Mbatia: Ajali ya MV NYERERE ni ya kujitakia tu

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia amesema kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika Ziwa Victoria ni ajali ya kujitakia.
Mbatia ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 21, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam, akisema zaidi ya asilimia 96 ya majanga yanasababishwa na wanadamu, asilimia nne tu ndiyo majanga asilia.

Soma Zaidi: Odinga atuma salamu za rambirambi ajali ya MV Nyerere
Mbunge huyo wa Vunjo akizungumzia kiundani kuhusu majanga, alieleza aina tatu za majanga na kubainisha kuwa kuzama kwa meli hiyo jana mchana Septemba 20, 2018, ni janga lililokuwa likijulikana, wahusika walikuwa wakijua.

Amesema Taifa linapopata janga moja kubwa, hutoa elimu ya kujikinga ili janga kama hilo lisijitokeze tena.
“Ukiacha ajali hii ya kivuko, meli za MV Spice Islanders na MV Bukoba ambazo zote zilizama, zilikuwa elimu tosha na hizi ajali za meli kuzama hazikupaswa kutokea tena,” amesema Mbatia.

“Ukikusanya ajali hizi ukiwa na takwimu sahihi za kutosha na rejea ya majanga unaweza kujua jinsi ya kuokoa raia, kulinda raia ili yasitokee tena majanga badala ya kulalamika na kunyoosheana vidole, kushikana mashati.”

Amesema ajali za aina hiyo zinapotokea, wengi huishia kutoa pole jambo ambalo halisaidii.
Amesema iwapo mapendekezo yaliyotolewa na Jaji Robert Kisanga baada ya kutokea kwa ajali ya MV Bukoba mwaka 1996, ufumbuzi wa nini kifanyike inapotokea ajali ya aina hiyo ungekwishapatikana.

Soma Zaidi: Wananchi wahoji kusitishwa kwa muda uokoaji ajali ya MV Nyerere
Mbatia ameshauri kuanzishwa kwa sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwalinda na kuwakinga wananchi.

"Kupanga ni kuchagua, kama walikuwepo wa Chadema walikufa, wa CUF walikufa wa NCCR walikufa, kitengo hicho licha ya kupigiwa kelele hakikuundwa na wanaozungumza ni Polisi, Mkuu wa Mkoa siyo watu maalumu wa maafa wenye elimu ya masuala hayo,” amesema.

"Mara nyingi ninazungumza bungeni kuikumbusha Serikali wajibu wake namba moja wa kulinda raia. Siasa na kubezana kunapoteza maana.”
Mbatia alimtolea mfano mbunge wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi aliyeonya juu ya kivuko hicho kuwa hakikuwa katika hali nzuri, hakuna aliyejali mpaka imetokea ajali hiyo.

Amesema Serikali ilimpa majibu mbunge huyo bungeni lakini haikutoa majibu sahihi, kwamba kama majibu yangetolewa ya kina, ajali hiyo isingetokea.
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
 
Hakuna mtu angependa ajali hiyo itokee,lakini kwenda mmoja kwa mmoja kwenye conclusion mapema hata kabla uchunguzi wakina ni ajali nyingine kwenye akili zetu na midomo yetu.
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Ni sahihi kwangu mimi nisiyejua chochote juu ya mambo ya maji niamini kuwa ile ajali isingeweza kuepukika kama ajali za ndege?
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Je sisi tunafanya jitihada kuzuia ajali?

Vyombo vyetu vya usafiri ni salama kiasi gani?

Vipi mamlaka zinazohusika zinajiandaaje kukabiliana na majanga kabla hayajatokea?

Watu wanaosema hiyo ni ajali tu nadhani uelewa wao upo chini sana.

Hivi huwa watujifunzi miaka yote hii?

Mambo kama haya yakitokea ndiyo utagundua baadhi ya nchi Afrika zipo nyuma sana. Inafiki kipindi hadi wananchi akili zao zimeshaganda wanaona umasikini, majanga na shida ni sawa tu kwao.

Poleni sana
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.

Kwa hiyo unataka kusemaje kuhusiana na ajali ya jana?
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.

Mara nyingi huwa ni uhayawani kulinganisha matatizo ya jirani yako na ya kwako. Kwanini ujifariji eti tu fulani naye anayo ya aina hiyo? We are strange creatures
 
Unataka uchungizi gan wakati mbunge alishasema mapema bungen wakampuuza kwa vile n mpinzani
Kuna watu humu wengi tu wanaoamini kuwa ajali haina kinga. Sasa kuwabadilisha mawazo hawa watu ni kazi kweli kweli ...........!!
 
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia amesema kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika Ziwa Victoria ni ajali ya kujitakia.
Mbatia ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 21, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam, akisema zaidi ya asilimia 96 ya majanga yanasababishwa na wanadamu, asilimia nne tu ndiyo majanga asilia.

Soma Zaidi: Odinga atuma salamu za rambirambi ajali ya MV Nyerere
Mbunge huyo wa Vunjo akizungumzia kiundani kuhusu majanga, alieleza aina tatu za majanga na kubainisha kuwa kuzama kwa meli hiyo jana mchana Septemba 20, 2018, ni janga lililokuwa likijulikana, wahusika walikuwa wakijua.

Amesema Taifa linapopata janga moja kubwa, hutoa elimu ya kujikinga ili janga kama hilo lisijitokeze tena.
“Ukiacha ajali hii ya kivuko, meli za MV Spice Islanders na MV Bukoba ambazo zote zilizama, zilikuwa elimu tosha na hizi ajali za meli kuzama hazikupaswa kutokea tena,” amesema Mbatia.

“Ukikusanya ajali hizi ukiwa na takwimu sahihi za kutosha na rejea ya majanga unaweza kujua jinsi ya kuokoa raia, kulinda raia ili yasitokee tena majanga badala ya kulalamika na kunyoosheana vidole, kushikana mashati.”

Amesema ajali za aina hiyo zinapotokea, wengi huishia kutoa pole jambo ambalo halisaidii.
Amesema iwapo mapendekezo yaliyotolewa na Jaji Robert Kisanga baada ya kutokea kwa ajali ya MV Bukoba mwaka 1996, ufumbuzi wa nini kifanyike inapotokea ajali ya aina hiyo ungekwishapatikana.

Soma Zaidi: Wananchi wahoji kusitishwa kwa muda uokoaji ajali ya MV Nyerere
Mbatia ameshauri kuanzishwa kwa sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwalinda na kuwakinga wananchi.

"Kupanga ni kuchagua, kama walikuwepo wa Chadema walikufa, wa CUF walikufa wa NCCR walikufa, kitengo hicho licha ya kupigiwa kelele hakikuundwa na wanaozungumza ni Polisi, Mkuu wa Mkoa siyo watu maalumu wa maafa wenye elimu ya masuala hayo,” amesema.

"Mara nyingi ninazungumza bungeni kuikumbusha Serikali wajibu wake namba moja wa kulinda raia. Siasa na kubezana kunapoteza maana.”
Mbatia alimtolea mfano mbunge wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi aliyeonya juu ya kivuko hicho kuwa hakikuwa katika hali nzuri, hakuna aliyejali mpaka imetokea ajali hiyo.

Amesema Serikali ilimpa majibu mbunge huyo bungeni lakini haikutoa majibu sahihi, kwamba kama majibu yangetolewa ya kina, ajali hiyo isingetokea.
Yeye mtaalam wa majanga amechukua hatua gani ktk ajali hii? Yupo bize kutoa kuongea na press ili kupata political gain kuliko kwenda field kutumia utaalam wake kusaidia huko? Shame on him!
 
Back
Top Bottom