Mbatia's Endorsement ni Busu la kifo!!

Mbatia's Endorsement ni Busu la kifo!!

Wanachokifanya CCM wanawapa nguvu Vyama vingine kama hivyo vya Nccr,CUF ili Chadema ikigoma mpk tume huru ya uchaguzi ipatikane then CUF,Nccr,Act wataendelea na uchaguzi kama kawaida na kupewa vijimbo viwili vitatu then chadema wakilalamika huko kwny jumuiya za kimataifa CCM itasema mbona wenzao wameshiriki uchaguzi fresh tu.

Inabidi kui counter attack hii strategy ya CCM kwa mbinu za kimedani.

Kwanza sidhani kwamba cdm wanadai tume huru kwa kuwa jumuiya ya kimataifa itahoji. Ila haya ni madai halali tena ya muda mrefu. Hata ccm wanajua fika muundo wa tume hii una walakini, ila kwakuwa msukumo wa kuidai ni mdogo, na baadhi ya vyama vinatumika kuhadaa umma, basi ccm wanaendelea kutumia mwanya huo. Iwapo tume hii itadaiwa kwa nguvu zote haitaepukika bila kujali hivyo vyama kama vitatumika. Ni bora cdm wasishiriki huo uchaguzi kwa kuidai hiyo tume huru ya uchaguzi, miaka mitano ni nini, mbona CUF. ya Maalim ikisusia uchaguzi uliobakwa na sasa muda umeisha bila ccm huko Zanzibar kuwa kwenye uhakika wa kushinda uchaguzi huu? Ni vyema kusimamia madai halali bila kuyumba kwa hizo trick za vyama visivyo na nguvu.
 
Mbatia ni mwepesi kuliko pamba , angekuwa hivyo unavyotaka kutuongopea hapa angesubiri apewe ubunge na UKAWA , na safari hii ndio mwisho wa ubunge wake , labda apewe viti maalum
Ndio anawapukutisha hivyo mdogo mdogo

Nccr inarudi katika viwango vyake vya 1995!
 
Bado sna kufika safari yetu si Mbowe si Mbatia si Lipumba si Maalim Seif si Zitto kabwe sio Magufuli wote wapo kwenye vita kugombea kula Cake ya Taifa...
Hello Jf

Napenda kuandika kupitia JF kutuma salamu kwa Mbatia na kundi lake kuwa hii endorsement yao ni kiss of death!

Kuna taarifa kwamba Mbatia na Lipumba waliyakubali mapendekezo yote ya JIWE bila masharti wala marekebisho isipokua kwa maalim Seif peke yake.

Napenda nimkumbushe Mbatia kwamba akionacho sasa si matakwa ya akina Mbowe au yeyote mwana mageuzi isipokua ni nguvu ya wakati!

Wakati una nguvu kuliko vifaru vya jeshi na zana zote za vita!! Huu wakati ni muafaka kwa wana mageuzi kuvuna walichopanda na si kukimbia chombo na kujitosa kwa CCM!!

CCM kiuhalisia haipo tena isipokua inaning'inia kwenye kamba nyepesi iitwayo DOLA.

Kukimbilia CCM kwa majira haya ni kama kukimbilia kifo!!

Hii task aliyopewa Mbatia kamwe asifikiri atashinda na NCCR kuibuka tena kamwe asifikiri hivyo.

Hii endorsement kwake is a kiss of death na itampoteza mazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG_20200320_223458.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi tusiofungamana na upande wowote ngoja tusubili mtanange, lakini kwa CCM hii ambayo imeonyesha uchapakazi uliotukuka hata kama muwe na tume kama ya kenya (IEBC) kushinda ni ngumu kwa wapinzani.

Tume huru sio kwa ajili ya cdm kuishinda ccm, bali ni mshindi halali kutokana na ridhaa ya wananchi kupatikana na kutangazwa. Huo utendaji wa ccm utaeleweka vizuri iwapo kuna uwanja sawa wa ushindani.
 
Mkuu kinachotafutwa hapo sio Tume huru ili eti upinzani ushinde bali ni kuipa uhalali ushindi wa yeyote yule awe CCM au CHADEMA.
Unajua kipindi wapinzani wanadai mgombea binafsi na tume huru 2014 CCM wengi walikejeli ila shida inakuja pale mwana CCM akikatwa kura za maoni kwa rafu, hata akienda upinzani hana assurance ya kushinda anaanza kuona umuhimu wa tume huru.
Kwahiyo tume huru ikiombwa tusiangalie kwa jicho la kwamba Mbowe au Seif ndio wanataka ushindi bali hata kina Kassim Majaliwa au Makonda wataihitaji 2025!!
Hata sasa hivi hii tume ipo huru.Sababu inatakiwa ifanye kazi kwa mujibu wa katiba ya JMT. Ibara ya 74(7) inasema wazi kuwa tume ya uchaguzi ni chombo huru ambacho kinatakiwa kifanye kazi kwa mujibu wa sheria. Hapa Tanzania uchaguzi unapofanyika kila chama huwa na wakala kuanzia kituo cha kupiga kura,jimboni hadi ngazi ya taifa. Hii ni kwa mujibu wa sheria. Na hata kura zikijumlishwa kuna form anasaini na kubaki na copy. Hivyo by any means necessary muwe na tume kama Iebc au hata hii iliyopo, mtapigwa tu.
 
Mkuu hizo fomu huwa zina msaada kwa. Wagombea ubunge tu ili kujengea hoja kuwa wamechezewa rafu ila kura za Urais hata uwe na fomu zote huwezi kwenda kupinga popote pale zaidi ya kukubali matokeo na ndio maana Hata Maalim Seif licha ya kudai kuibiwa hawezi shitaki popote pale so did Lowassa na hii ni shida ya sheria za uchaguzi.

Narudia tena tume huru sio kwa ajili ya ushindi kwa upinzani bali kujenga uhalali wa uchaguzi. Kumbuka Lowassa alipokua CCM hakuitaka tume huru ya warioba ila alivyokatwa CCM ndio akatambua umuhimu wa tume huru.

Hivyo faida sio kwa CHADEMA maana kweli wanaweza shindwa kama unavyotabiri ila angalau wataweka misingi mzuri wa demokrasia ili hata Kina Majaliwa au Mwigulu wakikatwa CCM wahakikishe ushindi wakihamia hata ACT kipindi hiko!!
 
ACT Wazarendo wameapa lije jua au mvua wao uchaguzi lazima watashiriki. Hawa wanatumika na nani?

Kama umeiangalia vizuri ACT nguvu yake iko Znz, na kule wana uhakika wa kupata viti vya ubunge maana karibia wote walikuwa CUF iliyosusia uchaguzi uliopita, na hakuna uwezekano wa wao kuporwa tena uchaguzi huu, kwani wataamua liwalo na liwe. Zito ni lazima ahakikishe ACT inashiriki uchaguzi kule Zanzibar ili ACT ipate ruzuku, kwa matarajio kuwa akipata ruzuku ya kutosha atajijenga huku bara. Lakini Zito anajua fika kuwa huku bara kura za upinzani ziko kwa washabiki wa cdm. Kuna wakati Zito anajitahidi kuishawishi cdm kwani anajua mtaji wa watu ilio nao cdm, na uelewa wa siasa za upinzani walio nao wanacdm. Lakini tofauti binafsi za Mbowe na Zito ndio zinakuwa kikwazo kwa muungano wa ACT na Cdm.

Zito anajua fika tume hii sio huru, lakini anakosa nguvu ya kuidai kwa nguvu, maana anajua kabisa hata tume ikiwa huru, bado chama chake hakina ushawishi mkubwa huku bara na watakaofaidika ni cdm. Ila anajua akipata nguvu kupitia njia ya Zanzibar, atapata ruzuku itakayompa nguvu ya kujijenga huku bara. Na kwakuwa lengo la dola ni kuiua cdm, basi yeye atatumia mwanya huo na nguvu yake ya ushawishi, kuchota mtaji wa upinzani ambao utakuwa umekosa chama, kwani lengo la Magufuli na dola ni kuiua kabisa cdm.
 
Mkuu hizo fomu huwa zina msaada kwa. Wagombea ubunge tu ili kujengea hoja kuwa wamechezewa rafu ila kura za Urais hata uwe na fomu zote huwezi kwenda kupinga popote pale zaidi ya kukubali matokeo na ndio maana Hata Maalim Seif licha ya kudai kuibiwa hawezi shitaki popote pale so did Lowassa na hii ni shida ya sheria za uchaguzi.

Narudia tena tume huru sio kwa ajili ya ushindi kwa upinzani bali kujenga uhalali wa uchaguzi. Kumbuka Lowassa alipokua CCM hakuitaka tume huru ya warioba ila alivyokatwa CCM ndio akatambua umuhimu wa tume huru.

Hivyo faida sio kwa CHADEMA maana kweli wanaweza shindwa kama unavyotabiri ila angalau wataweka misingi mzuri wa demokrasia ili hata Kina Majaliwa au Mwigulu wakikatwa CCM wahakikishe ushindi wakihamia hata ACT kipindi hiko!!
Ok fine mna tume kama ya kenya Iebc na jamaa anakubalika kama JPM nini kitakusaidia kwenye kura za urais? Jana kunywa kahawa tu chato ni kama amepata kura 30% za urais. Point yangu ni kwamba good derivery of results ndio zinakupa ushindi. Na siasa ni sayansi.
 
Hello Jf

Napenda kuandika kupitia JF kutuma salamu kwa Mbatia na kundi lake kuwa hii endorsement yao ni kiss of death!

Kuna taarifa kwamba Mbatia na Lipumba waliyakubali mapendekezo yote ya JIWE bila masharti wala marekebisho isipokua kwa maalim Seif peke yake.

Napenda nimkumbushe Mbatia kwamba akionacho sasa si matakwa ya akina Mbowe au yeyote mwana mageuzi isipokua ni nguvu ya wakati!

Wakati una nguvu kuliko vifaru vya jeshi na zana zote za vita!! Huu wakati ni muafaka kwa wana mageuzi kuvuna walichopanda na si kukimbia chombo na kujitosa kwa CCM!!

CCM kiuhalisia haipo tena isipokua inaning'inia kwenye kamba nyepesi iitwayo DOLA.

Kukimbilia CCM kwa majira haya ni kama kukimbilia kifo!!

Hii task aliyopewa Mbatia kamwe asifikiri atashinda na NCCR kuibuka tena kamwe asifikiri hivyo.

Hii endorsement kwake is a kiss of death na itampoteza mazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni bavicha na umeandika huku unaumia.
 
Hata sasa hivi hii tume ipo huru.Sababu inatakiwa ifanye kazi kwa mujibu wa katiba ya JMT. Ibara ya 74(7) inasema wazi kuwa tume ya uchaguzi ni chombo huru ambacho kinatakiwa kifanye kazi kwa mujibu wa sheria. Hapa Tanzania uchaguzi unapofanyika kila chama huwa na wakala kuanzia kituo cha kupiga kura,jimboni hadi ngazi ya taifa. Hii ni kwa mujibu wa sheria. Na hata kura zikijumlishwa kuna form anasaini na kubaki na copy. Hivyo by any means necessary muwe na tume kama Iebc au hata hii iliyopo, mtapigwa tu.

Unaongea nini boss, katiba ya nchi hii inasema kuwa nchi yetu ni ujamaa na kujitegemea, je huo ndio uhalisia kwakuwa imeandikwa kwenye katiba? Hii katiba ni ya mwaka 1977, miaka 40+ iliyopita. Haikidhi mahitaji ya sasa kwani mambo mengi yamebadilika kuanzia siasa hadi kizazi. Tuna katiba pendekezwa ambayo tulitoa maoni yetu kuhusu muundo wa tume, rais huyu kaigomea ili atawale kwa katiba yenye mapungufu, ambayo yatamnuufauisha yeye binafsi na chama chake. Ni hivi, tume hii sio huru, hata kama ingekuwa imeandikwa kwenye biblia fullstop.
 
ACT Wazarendo wameapa lije jua au mvua wao uchaguzi lazima watashiriki. Hawa wanatumika na nani?
Hawa wanatumika na Seif. Anajua kuwa; Lazima kura zote za kule Pemba achukue. Hivyo hana chama kingine cha kumpa hio kura ya Pemba.
 
Mkuu kinachotafutwa hapo sio Tume huru ili eti upinzani ushinde bali ni kuipa uhalali ushindi wa yeyote yule awe CCM au CHADEMA.
Unajua kipindi wapinzani wanadai mgombea binafsi na tume huru 2014 CCM wengi walikejeli ila shida inakuja pale mwana CCM akikatwa kura za maoni kwa rafu, hata akienda upinzani hana assurance ya kushinda anaanza kuona umuhimu wa tume huru.
Kwahiyo tume huru ikiombwa tusiangalie kwa jicho la kwamba Mbowe au Seif ndio wanataka ushindi bali hata kina Kassim Majaliwa au Makonda wataihitaji 2025!!
We jamaa kichwa sana, na unaelewa hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok fine mna tume kama ya kenya Iebc na jamaa anakubalika kama JPM nini kitakusaidia kwenye kura za urais? Jana kunywa kahawa tu chato ni kama amepata kura 30% za urais. Point yangu ni kwamba good derivery of results ndio zinakupa ushindi. Na siasa ni sayansi.

Hakuna anayejali Magufuli kushinda hata kwa asilimia 300, tunachotaka ashinde kihalali basi. Huko ulaya Barcelona, Real Madrid nk zinashinda kila mara, lakini inatumika technology ya Video Assistance Referee maarufu kama VAR, ili timu ikishinda ishinde kwa ushindi usioacha shaka. Mbona hatujasikia timu zinazoshinda zikigomea huo mfumo eti kwakuwa timu zao zina uwezo na zitashinda tu? Ni hivi, tunataka tume huru ya uchaguzi, ili mgombea awe ni yule hasa mwenye ridhaa ya wananchi.
 
Unaongea nini boss, katiba ya nchi hii inasema kuwa nchi yetu ni ujamaa na kujitegemea, je huo ndio uhalisia kwakuwa imeandikwa kwenye katiba? Hii katiba ni ya mwaka 1977, miaka 40+ iliyopita. Haikidhi mahitaji ya sasa kwani mambo mengi yamebadilika kuanzia siasa hadi kizazi. Tuna katiba pendekezwa ambayo tulitoa maoni yetu kuhusu muundo wa tume, rais huyu kaigomea ili atawale kwa katiba yenye mapungufu, ambayo yatamnuufauisha yeye binafsi na chama chake. Ni hivi, tume hii sio huru, hata kama ingekuwa imeandikwa kwenye biblia fullstop.
Kwa hiyo unataka kusema JMT ni nchi ya kibepari? Yaani hapa kuna mabeberu ndio wanaingoza hii Tz?
 
Back
Top Bottom