Mbeya: Hakimu wa Mahakama ya Wilaya auawa kwa kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira kali

Dah! Tukio Hilo nalifananisha na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa Mwanza ndg Mabina, Cha muhimu tuache kiburi cha wadhifa, cheo au ukwasi kuonea wengine.
Yaanih umepiga mlemle, nilipokua nikisoma nilikua napata picha ya Mabina tuu.
 
Sio ajabu Kuna mgosi alikua amepania kumfunga kule Handeni. Mgosi akaenda kwa wataalam (Kama kawaida Yao) mtaalam akasakizia kifo mbaya wa mgosi na kumuambia ' huyu harudi Handeni Tena.
Handeni isikie kwenye redio tu.
 
Nimekutana na hili andiko kwenye mitandao yetu hii, naamini mamlaka zitatuambia ukweli wa hii kitu....

Anaandika Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh. Siriel Mchembe👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

Niimepokea taarifa kutoka kwa DC Rungwe Dkt. Vincent Anney kwamba alfajiri ya leo, Hakimu Joakim Mwakyolo wa Mahakama ya Wilaya hapa Handeni ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko Busokelo Tukuyu/Rungwe.

Marehemu alikuwa likizo maana huko Rungwe ndipo anapotokea.

anzo cha kuuawa ni Mgogoro wa Ardhi kati yake na wanakijiji hicho anachotoka.

Alishindwa kesi ya ardhi Mahakama Kuu dhidi ya kijiji, lakini baada ya muda akaonekana kwenye eneo la Mgogoro akiwa ameongozana na Watu wawili.

Inadaiwa kuwa yeye na watu hao wawili kuna vitu walikuwa wanavichimbia ardhini kwenye eneo hilo la mgogoro jambo ambalo lilitafsiriwa na wanakijiji kwamba ni ushirikina.

Wananchi walipowazonga watatu hao na kuwahoji kuhusu suala hilo, ugomvi ukatokea kati yao, jambo lililopelekea mmoja wa watu waliokuwa na Hakimu huyo kuwapiga risasi wanakijiji wawili miguuni.

Baada ya hapo wananchi wakapandwa hasira na kumshambulia kwa mawe na silaha mbalimbali Hakimu huyo pamoja mmoja wa watu aliokuwa nao, huku mwingine akitoweka kuelekea kusikojulikana.

Hivyo vifo vilivyoripotiwa ni viwili. Hakimu pamoja na mmoja wa watu alikwenda nao kwenye eneo la mgogoro.

Pole sana Mhimili wetu wa Mahakama, hasa Hakimu wa Wilaya Handeni Mhe.Sabuni kwa kuondokewa na mtumishi huyu.Poleni ndugu zangu wa Handeni.

Tuwaombee pumziko la amani - Amina.

===================

TAARIFA RASMI YA MKUU WA WILAYA

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dkt. Vincent Anney amesema “Ni tukio la kweli, Hakimu alikuwa na mgogoro na Wanakijiji, yeye si mwananchi wa Rungwe ila alinunua eneo Rungwe.

“Zamani baba yake alikuwa anaishi Rungwe akahamia Kyela, hata yeye Hakimu alizaliwa hukohuko Kyela. Hapo kati alianzisha mgogoro na wananchi akisema anataka eneo la babu yake lakini hiyo ni sehemu nyingine, si seheu amayo tukio limetokea.

“Eneo ambalo limesababisha auawe ni kubwa kuna karibia ekari 1000, ni msitu na ni hifadhi ambayo imekuwa ikisadia mvua, alinunua kinyemela, wananchi wakamshtaki Mahakamani.

“Akashindwa kesi, alikuwa katika harakati za kukata rufaa, kesi ikiwa imeisha akaenda shambani akiwa na watu wengine wawili akaanza kuchimbachimba, inasemakana alikuwa anachimba dawa.

“Yakatokea majibizano kati yake na Wananchi waliofika eneo hilo, akatoa bastola na kuwapiga risasi Wananchi wawili miguuni.

“Wananchi wakakasirika na kuanza kumpiga kisha kusababisha kifo chake pamoja na mmoja kati ya wale watu wawili alioongozana nao, mwingine mmoja alitokomea haijulikani alipokwenda.

“Tumeshawakamata watu kama saba hivi kutokana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea.”
Niwaonye tu wenye mwelekeo wa kibwanyenye kwamba watanzania hawataki dhuluma za ardhi. Ukiwa unaamini awamu hii ataweza kuwadhulumu wanakijiji ardhi yao fikiria tena.
 
Unajiamini kwa watu wa kijijini wenye umoja watakuua hao.
Picha linaanza angeanza kwa kuangalia kwenye huo mgogoro ni wananchi wangapi walikua wakijitokeza mahakamani. Kama ni wengi angeufyata tu maana wakiwa na umoja hao chuki yao hurithisha vizazi na vizazi.
 
Hakimu hakuheshimu hukumu iliyotolewa na mahakama ikiwa yeye ni expert katika masuala ya kesi na sheria....alale anapostahili
Alifanyaje kwani zaidi ya kuchimbachimba sijui dawa, wangemuacha achimbe hizo dawa aondoke zake
 
Siku zote napinga suala la kumiliki silaha, ukiwa na silaha za moto unakuwa ni mwenye kijiamini kupita maelezo, hapo hakimu asingekuwa na silaha pengine wangeweza kuzungumza na yakaisha.

Jambo lingine, serikali iangalie hawa watu waliopewa Mamlaka ya uamuzi. Hakimu mzima umeshindwa kwenye kesi badala ukate rufaa unalazimishia mabavu, yawezekana hata hukumu zake ni za kijanjajanja.

Wananchi waliotenda jinai hiyo pia ni wahalifu. Kuua mtu sio suluhisho ila ni kuongeza ukubwa wa tatizo. Hao wahalifu wasakwe.

Yote kwa yote , Mungu azipumzishe roho za Marehemu mahali pema peponi na majeruhi awape uponyaji wa haraka.
Kosa la hakimu hapo ni kuchimbachimba au? Sioni sehemu kama alivunua sheria yoyote
 
Kushindwa kwake ilikuwa halali ndio maana akaona atumie ndumba kupindua mambo. Angejua hata bastola hangeitoa.
.
 
Alienda kufanaya nini teena, wakati angesubiri rufaa. Kwanini achimbe chimbe au bastola aliiona dili kwake?
 
Huyo hakimu fala sana aliamini wanakijiji wameroga nadhani alikuja na uchawi wake umsaidie rufaa chizi kweli huyo, mijitu kama hio ife tu tena sio ya kuionea huruma, watu wa sheria ni madevil they're not God believers most of them, very selfish Carrier.
Alafu ulichosema ni kweli kabisa,Watu waliosomea Sheria Wana viburi sana na kujisikia, kuliko hata ma engineer au ma doctor wenye taaluma ngumu!!
 
Kuna tofauti Kati ya KUSOMA na KUELIMIKA sasa mtu ambaye ni mwanasheria kitaaluma anaposhindwa kuheshimu maamuzi ya mahakama huyo kasoma ila hajaelimika
Elimu haitoi ubinaadam mkuu, huyo ni munyama mwenye elimu.Si umesikia na risasi zilikuwemo.
 
Back
Top Bottom