Mbele ya Urusi, Marekani lazima ale kona!

Mbele ya Urusi, Marekani lazima ale kona!

Nina uhakika SAA hii Trump atakuwa anajutia mkwara wake wa kuitishia urusi kuwa ijiandae maana ataishambulia Syria kwa makombora mazuri, mapya na janja!! (nice, new and smart)). Saa hii anajiuliza nisiposhambulia kama nilivyoahidi dunia yote wataniona mwoga! na nikishambulia maana yake nitegemee urusi kujibu mapigo kwa nguvu zote kama walivyoonya!!
Kitakachotokea ni marekani kutafuta upenyo wa kula kona kistaarabu kwa kuja na ngonjera hii: "Tumethibitisha kuwa hakuna silaha za kemikali alizotumia Syria kwa hiyo ule mpango wa kuishambulia tumeusitisha". Kwa namna hiyo atakuwa amekula kona kiaina!!!
Mshirika wake namba moja uingereza keshaonyesha dalili za kuingia mitini tayari na amesema itabidi marekani iwe na uthibitisho kwanza!!
Timu trump jiandaeni kisaikologia kumwona kinara wenu akila kona!! Kwanza alisema masaa 48 na yameisha!! Mdogo wake ufaransa akasema masaa 72 watakuwa wameshambulia nayo yanaishia!!! Timu trump jiandaeni kwa fedheha!!! Huwezi kumtishia nyau Putin!!
Kagua pichu mkuu
 
Habari za asubuhi ndugu na marafiki, nadhabu mko njema na mungu anazidi kuwasaidia.

Kwa kweli mimi(nkobhe255) nilikuwa bonge la shabiki kwa udharimu unaofanywa na Marekani kwa baadhi ya mataifa madogo duniani. Marekani alijulikana kama mbabe wa dunia ambaye alikuwa na mamlaka ya kufanya chochote kile na asifanywe chochote kile na yeyote yule including UN. Lakini ubabe wa Marekani kimataifa umefikia mwisho siku hizi za karibuni. Nitatumia mifano ifuatayo:

(1)Mgogoro na N. Korea. Kila mtu alifuatilia juu ya sakata lililotishia kuzuka kwa vita kati ya USA na N. Korea, ilifikia kipindi USA wakapeleka kila aina ya Silaha katika mipaka ya N. Korea. Hapa niliamini huo utakuwa ndo mwisho wa N. Korea. Lakini kila mtu alijionea jinsi USA alipoamua kuyarudisha majeshi yake nyuma baada ya kupima urefu wa maji. Hapa niliumia na nilitumia zaidi ya siku 2 bila kula wala kunywa, mpaka watu wakanishangaa.

(2)Mgogoro wa Ukraine. Kabla Urusi haijainyakua CRIMEA ambalo ni jimbo la UKRAINE lililopo mpakani na Urusi, tuliona jinsi Marekani alivyotishia kusambaratisha utawala wa CREMRINE, Mpaka ikafikia hatua bunge la CONGRESS la Marekani kupitisha mswaada wa kupeleka silaha nzito kule Ukraine, lakini kila mtu anajua kilichotokea, mpaka sasa jimbo hilo la Crimea lilishanyakuliwa na Urusi.

(3)Mgogoro wa Syria. Yaani hapa ndo nimechanganyikiwa kabisa, hii ni baada ya Marekani kuahidi majibu kwa serikali aliyoiita dhalimu duniani ndani ya saa 24 to 48, halafu baadae akatweet eti baada ya saa 72.Chakushangaza ni baada ya haya masaa 72 kuyoyoma ndipo washirika wa Marekani walipoona mambo ni mazito wote wakakacha. Mfano, mpaka mda huu, UK, France na Germany wamegoma kufanya shambulizi la pamoja huko Syria wakishirikiana na Marekani. Kwakweli nimechanganyikiwa kinoma, yaani USA ndo anatufanyia sisi TEAM mawigi hivi? Nimechoka kuumia aisee, sasa lasmi najiunga na TEAM mbilikimo(Putin). Huyu USA amezidiwa na Israel, Israel kamuanzishia ili kumuonyesha njia ila cha kushangaza USA kabweka weeeee mwishowe akarudi nyuma, Pumbavu TEAM Mawigi na HONGERA TEAM Mbilikimo(Putin) kwa ushindi.

MY TAKE.

Ukweli ni kwamba, japo Marekani wana Silaha nyingi na nzito lakini ni waoga kupigana vita, ndo maana wanashindwa kuthubutu chochote, Trump kashindwa kuamrisha tu? Mbona Putin kashayapa makeshi yake yote ruhusa na kujibu mapigo? Kwanini Mawigi kashindwa?

Huu ubabe wa Marekani kila mwaka unaenda unapungua, kijeshi na kiuchumi. Baada ya hili, washirika wengi wa Marekani wataanza kukimbilia Urusi ili kujihakikishia usalama wao baada ya kushindwa kuona msaada wa Marekani. Pia mataifa mengi yaanza kukimbilia China kiuchumi ili kulinda masoko yake ya fedha duniani hapo baadae.

Bye bye Team Mawigi, nadhani teaam Mbilikimo mtanikaribisha.
Pole dogo,ulijidai kujifanya mjuuuuvi
 
km nakuona ulivyojificha
Strikes in Syria did not hit areas near Russian bases: Moscow*.The Russian defence ministry said that none of the rockets launched in the Syria attack entered the zones where Russian air defence systems are protecting facilities, Russianpress agency TASS reported.
 
Sasa Mkuu ulitaka wapitishe huko kwani warusi ndo waliotuhumiwa kutumia hizo chemical weapons kwa Raia?! Hata angekua Mrusi asingethubutu kupiga sehemu alipo US ndo maana hata huko Syria Hawa watu huwa wanawasiliana kwa kila kitu kwamba Leo watapiga wapi ili kuepusha ajali ambazo zinaweza sababisha mgogoro mkubwa baina yao.

Kumbuka Russia ndiye aliyesema kwamba US akirusha kombora kuelekea Syria bhas angetungua makombora na kushambulia sehemu yalipotoka,Je baada ya US na allies wake kushambulia Kuna meli iliyozamishwa?!
 
Walisema watashambulia kama askari wake au vituo vyake vingelengwa! Trump akaingia baridi!
 
Nina uhakika SAA hii Trump atakuwa anajutia mkwara wake wa kuitishia urusi kuwa ijiandae maana ataishambulia Syria kwa makombora mazuri, mapya na janja!! (nice, new and smart)). Saa hii anajiuliza nisiposhambulia kama nilivyoahidi dunia yote wataniona mwoga! na nikishambulia maana yake nitegemee urusi kujibu mapigo kwa nguvu zote kama walivyoonya!!
Kitakachotokea ni marekani kutafuta upenyo wa kula kona kistaarabu kwa kuja na ngonjera hii: "Tumethibitisha kuwa hakuna silaha za kemikali alizotumia Syria kwa hiyo ule mpango wa kuishambulia tumeusitisha". Kwa namna hiyo atakuwa amekula kona kiaina!!!
Mshirika wake namba moja uingereza keshaonyesha dalili za kuingia mitini tayari na amesema itabidi marekani iwe na uthibitisho kwanza!!
Timu trump jiandaeni kisaikologia kumwona kinara wenu akila kona!! Kwanza alisema masaa 48 na yameisha!! Mdogo wake ufaransa akasema masaa 72 watakuwa wameshambulia nayo yanaishia!!! Timu trump jiandaeni kwa fedheha!!! Huwezi kumtishia nyau Putin!!
Mpaka muda huu naona Mrussi ndie kala kona maana ali haidi kushambulia atakae anza mshambulia pamoja na kupiga kule shambulio lilipo toka
Ila watu mpo zzzzzzzziiii kimya mna subiri ajib mapigo wanaume wame tia nanga baharini hamja rusha hata ka grenade!!!!
 
Marekani bila vikwazo na kuomba support kutoka kwa EU ana jipya.......ki ufupi kama inatokea battle ya kueleweka marekani anakaa mapema sana
Hivi unajua marekani anatoa kiasi gani kusupport Nato yeye ndo anatoa asilimia Kubwa marekani haitaji msaada kutandika mtu anajeshi na vifaa vya Karne ijayo
 
Kwa mapanki alikula kona pia!! Alimtishia kwa kuamru kikosi cha meli za kivita ziende huko pwani ya Korea, Kiduku akamwambia zikivuka mstari Fulani nitazizamisha!! Trump akakumbuka jinsi NK ilivyozamisha manoari ya kivita ya Korea kaskazini Mara tu ilipovuka mpaka na kuingia kwenye maji yake akaona heri aibu kuliko fedheha meli zake zikala kona mpaka leo!!!
SAA hii kim kamwalika Trump kwenye mazungumzo kama "wanaume" wawili na si kama mvulana na mwanaume!!
Haya maneno ndio yaliyomfanya Russia akakimbilia UN. Upuuuzi wa kuwaamnini North Korea. Iyo ishu ya kuzamisha chombo weka link, tuamini mbali na apo ni uongo tuuu
 
The US had communicated with Russia ahead of the strikes through the normal procedures of their "deconfliction" hotline, which is used to prevent accidental clashes in a war zone. Trump kampigia magoti Putin kumwomba amruhusu ashambulie kwa masharti kuwa ni shambulizi la Mara moja tu lisilozidi SAA moja na asijichanganye kuingia maeneo yenye silaha za Russia!! Hata hivyo makombora 71 kati ya 103 yamedunguliwa na silaha za kizamani sana za soviet za miaka ya sabini zinazotumiwa na Syria yaani S125!!! Aibu!!!
Toa hiyo takataka yako. Ulikuwepo wakati wanaongea.
 
Toa hiyo takataka yako. Ulikuwepo wakati wanaongea.
Tatizo ni kwamba hufuatilii vyanzo vingi vya habari za kimataifa. Hiyo nimeinukuu wala sijasema mimi. Ndiyo maana shambulio lilikoma baada ya dakika 50 tu. Zaidi ya hapo mzee mzima angevuliwa nguo.
 
Umeshajiuliza ni kwanini shambulizi hilo limefanywa na mataifa matatu makubwa kijeshi? Je nikikuambia kuwa US iliburuzwa na uingereza utanielewa? Uingereza, ufaransa, poland ukrane na uturuki wote hao ndo wanaompa nguvu US, urus hawez kupambana na mataifa yote hayo kwa msaada wa china pekee
 
Haya maneno ndio yaliyomfanya Russia akakimbilia UN. Upuuuzi wa kuwaamnini North Korea. Iyo ishu ya kuzamisha chombo weka link, tuamini mbali na apo ni uongo tuuu
Tatizo watu ujanja wenu unaanzia Jf na kuishia Jf. Hebu ona hapa>
North Korea: 'No apology' for S Korea Cheonan sinking - BBC News
www.bbc.com/news/world-asia-32013750
Mar 24, 2015 - North Korea rejects South Korean calls for an apology over the sinking of a warship, almost five years after the disaster killed 46 sailors.
 
Back
Top Bottom