Mbeya: Hakimu wa Mahakama ya Wilaya auawa kwa kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira kali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Nimekutana na hili andiko kwenye mitandao yetu hii, naamini mamlaka zitatuambia ukweli wa hii kitu....

Anaandika Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh. Siriel Mchembe👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

Niimepokea taarifa kutoka kwa DC Rungwe Dkt. Vincent Anney kwamba alfajiri ya leo, Hakimu Joakim Mwakyolo wa Mahakama ya Wilaya hapa Handeni ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko Busokelo Tukuyu/Rungwe.

Marehemu alikuwa likizo maana huko Rungwe ndipo anapotokea.

Chanzo cha kuuawa ni Mgogoro wa Ardhi kati yake na wanakijiji hicho anachotoka.

Alishindwa kesi ya ardhi Mahakama Kuu dhidi ya kijiji, lakini baada ya muda akaonekana kwenye eneo la Mgogoro akiwa ameongozana na Watu wawili.

Inadaiwa kuwa yeye na watu hao wawili kuna vitu walikuwa wanavichimbia ardhini kwenye eneo hilo la mgogoro jambo ambalo lilitafsiriwa na wanakijiji kwamba ni ushirikina.

Wananchi walipowazonga watatu hao na kuwahoji kuhusu suala hilo, ugomvi ukatokea kati yao, jambo lililopelekea mmoja wa watu waliokuwa na Hakimu huyo kuwapiga risasi wanakijiji wawili miguuni.

Baada ya hapo wananchi wakapandwa hasira na kumshambulia kwa mawe na silaha mbalimbali Hakimu huyo pamoja mmoja wa watu aliokuwa nao, huku mwingine akitoweka kuelekea kusikojulikana.

Hivyo vifo vilivyoripotiwa ni viwili. Hakimu pamoja na mmoja wa watu alikwenda nao kwenye eneo la mgogoro.

Pole sana Mhimili wetu wa Mahakama, hasa Hakimu wa Wilaya Handeni Mhe.Sabuni kwa kuondokewa na mtumishi huyu. Poleni ndugu zangu wa Handeni.

Tuwaombee pumziko la amani - Amina.

===================

TAARIFA RASMI YA MKUU WA WILAYA

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dkt. Vincent Anney amesema “Ni tukio la kweli, Hakimu alikuwa na mgogoro na Wanakijiji, yeye si mwananchi wa Rungwe ila alinunua eneo Rungwe.

“Zamani baba yake alikuwa anaishi Rungwe akahamia Kyela, hata yeye Hakimu alizaliwa hukohuko Kyela. Hapo kati alianzisha mgogoro na wananchi akisema anataka eneo la babu yake lakini hiyo ni sehemu nyingine, si sehemu ambayo tukio limetokea.

“Eneo ambalo limesababisha auawe ni kubwa kuna karibia ekari 1000, ni msitu na ni hifadhi ambayo imekuwa ikisadia mvua, alinunua kinyemela, wananchi wakamshtaki Mahakamani.

“Akashindwa kesi, alikuwa katika harakati za kukata rufaa, kesi ikiwa imeisha akaenda shambani akiwa na watu wengine wawili akaanza kuchimbachimba, inasemakana alikuwa anachimba dawa.

“Yakatokea majibizano kati yake na Wananchi waliofika eneo hilo, akatoa bastola na kuwapiga risasi Wananchi wawili miguuni.

“Wananchi wakakasirika na kuanza kumpiga kisha kusababisha kifo chake pamoja na mmoja kati ya wale watu wawili alioongozana nao, mwingine mmoja alitokomea haijulikani alipokwenda.

“Tumeshawakamata watu kama saba hivi kutokana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea.”
 
F2C91290-EFD1-4CF2-AA11-C9E156F1DAEF.jpeg
 
Nchi hii migogoro ya ardhi inachochewa na wenye mamlaka. Kuna ardhi zaidi ya miaka ishirini mamlaka ya wilaya inatuzungusha kuja kuipima ama kutulipa fidia wachukue Sasa mambo Kama haya siyo kabisa. Ona Sasa mambo ya hovyo mtumishi wa mahakama kukosa uelewa wa Sheria.
 
Siku zote napinga suala la kumiliki silaha, ukiwa na silaha za moto unakuwa ni mwenye kijiamini kupita maelezo, hapo hakimu asingekuwa na silaha pengine wangeweza kuzungumza na yakaisha.

Jambo lingine, serikali iangalie hawa watu waliopewa Mamlaka ya uamuzi. Hakimu mzima umeshindwa kwenye kesi badala ukate rufaa unalazimishia mabavu, yawezekana hata hukumu zake ni za kijanjajanja.

Wananchi waliotenda jinai hiyo pia ni wahalifu. Kuua mtu sio suluhisho ila ni kuongeza ukubwa wa tatizo. Hao wahalifu wasakwe.

Yote kwa yote , Mungu azipumzishe roho za Marehemu mahali pema peponi na majeruhi awape uponyaji wa haraka.
 
Ndiyo Yale Yale ya mahakama kutoa zuio la kujenga, kubomoa Mali za wananchi ila serikali inafanya Kwa kiburi. Ipo siku tutatengeneza kina general Makenga.
 
Siku zote napinga suala la kumiliki silaha, ukiwa na silaha za moto unakuwa ni mwenye kijiamini kupita maelezo, hapo hakimu asingekuwa na silaha pengine wangeweza kuzungumza na yakaisha.

Jambo lingine, serikali iangalie hawa watu waliopewa Mamlaka ya uamuzi. Hakimu mzima umeshindwa kwenye kesi badala ukate rufaa unalazimishia mabavu, yawezekana hata hukumu zake ni za kijanjajanja.

Wananchi waliotenda jinai hiyo pia ni wahalifu. Kuua mtu sio suluhisho ila ni kuongeza ukubwa wa tatizo. Hao wahalifu wasakwe.

Yote kwa yote , Mungu azipumzishe roho za Marehemu mahali pema peponi na majeruhi awape uponyaji wa haraka.
Afrika ujinga ni tatizo kuu. Hakimu amekufa Kwa ujinga wake
 
Nchi hii migogoro ya ardhi inachochewa na wenye mamlaka. Kuna ardhi zaidi ya miaka ishirini mamlaka ya wilaya inatuzungusha kuja kuipima ama kutulipa fidia wachukue Sasa mambo Kama haya siyo kabisa. Ona Sasa mambo ya hovyo mtumishi wa mahakama kukosa uelewa wa Sheria.
Huyo hakimu fala sana aliamini wanakijiji wameroga nadhani alikuja na uchawi wake umsaidie rufaa chizi kweli huyo, mijitu kama hio ife tu tena sio ya kuionea huruma, watu wa sheria ni madevil they're not God believers most of them, very selfish Carrier.
 
Huko tu Kigoma Kuna mgogoro wa kanisa katoliki na CCM kisa chama hawataki kupisha eneo la kanisa, siku yakitokea na huko maafa tukutane hapa kupozana na kulaumiana, sooo fooooooool
 
Huko tu Kigoma Kuna mgogoro wa kanisa katoliki na CCM kisa chama hawataki kupisha eneo la kanisa, siku yakitokea na huko maafa tukutane hapa kupozana na kulaumiana, sooo fooooooool
Juu ya kanisa katoliki au CCM kuchukua maamuzi ya kuua au ugomvi wa kuumizana ,nakataa kabisa. Kama ni wewe umepanga kufanya fujo kulisingizia kanisa au CCM na kuja kusema niliwaambia ,acha wazo hilo.
 
Mkuu kuwa na hekima basi, mbona unakuwa Kama mtoto mdogo usiyejua kitu? Juzi tu ukuta wa jengo la darasa ulibomolewa je hiyo siyo alarm ya kuwa mgogoro huo unahitaji utatuzi wa haraka. Askofu alisema endapo CCM hawataondoa shule Yao hapo atawatangazia waumini kuwa chama kimekuwa adui wao nao watajua namna ya kudeal nao. Wakeup guys!
 
Siku zote napinga suala la kumiliki silaha, ukiwa na silaha za moto unakuwa ni mwenye kijiamini kupita maelezo, hapo hakimu asingekuwa na silaha pengine wangeweza kuzungumza na yakaisha.

Jambo lingine, serikali iangalie hawa watu waliopewa Mamlaka ya uamuzi. Hakimu mzima umeshindwa kwenye kesi badala ukate rufaa unalazimishia mabavu, yawezekana hata hukumu zake ni za kijanjajanja.

Wananchi waliotenda jinai hiyo pia ni wahalifu. Kuua mtu sio suluhisho ila ni kuongeza ukubwa wa tatizo. Hao wahalifu wasakwe.

Yote kwa yote , Mungu azipumzishe roho za Marehemu mahali pema peponi na majeruhi awape uponyaji wa haraka.
Punguza ujuaji na uache dhihaka kwa Mungu. Unaambiwa alikuwa anaroga alafu hapo hapo unamshauri Mungu awaweke mahala pema. Umekariri au?
 
Back
Top Bottom