Jimbo la Mbinga, alikaririwa akisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya.

  Kauli hiyo iliwafanya maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaojihusisha na dawa za kulevya.

  Baada ya tamko hilo, juzi Ofisi ya Rais Ikulu iliwakosoa viongozi hao kwa kutoa tamko la kusikitisha, ambalo ililiita kuwa halikustahili kutolewa nao.

  Ikulu iliweka bayana kuwa viongozi wa dini si malaika au watakatifu hapa duniani, kwani wanaweza kutumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa katika jamii.

  Source: Tanzania Daima.

  Angalizo langu: Ni mpambano kati ya Kanisa na Rais. Nafuu itakuwa kwa sie walalahoi kwani wauza unga wanaiharibu jamii na kama ni watu wenye nguvu basi nafikiri mahakama ya umma inawatosha kuwahukumu. Nawapa hongera sana maaskofu kwa ujasiri wenu watajeni jamii iwahukumu!!!!
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  mmmh tutasikia mengi..na nyie viongozi wa dini hebu fanyeni kazi ya mungu huko na mzidi kuwaombea kondoo wenu sio madawa madawa :shut-mouth:
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Afwadhali mchungaji aseme kabisa kabisa, wachungaji, maaskofu, waumini, mashehe, watumishiwa usalama, wafanyibiashara. Taja wote, lakini angalia wasije wakakusukulize kama nanihii.:shut-mouth:
   
 4. g

  gambatoto Senior Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Pentecost Church (TEC) la mjini Mbeya, William Mwamalanga, amesema wanatarajia kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kutaja hadharani orodha ya vigogo wanaoshiriki katika biashara ya dawa za kulevya.

  Kauli ya mchungaji huyo imekuja siku moja baada ya Ofisi ya Rais (Ikulu) kuwataka maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kuacha kutoa saa 48 kwa Rais Jakaya Kikwete kutaja majina ya viongozi wanaouza dawa za kulevya bali yeyote anayejishuku ajisamilishe au atajwe.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mwamalanga alisema kundi la viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali wamepanga kukutana kwa ajili ya kutaja majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo.

  Alisema wanatarajia kutaja majina yote, si ya viongozi wa dini ya Kikristo pekee, bali hata wale waliopo nje ya Ukristo, ambao taarifa zao zimefika hadi kwa Rais Kikwete.

  "Si kwamba tutataja majina ya maaskofu na wachungaji pekee, bali tutataja hadi wale waliomo ndani ya Ofisi ya Rais, ambao wanafanya biashara hiyo, wabunge pamoja na mawaziri," alidai mchungaji huyo.

  Alisema wana taarifa kamili ya viongozi wa dini ambao wanatumia makanisa kama vivuli na kujificha, kumbe wanaendesha biashara hiyo haramu inayoangamiza taifa.

  Mchungaji Mwamalanga alisema lengo ya kutaja majina hayo hadharani ni kutaka kumsaidia Rais Kikwete na kuisafisha nchi iondokane na uingizaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

  "Kwa sasa tupo Dodoma na leo tunatarajia kutaja majina hayo ambayo Rais Kikwete anashindwa kuyataja, ili kumsaidia …maana taarifa za orodha hiyo tuliwahi kumfikishia katika ofisi yake mwaka 2006," alisema.

  Alisema viongozi wa dini wanaotumia makanisa kama vivuli huku wakiendesha biashara hiyo wanafahamika wazi, lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua.

  Aliongeza kuwa wanategemea kuwa orodha hiyo ikiwekwa hadharani wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachunguza.

  Alibainisha kuwa kama vyombo vya dola vitapuuzia orodha hiyo watakayoitaja, kamwe mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayawezi kuzaa matunda.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Rais Kikwete akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Killian katika sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo, kuwa askofu wa Jimbo la Mbinga, alikaririwa akisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya.

  Kauli hiyo iliwafanya maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaojihusisha na dawa za kulevya.

  Baada ya tamko hilo, juzi Ofisi ya Rais Ikulu iliwakosoa viongozi hao kwa kutoa tamko la kusikitisha, ambalo ililiita kuwa halikustahili kutolewa nao.

  Ikulu iliweka bayana kuwa viongozi wa dini si malaika au watakatifu hapa duniani, kwani wanaweza kutumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa katika jamii.  Source: Tanzania Daima ya Leo

  Kanisa kutoa orodha ya wauza ‘unga'
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Huyu naye ametaka vyombo vya habari vitutangazie dhehebu lake tujue kwamba nalo lipo kati ya madhehebu yanayochukua kasi Tz.
  Swali langu dogo kwake mheshimiwa huyo ni je kama aliwafahamu alikuwa wapi siku zote kutaja? au ana ushirika na JK kiasi kwamba walikubaliana kwamba nikichokoza mjadala wewe wataje? Haya bwana ngoja tusubiri tuone kama atatwambia ni wakina nani kama si story kama za rafikiye Kikwete!
   
 6. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  du huu mwaka si mchezo mambo ni balaaa
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamaa hawa wanataka mtaja Riz One!
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  wataje kabisa ili moto uwake pande zote
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Wauza unga hawa hapa(sembe,ngano,muhogo,mchele nk)...:A S 103::A S 103:
  1. Bakhressa
  2. Azania
  3. Mteja
   
 10. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,424
  Likes Received: 3,786
  Trophy Points: 280
  Mi JK ananishangaza sana................
  Ile orodha ya waharibifu wa bandari anayo.......... lakini hajafanya kitu.......
  Orodha ya wahusika wa mishahara hewa ................. anayo hajafanya kitu.............
  Meremeta................ hata muwasulubishe hawafanyi kitu...................
  Huyo askofu kasema orodha ya wauza unga unayo toka 2006............ hujafanya kitu..........
  Mafisadi orodha unayo........................... umewashindwa..................

  JK....... KUISHIA KUFAHAMU ORODHA TU HAKUTAKUSAIDIA KITU KATIKA HIZI HARAKATI ZA KUVUANA MAGAMBA.....................KWENYE HILI LA MADAWA MMENIKUMBUSHA AMINA CHIFUPA
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Angalia asije kukuitia press conference na kukupa siku 7 umtake razi:biggrin1:
   
 12. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kikwete ni gamba tu,
   
 13. M

  Masuke JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Amesema walimpelekea orodha tangu 2006.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tunamakaribisha sana mwamalanga kututajia orodha hii hata rais alisema anahitaji msaada wa viongozi wa dini kumsaidia ni mwanzo mzuri.
   
 15. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Orodha ikitajwa JK atasema "ukiwakamata wauzaji wote wa dawa za kulevya Nchi itayumba". Kwahiyo Maaskufu wapige kimya kama yeye JK alivyo potezea..
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  au wamtaje JK mwenyewe najua watajibu mashambulizi kama walivyo fanya kwa wamiliki wa Dowans ingawa tulitajiwa wakurungezi...
   
 17. M

  MPG JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kuona RAIS mlopokaji kama huyu KIKWETE wa CCM,Sasa kazi anayo mpaka watumishi wa IKulu,wabunge,mawaziri....baba punguza kulopoka ona sasa utawala wako hautawaliki.ANGUKO LA CCM LIMETIMIA.
   
 18. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  mbu sugu, do you have any relationship with Malaria Sugu? being genetically, ideologically etc. Thank you
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Lakini pia tuwe macho sana na mwamalanga ni mchungaji tapeli hana kanisa analiongoza pale Mbeya mjini na hata hawajibiki kwa kanisa lolote hapa nchini linalomtambua uchungaji wake.

  Huyu hana tofauti na Christopher mtikila, sio vema akatumia jina la mchungaji kutia uzito habari yake lakini kama ilivyo kwa Watanzania wote kuwataja kwa majina watu hao itakuwa ni uzalendo wa juu sana na tunaomba Mungu amtie nguvu ili aweze kuwataja kwa majina.

  Hata hivyo, nina mashaka kwa jinsi ninavyomfahamu Mwamalanga anapenda sana kupata umaarufu kwa njia kama hizo na mwisho wake hatatekeleza kile ambacho wengi tunasubiri kwa hamu kubwa kutoka kwake.

  Haya JF tuelekeze macho na masikio yetu Dodoma kwa Mwamalanga pengine safari hii itaibuka kuwa Mwamalanga tofauti.
   
 20. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hawa nao msaada less, tangu mwaka 2006 wanahiyo list wamekaa nayo?
  Watoto au wa Tanzania wangapi wameangamia tangu wawajue hao wauza unga?
  Hawa pia wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuficha waharifu kwa muda wote huu 5 years.
   
Loading...