Wakati mfumo wa vyama vingi unaanzishwa hapa Tanzania, mimi nilikuwa kijana na mpenzi wa vyama vingi. NCCR ilijaa sana watu wa system na hata baadhi ya wanamageuzi walishtuka na kukimbia. Kwa uelewa wangu mdogo, hiki siyo chama cha upinzani. Na ndiyo maana hata kwenye utawala wa awamu ya 4, JK aligawa nafasi moja ya ubunge wa kuteuliwa na kumpa mwenyeketi wa hiki chama. Tangu lini Rais akamteua mpinzani kuwa mbunge tena ukizingatia wapo makada kibao wa CCM ambao wamekosa nafasi.