Mbele ya Urusi, Marekani lazima ale kona!

Mbele ya Urusi, Marekani lazima ale kona!

wewe baki na yesu sisi tunataka wapasuane siria ni waarabu walishawaonea babu zetu,hivyo basi wauane upesi
 
Hata mimi nashangaa....PUTIN siyo mfupi kiasi cha kuitwa mbilikimo...dah...western propaganda nyingine ni shiiiiiida
Wala siyo western prop,ni yeye tu mleta mada.Kwa hili west hawahusiki.
 
Point kubwa ni kuwa Marekani hata siku moja hataki vita ipigwe kwenye ardhi yake.

Sasa na vitisho vya Putin na Kiduku kuwa na silaha zenye zenye uwezo wa kupiga US mainland within minutes (Intercontinental Balistic Missiles) na zenye uwezo wa kukwepa radar detection ndio jambo ambalo linawakosesha raha na kufyata mkia.

Pia madai ya Kiduku kuwa na Nuclear war heads na ICBMs kunawanyima usingizi US maana wanajua wakilianzisha tu jamaa hawatajibizana nao kwenye uwanja wa mapambano bali wata focus US mainland ndio pawe uwanja wa mapambano na pawe totally devastated.

Ni raisi gani anaweza kutake risk zote hizo? Hakuna labda awe taahira.
Tambua jambo moja kubwa Kiduku anapewa tekinolojia na mrusi, na kawekwa pale kwa kazi maalumu, kama warusi walivyofanya cuba ndicho walichokifanya korea kaskazin. Kumbuka kambi kubwa za marekani zilizopo asia zipo korea kusini na japan, hivyo kiduku kazi yake kubwa endapo vita itatokea between russia na marekani la kwanza analotakiwa fanya ni kuhakikisha korea kusini na japan zinakuwa majivu within a second
 
Mashambulizi ya kijeshi ni mbinu za kumpoteza adui. Trump katoa taadhali, majeshi ya Syria, Iran na Urusi wapo makini kwa sasa hivi. Zikipita siku Majeshi yatajisahau huo ndo wakati wa America kutuma Kombora. Mfano nzuri kutoka kwa Israel Mashambulizi yao huwa wanatulia utasikia alfajili uwanja wa ndege umeshambuliwa
Hakuna cha mbinu za kumpoteza adui wala nini. Kaingia baridi baada ya kuona Putin hatishiki!!! Mwenyewe kalazimika kubadili gia angani!
 
Nina uhakika SAA hii Trump atakuwa anajutia mkwara wake wa kuitishia urusi kuwa ijiandae maana ataishambulia Syria kwa makombora mazuri, mapya na janja!! (nice, new and smart)). Saa hii anajiuliza nisiposhambulia kama nilivyoahidi dunia yote wataniona mwoga! na nikishambulia maana yake nitegemee urusi kujibu mapigo kwa nguvu zote kama walivyoonya!!
Kitakachotokea ni marekani kutafuta upenyo wa kula kona kistaarabu kwa kuja na ngonjera hii: "Tumethibitisha kuwa hakuna silaha za kemikali alizotumia Syria kwa hiyo ule mpango wa kuishambulia tumeusitisha". Kwa namna hiyo atakuwa amekula kona kiaina!!!
Mshirika wake namba moja uingereza keshaonyesha dalili za kuingia mitini tayari na amesema itabidi marekani iwe na uthibitisho kwanza!!
Timu trump jiandaeni kisaikologia kumwona kinara wenu akila kona!! Kwanza alisema masaa 48 na yameisha!! Mdogo wake ufaransa akasema masaa 72 watakuwa wameshambulia nayo yanaishia!!! Timu trump jiandaeni kwa fedheha!!! Huwezi kumtishia nyau Putin!!
Kona mbaya kabisa ya kufa MTU!!!cheza na Urusi aiseh.!!!?
 
Raia wana betting utadhani wanao kufa siyo binadamu
 
Wala siyo western prop,ni yeye tu mleta mada.Kwa hili west hawahusiki.

Uko sahihi....ila anafanya propaganda kwa niaba ya western....halafu baadhi ya vyombo vya habari vya west humita PUTIN kuwa ni diminutive ...
 
Huu uzi nahisi umetolewa na kijana wa darasa la saba, tena failure. Haelewi kabisa implications za vita ila anasumbuliwa tu na ushabiki maandazi.

Majuzi tu kwenye ile suspected chemical attack ya awali mbona Syria ilishambuliwa sasa hizo S400 zilienda wapi siku hiyo au hata Israel walipowashambulia majuzi hizo "Sophisticated Air Defense Systems" mbona hazikuzuia shambulizi.

Watanzania wanapenda sana ushabik maandazi. Hao American Military mbona wapo kwenye ardhi ya Syria muda mrefu mbona siku zote hizo wasivurumishwe na The Russian Red Army? Mbona hamfikirii hilo? Kelele ndio nyingi tu humu for nothing.
 
Mashambulizi ya kijeshi ni mbinu za kumpoteza adui. Trump katoa taadhali, majeshi ya Syria, Iran na Urusi wapo makini kwa sasa hivi. Zikipita siku Majeshi yatajisahau huo ndo wakati wa America kutuma Kombora. Mfano nzuri kutoka kwa Israel Mashambulizi yao huwa wanatulia utasikia alfajili uwanja wa ndege umeshambuliwa
Urussi sio Afghanistan mjomba...eti majeshi ya urussi yajisahau hivi unajua unachokisema
 
Back
Top Bottom