Mbeya: Jiji au Kijiji kikubwa?

Mbeya: Jiji au Kijiji kikubwa?

Mbeya ni Kijiji Kikubwaaa! Tatizo kubwa linalofanya maendeleo ya Mbeya yadorore ni tabia ya vijana haswa wazawa kuukimbia mji wao, wengi wanakumbilia Dar hawana mzuka wa kuendeleza kwao.
We hujui lolote kuhusu Mbeya, research yako ni hopeless kabisa . Ktk watu wanaoongoza kupenda kwao ni watu wa nyanda za juu. Mbeya ni moja wapo ya mji pekee ambao unajengwa na unaendelea kwa kazi na juhudi za wenyeji wenyewe bila nguvu ya serikali (kama ilivyo Dodoma, Arusha na Dar) .
Vijana wa Mbeya ni wachapa kazi na kazi za kufanya Mbeya zipo za kutosha. Sio kweli kabisa hoja yako
 
Nadhani kuna sehemu sisi kama watanzania tunakwama sana.

Nani alisema uwepo wa wapishi wazuri wa chakula ni miongoni mwa vigezo vya sehem kupandishwa hadhi kuwa jiji?
Mbeya hakuna nyumba nzuri, uzuri wa nyumba ni nini? utakuta unajisifia tu lakini unakotoka nyumba nzuri zilizopo sio zenu ni za mashirika ya serikali au hotel za kitalii na wewe kwenu na wazazi wako mnakaa nyumba za tembe.

Kila sehem ina umaarufu wake na Jiji la Mbeya maarufu si kwa Majengo au upishi wa chakula.
Muhimu ukifika sehem shughulikia lililokupeleka kuliko kuanza kuchunguza mambo ambayo hayana msaada kwako,, au wewe ni afisa mipango miji?

Tumechoka na thread zenu za kuisema Mbeya , sisi wenyewe wana Mbeya tumeridhika na jiji letu maana Kisoka tupo vizur , kielim tupo vizur, nguo na viatu vinapatikana kwa wing na ubora mzur. Chakula na matunda ndio usiseme.

Mwisho. Ukiona Mbeya kuwa jiji wewe inakuuma sana nenda Mahakamani fungua kesi ya madai ya kutaka Mbeya iondolewe hadhi hiyo ili wewe uridhike.
Mmaa gwee asukile na kumaso issaa kofiki? Tunkolileeko kuno uswe? Akomile ingafi
 
Acha dharau wewe!!!. Mtu wa aina yako Ukute unatokea huko Katerero -Bukoba.
Haijalishi natokea wapi. Hiyo hakuifanyi Mbeya isiwe kijiji kimoja kikubwa! Kitakachobadilisha ni wanambeya wenyewe kupambana na kuijenga Mbeya yao.
 
Kwa kuongeza Mbeya ni mji ambao wakazi wake wengi wana uhakika wa milo mitatu tofauti na karibia miji yote Tanzania.

Kuna watu wanaishi Mbeya wanamaisha mazuri kushinda aliyeko Dar au hata pale Washington.

Thread yako haina mashiko unakejeli tu ,ungekuwa muungwana ungetoa mawazo nini kifanyike pia ili kuwe na hadhi nzuri zaidi ila umeishia kukeji tu,

Kila mji una mazuri yake na mapungufu yake , Kufika kwenye miji ya watu huna hata wiki unaanza kukejeli bila ushauri pia sio vizuri ,


By the way Dar ni kijiji kikubwa cha wala lala hoi. (Wengi wao)

Watu wa Mbeya wanaishi maisha mazuri sana kushinda wa Dar es salam .kwanini

Mazingira mazuri sana ya Mbeya
Hewa safi
Wengi wana uhakika wa milo mitatu
Wengi wana uhakika wa mahali pa kulala
Usafiri wao wa uma (daladala ) ni mzuri sana kushinda miji yote Tanzania.
Uhakika wa huduma ya maji
Kuna makazi mazuri sana Ituha ,iwambi ,forest ,isyesye na igawilo ya juu yenye hadhi ya Copenhagen


Usafiri wa barabara ,ngege na treni upo wa kuufikia mji.


Mbeya pale bana pako vizuri kiasi chake acha nongwa Mkuu

Pia uswahili nayo mbeya inayo mitaa kama isanga ,mabatini, ccm,Makondeko ,isengo ,majengo kule.



Mbeya ilipewa hadhi sababu ya idadi ya watu, pia mbeya hamna majengo marefu sababu ni eneo la bonde la ufa ,ni mji pia ulio telekezwa na serekali ya Mh Jiwe.

NB. Mimi sio mzaliwa wa Mbeya wala sijakulia Mbeya .Harakati za maisha zimenifanya tu nikujue.
Hapo uliposema "yenye hadhi ya Copenhagen" hebu temea mate chini mkuu!!
 
Kwa hadhi ya Tanzania yetu Mbeya ni jiji kutokana na idadi ya watu pia mapato. Lakini pia kama ukiwa umesafiri walau nchi za Ulaya na Asia utakuja kusema pia Dar es salaam Sio jiji ni kijiji. Angalia mafuriko yaliyopo baadhi ya mitaa Dar es salaam. Angalia sqatas zilizopo Dar es salaam . Kwa level ya Tanzania Mbeya ni jiji
Hiyo idadi ya watu yenyewe hata siioni. Yaani barabara zimepoa hizo utasema watu wamekimbia vita
 
Hiyo idadi ya watu yenyewe hata siioni. Yaani barabara zimepoa hizo utasema watu wamekimbia vita
Dada yangu Mimi nmeishi Mbeya . Kweli kabisa mwanjelwa na kabwe mpaka mitaa ya mama John huoni msululu wa watu. Kwa kweli Mimi niliishi Mbeya Mwaka 2014 na mara ya mwisho kwenda ilikuwa 2015 . Watu walikuwa wengi tuu. Huoni movement ya dalala kweli. Hiyo stendi ya Kabwe na Mwanjelwa labda sijui kwa sasa pamekuwaje. Ila kule Mbeya mjini kabisa ndio utaona mvt ya watu ni chache kabisa. Biashara zilihamia Mwanjelwa na Kabwe huko. Ila kwa Tanzania jiji angalau ni Mwanza na Dar es salaam haya mengine yaliyobaki ni majiji ya kisiasa tuu. Kuanzia Mbeya, Dodoma, Tanga na Arusha. Hata hivyo haya majiji yote ya angalau bado miundombinu Sio mizuri mfano Dar es salaam na Mwanza hakuna flyover na shopping malls nzuri. Kwa mwanza ipo Rockcity shopping malls Ila bado haijachangamka na kwa Dar ipo mlimani city . Bado nchi yetu tuna safari ndefu ya kwenda kwenye maendeleo. Kwa kawaida kutokana na idadi ya watu Dar es salaam Ilibidi iwe na high speed railways ili na fly over ili kupinguza foleni
 
Labda kwanza turudi kwenye vigezo vilivyofanya iitwe Jiji.
Nimefika Mbeya nimechoka mwenyewe. Nyumba nyingi siyo nzuri. Chakula kwenye migahawa usiseme. Yaani hamna kitu kwa kweli. Kazi ya ziada inahitajika. Bado saaaana
 
Nimefika Mbeya nimechoka mwenyewe. Nyumba nyingi siyo nzuri. Chakula kwenye migahawa usiseme. Yaani hamna kitu kwa kweli. Kazi ya ziada inahitajika. Bado saaaana
Tumia akili kidogo umepewa bure na Mungu.

Umefika Mbeya sehemu gani? Umetembelea maeneo gani? Yataje japo machache tu. Unaweza kufikia Uyole na ukaishia huko na ikawa ndiyo picha yako kamili ya Mbeya. Ni sawa na kufikia Buguruni kwa Mnyamani useme umefika Dar umekuta hali si nzuri. Au umefika kwa Mrombo Arusha na ikawa ndiyo picha ya Arusha nzima kwako.

Nimesema tumia akili kidogo. Umepewa bure hujanunua. Ili eneo litangazwe kuwa jiji lazima likidhi vigezo fulani. Mbeya ilikidhi siku nyingi mno. Unavijua vigezo hivyo? Sema kipi kimepwaya kwa Mbeya. Usidhani mtu anaamka usiku na kusema eneo fulani ni jiji. Sio kwa majiji tu, hata miji midogo ina vigezo vyake kadhaa.

Hujiulizi kwa nini miji mingine mingi tu sio majiji? Vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
Mbeya ni Kijiji Kikubwaaa! Tatizo kubwa linalofanya maendeleo ya Mbeya yadorore ni tabia ya vijana haswa wazawa kuukimbia mji wao, wengi wanakumbilia Dar hawana mzuka wa kuendeleza kwao.
Ungeanza kusema kwenu wapi kwanza halafu ndo useme kwa wengine. Tuambie kwenu wapi ili tulinganishe na Mbeya.
 
Back
Top Bottom