Soko kuu lililopo katika mji mdogo wa Tunduma uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambia linateketea kwa moto hivi sasa. Chanzo cha moto hakijajulikana, ila inasemekana kulikuwa na matatizo ya umeume mchana wa leo, na watu wengi wa hapo sokoni walikuwa wamewasha majenereta. Juhudi za kuuzima zinaendelea, na hadi jirani wa Zambia wanasaidia kuuzima.
Source: Festo Sikagonamo wa ITV