Mbeya: Jiji au Kijiji kikubwa?

Mbeya: Jiji au Kijiji kikubwa?

Mbeya wanaongoza kwa kulima mchele lakini cha ajabu ukienda migahawani chakula ni kibaya, labda ujipikie mwenyewe.

Mji una majengo ya kawaida na mengine ni ya zamani yaliyochakaa, ukiachana na town centre pale kwenye jengo la nssf unagundua kabisa hakuna majengo mengine yenye mvuto wa kushangaza, labda uende tena kusafisha macho jengo la city pub pale, zaidi ya hapo ukienda Soweto, mwanjelwa, kabwe, mamajoni, sinde, na maeneo mwengine ya kwenye barabara unaona kabisa majengo ni ya kawaida sana na mbaya zaidi kuna majengo yana bati za miaka ya 90 hadi yamebadilika rangi.

Mbeya inadorora kwenye sekta ya bata, yani mbeya ukiachana na city pub inatia Huruma, hakuna kumbi za cinema, sehemu za swimming pool nahisi ni moja pale forest sheli ya mafuta, night clubs za kawaida mno na zimedorora, burudani za shoo za wasanii ni kama hakunaga kabisa maana hata wasanii wakija wanaoenda kucheki show ni wachache sana, n.k

Mbeya bidhaa nyingi za kisasa na orijino upatikanaji wake ni shida, ukitaka kununua kwa mfano Samsung galaxy s10 au iPhone latest kwa mbeya kupata ni kazi sana labda uagize, hata maduka yao vinara kama Dubai electronics pale mjini kukuta hivi vitu labda iwe kwa order.

Shule za international syllabus, ukiachana na shule hizi zinazofata mitaala ya Necta jiji la mbeya hakuna hata shule moja ya kimataifa inayofata mitaala ya syllabus za kimataifa kama Cambridge, hata iringa wana shule ya aina hii unaitwa iringa international school, kwa arusha na dar zipo kama international school of Tanganyika, braeburn, international school of moshi, Kentucky, n.k

Magari- najua sio sifa ya jiji lakini bado imebidi nigusie kwasababu nikivuta picha ya majiji kama dar, mwanza na Arusha na hata baadhi ya mikoa kuna nyomi ya mashine za kibabe kuanzia range rovers, bmw za bei mbaya, bentley, porsche, benz za kibabe, n.k ila kwa mbeya niwe mkweli tu kwamba hakunaga magari labda tuviite vyombo vya usafiri, yani hata range rover ipo ile toleo la zamani na inatumika kwenye maharusi

Nguvu za Giza: kuna matukio mengi kiasi ya kuashiria kuwepo utumiaji nguvu za Giza ili watu wawe matajiri kwa mfano matajiri wengi wa mbeya wafanyabiashara wanaaminika kupata utajiri wao kwa booster ya kafara za kichawi kugeuza watu misukule , pia imetokea Mara kwa mara watoto wanaozikwa baada ya kipindi wanaonekana mitaani, makaburi hufukuliwa na watu kushangazwa na migomba iliyomo kwenye majeneza badala ya maiti iliyoshuhudiwa ikizikwa.

Vyuo- ukiachana na chuo cha MUST kwengine vyuo vina changamoto, ukianza kule block t chuo cha teku hakina hadhi na kwa sasa wamefungiwa kudahili wanafunzi wa degree, ukija foresti kuna tawi la mzumbe ni kichekesho maana eneo ni dogo na hakuna hata chumba cha computer za wanafunzi na hostel ni ndogo, ukija chuo cha cbe wana kaeneo kadogo kiasi kwamba wamekodisha ukumbi wa bar ya b.o.t sehemu ambayo ni ya starehe na inatishia usalama wa wanafunzi wa kike, pia maisha ya geto kwa mwanafunzi wa chuo wa mbeya nayo ni shida maana kuoata geto standard kwa mbeya ni pasua kichwa.

Usafiri wa anga nao umeanza kudorora kwa spidi ya juu mno baada ya fastjet kufyekelewa mbali, hii ni kutokana na wana mbeya wengi kutoweza kuhimili bei za air Tanzania ambazo zipo juu tofauti na hapo zamani kwa fastjet ambao hata ukiwa na elf 60 uliweza kuruka mbeya hadi dar, Hali ya uwanja wa songwe kwa sasa ni mbaya na hata shuttle na taxi zimepungua kwa sababu abiria wamepungua sana na pia air tanzania inakuja Mara chache sana

Shopping mall- lile soko kuu la kimataifa la pale mwanjelwa limedorora sana, hata ukiingia kufanya shopping unaweza kuahirisha.
 
Yn ww hapo hujaangalia sifa za jj Bali umefanya Ku compare mby na dar ki2 unachojua kabsa hakiwezekan
 
Jamani mbeya kibongo bongo iko okey!! Nmepita majiji kama Milan,Newyork, Washington DC,Paris na Munich kidogo yani ukitoka kwenye haya majiji ukatupwa dar utasema umeshushwa toka peponi kwenda jehanam,tupigane tujenge miji yetu ipendeze dar nayo bado xana tena xana tu
 
Five star hotel in mbeya city
everydaymbeya_1___BxktVVRldoI___.jpeg
 
Kwa kuongeza Mbeya ni mji ambao wakazi wake wengi wana uhakika wa milo mitatu tofauti na karibia miji yote Tanzania.

Kuna watu wanaishi Mbeya wanamaisha mazuri kushinda aliyeko Dar au hata pale Washington.

Thread yako haina mashiko unakejeli tu ,ungekuwa muungwana ungetoa mawazo nini kifanyike pia ili kuwe na hadhi nzuri zaidi ila umeishia kukeji tu,

Kila mji una mazuri yake na mapungufu yake , Kufika kwenye miji ya watu huna hata wiki unaanza kukejeli bila ushauri pia sio vizuri ,


By the way Dar ni kijiji kikubwa cha wala lala hoi. (Wengi wao)

Watu wa Mbeya wanaishi maisha mazuri sana kushinda wa Dar es salam .kwanini

Mazingira mazuri sana ya Mbeya
Hewa safi
Wengi wana uhakika wa milo mitatu
Wengi wana uhakika wa mahali pa kulala
Usafiri wao wa uma (daladala ) ni mzuri sana kushinda miji yote Tanzania.
Uhakika wa huduma ya maji
Kuna makazi mazuri sana Ituha ,iwambi ,forest ,isyesye na igawilo ya juu yenye hadhi ya Copenhagen


Usafiri wa barabara ,ngege na treni upo wa kuufikia mji.


Mbeya pale bana pako vizuri kiasi chake acha nongwa Mkuu

Pia uswahili nayo mbeya inayo mitaa kama isanga ,mabatini, ccm,Makondeko ,isengo ,majengo kule.



Mbeya ilipewa hadhi sababu ya idadi ya watu, pia mbeya hamna majengo marefu sababu ni eneo la bonde la ufa ,ni mji pia ulio telekezwa na serekali ya Mh Jiwe.

NB. Mimi sio mzaliwa wa Mbeya wala sijakulia Mbeya .Harakati za maisha zimenifanya tu nikujue.
Wana uhakika wa milo mitano mana mwili wa mwana mbeya ni balaa
 
wewe kwanza ni maskini sana.... sasa si umeenda kwa mama ntilie kutokana na kipato chako??? sasa wewe unataka wali kuku kwa buku jero ..... unapata kutokana na hela yako mbwamwitu ww!!! jiwe mwenyewe anaifahamu na kuiheshimu mbeya..... unasema eti nyumba??? fala kweli ww.... wapi mkoa gani umeenda umekuta magorofa matupu maskini ww.....


mbeya ni nchi
 
Umeandika mithili ya mshambuliaji wa football, anayewaza kushangilia badala ya kufunga. Matokeo yake hafungi, na hatoshangilia. Mie si mwenyeji wa mbeya, lakini naifahamu mbeya, Arusha, dar, na mwanza. Je, haya yanastahili kuwa majiji, ukilinganisha na paris?....siku Dodoma ikiwa jiji uje uandike tena, maana utaandika sana this time. Hahahaha! Penda vyako.
 
Naona wanafunzi wamefunga shule wameamua kuufufua tena huu uzi, tushaufunga kitambo sana
 
Back
Top Bottom