MBEYA: Kanisa kutoa orodha ya wauza unga

MBEYA: Kanisa kutoa orodha ya wauza unga

Nipo hapa Nyerere Square tangu asubuhi. Mbona hawatokei au wanafanyia wapi
 
sina uhisiano wowote na malaria sugu japo mimi ndiye mbu sugu niliyemuuma na kusababisha kichwa chake kushindwa kufikiri vema. Ukifuatilia thread zangu hazifungamani na mtazamo wa huyo bwana.... kimsingi najivuna kutokuwa ndugu yake hatulingani katika fikra zetu.
 
Kila mtu akimpelekea orodha Rais ya wauza madawa na kumtaka atangaze bila kujali kwamba ni kweli au la mmmmmh nchi italipuka. Mtu akichukua mke wangu kwa hasira namtangaza kwa Rais ni muuza madawa wapi na wapi? tutafika?
 
Hawa nao msaada less, tangu mwaka 2006 wanahiyo list wamekaa nayo?
Watoto au wa Tanzania wangapi wameangamia tangu wawajue hao wauza unga?
Hawa pia wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuficha waharifu kwa muda wote huu 5 years.
Mkuu hata JK alisema anawajua...sasa mkuu wakaya kama alisema anawajua na akaa kimya wewe sisimizi utakuwa na kiherehere gani tena sanasana wata ku-Amina
 
mtu tapeli utamjua tu.... anajiita mchungaji wakati sio kweli lakini hapohapo anataka akitoa taarifa kwa uuma zikubarike kwa jamii. Yuko pale mbeya mjini anaendesha kampuni ya kitapeli ya mazingira ni katika mtindo wake huo huo. ndio maana nasema tuwe na subira pengine safari hii hatakuwa mwamalanga yule yule ninayemfahamu.
 
Hata obama alisema anawajua vigogo wa madawa ya kulevya lakini wapo aliowataja na wengine kasema akiwataja sasa atakuwa anaingilia hatua za uchunguzi?
 
na Betty Kangonga

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Pentecost Church (TEC) la mjini Mbeya, William Mwamalanga, amesema wanatarajia kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kutaja hadharani orodha ya vigogo wanaoshiriki katika biashara ya dawa za kulevya.

Kauli ya mchungaji huyo imekuja siku moja baada ya Ofisi ya Rais (Ikulu) kuwataka maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kuacha kutoa saa 48 kwa Rais Jakaya Kikwete kutaja majina ya viongozi wanaouza dawa za kulevya bali yeyote anayejishuku ajisamilishe au atajwe.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mwamalanga alisema kundi la viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali wamepanga kukutana kwa ajili ya kutaja majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo.

Alisema wanatarajia kutaja majina yote, si ya viongozi wa dini ya Kikristo pekee, bali hata wale waliopo nje ya Ukristo, ambao taarifa zao zimefika hadi kwa Rais Kikwete.

"Si kwamba tutataja majina ya maaskofu na wachungaji pekee, bali tutataja hadi wale waliomo ndani ya Ofisi ya Rais, ambao wanafanya biashara hiyo, wabunge pamoja na mawaziri," alidai mchungaji huyo.

Alisema wana taarifa kamili ya viongozi wa dini ambao wanatumia makanisa kama vivuli na kujificha, kumbe wanaendesha biashara hiyo haramu inayoangamiza taifa.

Mchungaji Mwamalanga alisema lengo ya kutaja majina hayo hadharani ni kutaka kumsaidia Rais Kikwete na kuisafisha nchi iondokane na uingizaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

"Kwa sasa tupo Dodoma na leo tunatarajia kutaja majina hayo ambayo Rais Kikwete anashindwa kuyataja, ili kumsaidia …maana taarifa za orodha hiyo tuliwahi kumfikishia katika ofisi yake mwaka 2006," alisema.

Alisema viongozi wa dini wanaotumia makanisa kama vivuli huku wakiendesha biashara hiyo wanafahamika wazi, lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua.

Aliongeza kuwa wanategemea kuwa orodha hiyo ikiwekwa hadharani wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachunguza.

Alibainisha kuwa kama vyombo vya dola vitapuuzia orodha hiyo watakayoitaja, kamwe mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayawezi kuzaa matunda.

Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Rais Kikwete akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Killian katika sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo, kuwa askofu wa Jimbo la Mbinga, alikaririwa akisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Kauli hiyo iliwafanya maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Baada ya tamko hilo, juzi Ofisi ya Rais Ikulu iliwakosoa viongozi hao kwa kutoa tamko la kusikitisha, ambalo ililiita kuwa halikustahili kutolewa nao.

Ikulu iliweka bayana kuwa viongozi wa dini si malaika au watakatifu hapa duniani, kwani wanaweza kutumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa katika jamii.


Source: Tanzania Daima.

Angalizo langu: Ni mpambano kati ya Kanisa na Rais. Nafuu itakuwa kwa sie walalahoi kwani wauza unga wanaiharibu jamii na kama ni watu wenye nguvu basi nafikiri mahakama ya umma inawatosha kuwahukumu. Nawapa hongera sana maaskofu kwa ujasiri wenu watajeni jamii iwahukumu!!!!

Naomba kunukuu" Alisema viongozi wa dini wanaotumia makanisa kama vivuli huku wakiendesha biashara hiyo wanafahamika wazi, lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua." mwisho wa kunukuu.

Maneno hayo hapo kayaongea mtu wa TEC sasa yule askofu wa CCT ampe masaa 48 tena. Hapa Mokiwa anaenda kuumbuka, kwani raisi anawasemaji wengi, na atakuwa kawateuwa hao wa TEC wamjibu Mokiwa. TEC watajeni wote bila kuficha.
 
Binafsi sina ugomvi na mwamalanga na nitampongeza sana akitaja orodha yake lakini Jf naomba fuatilieni jina hili la mwamalanga huko mbele mtakuja kukubaliana na mimi kuwa ni mtu hatari anayejivika uchungaji ambao hakuwahi kusomea popote na ndio tatizo la waandishi wa habari wetu hawafuatilii hadhi hiyo kaipata kutoka chuo kipi au yeye yuko chini ya askofu yupi hapa nchini ama dhehebu lipi la dini ya kikristo hapa nchini ambalo linamtambua.
 
Tukumbuke pia kwamba hii sio mara ya kwanza kwa mwamalanga kuutangazia umma kwamba ana orodha hiyo na kutoa ahadi ya kuitangaza hadharani. kama nakumbuka ni mara ya nne sasa.
 
Naomba nisieleweke kwamba napinga vita dhidi ya dawa za kulevya ila tu sina imani na mwamalanga na ili imani yangu irudi kwake ni mpaka pale atapotangaza orodha hiyo. Kimsingi, mimi najua ni tapeli anayeishi kwa ujanja janja siku za kuishi zinasogea.
 
au wamtaje JK mwenyewe najua watajibu mashambulizi kama walivyo fanya kwa wamiliki wa Dowans ingawa tulitajiwa wakurungezi...

naona hamjaielewa hiyo taarifa. wamesema wao ndio walio mpelekea raisi orodha ya majina, nadhani kama jina la raisi lingekuwemo wasingempelekea na bado wamesema maneno yale yale aliyoyaongea Rais j2 iliyopita kule Iringa kuwa "Alisema viongozi wa dini wanaotumia makanisa kama vivuli huku wakiendesha biashara hiyo wanafahamika wazi, lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua." na maofisa ndani ya ofisi ya Rais hawajasema rais. sasa raisi anaweza kuwa alishindwa kutaja yeye, kwahiyo kawaomba walewale waliompelekea ndio wayataje ambapo kwa statement ya hao TEC inaonekana CCT watakuwemo wengi kwenye orodha hiyo. JK kawapambanisha Drug dealer yetu macho na masikio.
 
jk lazima awe ndani, ......... zile zilikuwa dili zake alipokuwa waziri wa mambo ya nje! ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mnataka ajitaje mwenyewe???????
 
Kuna mtu aliwahi niambia kwamba mwamalanga ana tabia ya kuwa na orodha ya majina na kisha anawafuata baadhi ya watu kwamba majina yao yako kwa Rais, polisi na Usalama wa Taifa kwa hatua lakini wale wenye kuamini kwamba wanaweza kubambikiwa kesi kwa hofu tu wanampatia fedha huyu mchungaji mwamalanga na hasa wahindi wakati sio kweli lakini kwake anasogeza siku za kuishi duniani. Inaelezwa kwamba katika utapeli wake amejiweka karibu sana na baadhi ya viongozi wa kisiasa, wakuu na maafisa wa vyombo wa dola kwa kivuli cha uchungaji. Kamwe huwezi kumkuta yuko karibu na viongozi wengine wa dini kwani watamshitukia
 
Jamani hebu tusaidia

Unajua mtu ukisoma kwa mara ya kwanza hii habari unajua TEC na CCT wamekaa na kuandaa haya.... ati kanisa kutoa orodha, ni bora wangesema kanisa la pentekoste mbeya kutoa orodha

i think it is an intentional move by the media to magnify bullshit na kuendelea kugombanisha wakristu na wanasiasa

sijui inatufikisha wapi hii fooking move
 
Mi JK ananishangaza sana................
Ile orodha ya waharibifu wa bandari anayo.......... lakini hajafanya kitu.......
Orodha ya wahusika wa mishahara hewa ................. anayo hajafanya kitu.............
Meremeta................ hata muwasulubishe hawafanyi kitu...................
Huyo askofu kasema orodha ya wauza unga unayo toka 2006............ hujafanya kitu..........
Mafisadi orodha unayo........................... umewashindwa..................

JK....... KUISHIA KUFAHAMU ORODHA TU HAKUTAKUSAIDIA KITU KATIKA HIZI HARAKATI ZA KUVUANA MAGAMBA.....................KWENYE HILI LA MADAWA MMENIKUMBUSHA AMINA CHIFUPA

alichokifanya kawarudishia walio mpelekea hiyo orodha waisome wao wenyewe, sasa wasingeshitukiza kuisoma kwahiyo aliwatafutia kasi ya kuisoma na TEC wakauchuna kwanza ili CCT wajiingize kichwakichwa kisha TEC wafanye mambo. sasa subiri waisome, maana ikisomwa na TEC ndio patakuwa patamu kwani angesoma JK mfano akamtaja askofu wako ungesema ameleta udini, sasa kawaachia TEC kwani wao wakimsoma askofu wako hutoweza sema wameleta udini. jamani wachangiaji msikurupuke kuchangia isomeni hiyo muielewe vyema. majibu hayo ya TEC ni mtihani mkubwa kwa CCT na mokiwa wake
 
Huyu anacheza watamchifupa subirini tu muone
 
Jamani, wauza unga wanajulikana. Hata jf humu wamo. Tutaje list yetu. Mimi namjua mmoja. Kwa ruksa ya mods nitamtaja.
 
Back
Top Bottom