Mbatia: Ajali ya MV NYERERE ni ya kujitakia tu

Mbatia: Ajali ya MV NYERERE ni ya kujitakia tu

Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Kwa hiyo ingekuwa ni kwa wazungu nao wangesema giza limeingia tunaenda kulala tutaendelea na uokoaji (uopoaji??) kesho siyo?
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Ulitaka ujumbe upi utufikie ikiwa majanga halali ni asilimia nne tu?
 
Yeye mtaalam wa majanga amechukua hatua gani ktk ajali hii? Yupo bize kutoa kuongea na press ili kupata political gain kuliko kwenda field kutumia utaalam wake kusaidia huko? Shame on him!
Ikiwa mbunge husika, kwa mujibu wa Mbatia, aliwahi kulalamikia hiki kuvuko akiwa bungeni , naye Mbatia amekumbusha kwamba kwa ajali za majini mbili bado serikali haijajifunza na kuchukua tahadhari, ulitaka atoe pesa yake mfukoni kurekebisha hayo mapungufu?
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Kweli ww ni mpuuzi,, ndege ndiyo usafiri ulio salama kuliko yote,,,
Sikio la kufa halisikiagi dawa ww
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Ndugu usafiri wa ndege ndio usafiri salama kuliko aina nyingine za usafiri duniani, sababu; Kujifunza kutokana na makosa. Kila ndege zinapoanguka, kuna uchunguzi unafanyika na makosa kuwekwa wazi na kuweka utaratibu wa kuhakikisha hayajirudii. Tulijifunza nini kwenye Mv Bukoba, MV Skagit, MV Spice Islander? Kwanini hata list ya abiria wa hii ferry hakuna?

We need to learn.
 
Mbatia acha siasa katika jambo Kama hili tusiilaumu serekali hii ni ajali kama zilivyo ajali nyingne sio kulaumu kila jambo
 
Yaliyopangwa na Mungu, hakuna binadamu wa kuyazuia. Tumshukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.

Disaster Management act ipo tangu 2015 tatizo kuthibiti majanga siyo hitaji muhimu la Taifa. Several major incidents occurred and could have been an alarm for our preparedness.
1. Have we established Management Rescue Team? It is trained? In this case not even necessary to ask if it is well trained!
2. If National Disaster Management Rescue Team (NDMRT) is available, is it active 24/7?
3. Does NDMRT have well organised Rescue Equipment?
4. Does rescue equipment available and well serviced / checked for readiness 24/7?
5. Does NDMRT planned periodic emergency drills?
6. Does NDMRT conduct periodic emergency drills as a part of training and efficiency checks?

Tuko bize kununua watu… na popularity … These two are main agenda/ top priorities as a nation...NDM is not even among 100 top list if any!
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Watu wengine bwana!! Ajari ngapi za ndege zimetokea kwa uzembe?? Haps kwetu karibia asilimia 90 huwa ni uzembe wa ki binadamu tu!! Sasa ksma kweli kivuko kina uwezo wa kubeba abiria 100,leo wanasema kulikuwa na abiria karibia 400!! Unategemea nini?? Sababu za kitoto eti kilipokaribia kutia nanga abiria wote wakasogea mbele, ndipo kikakosa balance na kupinduka,!!! Kitakuwa kilikuwa na tatizo basi,
 
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia amesema kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika Ziwa Victoria ni ajali ya kujitakia.
Mbatia ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 21, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam, akisema zaidi ya asilimia 96 ya majanga yanasababishwa na wanadamu, asilimia nne tu ndiyo majanga asilia.



Soma Zaidi: Odinga atuma salamu za rambirambi ajali ya MV Nyerere
Mbunge huyo wa Vunjo akizungumzia kiundani kuhusu majanga, alieleza aina tatu za majanga na kubainisha kuwa kuzama kwa meli hiyo jana mchana Septemba 20, 2018, ni janga lililokuwa likijulikana, wahusika walikuwa wakijua.



Amesema Taifa linapopata janga moja kubwa, hutoa elimu ya kujikinga ili janga kama hilo lisijitokeze tena.
“Ukiacha ajali hii ya kivuko, meli za MV Spice Islanders na MV Bukoba ambazo zote zilizama, zilikuwa elimu tosha na hizi ajali za meli kuzama hazikupaswa kutokea tena,” amesema Mbatia.



“Ukikusanya ajali hizi ukiwa na takwimu sahihi za kutosha na rejea ya majanga unaweza kujua jinsi ya kuokoa raia, kulinda raia ili yasitokee tena majanga badala ya kulalamika na kunyoosheana vidole, kushikana mashati.”



Amesema ajali za aina hiyo zinapotokea, wengi huishia kutoa pole jambo ambalo halisaidii.
Amesema iwapo mapendekezo yaliyotolewa na Jaji Robert Kisanga baada ya kutokea kwa ajali ya MV Bukoba mwaka 1996, ufumbuzi wa nini kifanyike inapotokea ajali ya aina hiyo ungekwishapatikana.



Soma Zaidi: Wananchi wahoji kusitishwa kwa muda uokoaji ajali ya MV Nyerere
Mbatia ameshauri kuanzishwa kwa sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwalinda na kuwakinga wananchi.



"Kupanga ni kuchagua, kama walikuwepo wa Chadema walikufa, wa CUF walikufa wa NCCR walikufa, kitengo hicho licha ya kupigiwa kelele hakikuundwa na wanaozungumza ni Polisi, Mkuu wa Mkoa siyo watu maalumu wa maafa wenye elimu ya masuala hayo,” amesema.



"Mara nyingi ninazungumza bungeni kuikumbusha Serikali wajibu wake namba moja wa kulinda raia. Siasa na kubezana kunapoteza maana.”
Mbatia alimtolea mfano mbunge wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi aliyeonya juu ya kivuko hicho kuwa hakikuwa katika hali nzuri, hakuna aliyejali mpaka imetokea ajali hiyo.



Amesema Serikali ilimpa majibu mbunge huyo bungeni lakini haikutoa majibu sahihi, kwamba kama majibu yangetolewa ya kina, ajali hiyo isingetokea.

Naona Mbatia baada ya kupotea kabisa katika ramani ' Ajali ' ya Mwanza imemrudisha katika mstari na sasa ni mbele kwa mbele!
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Sasa hata vikosi vya uokoaji navyo tuseme na wazungu walianza kudondoka na ndsge tangu enzk hizo. Tuache visingizio kuna mahala najisikia nichukue kiboko niwapige wanasiasa
 
Hakuna mtu angependa ajali hiyo itokee,lakini kwenda mmoja kwa mmoja kwenye conclusion mapema hata kabla uchunguzi wakina ni ajali nyingine kwenye akili zetu na midomo yetu.
Sasa unataka uchunguzi gani wakati watu tumezoea magumashi, tuache kucheza na maisha ya watu. Ili swala la hicho kivuko liliongelewa sana lkn kwa vile ilikuwa inatoka upinzani wakapuuzwa. "Yaani upinge bajeti yangu arafu uniombe maendereo?" Ndipo tulipofikia hapa.
 
Ikiwa mbunge husika, kwa mujibu wa Mbatia, aliwahi kulalamikia hiki kuvuko akiwa bungeni , naye Mbatia amekumbusha kwamba kwa ajali za majini mbili bado serikali haijajifunza na kuchukua tahadhari, ulitaka atoe pesa yake mfukoni kurekebisha hayo mapungufu?
Kwa hiyo amezira kwenda kusaidia watu field kwa kitu alichosomea? Mwisho wa siku nafikiri deep down anafurahi maana anapata fursa kuongea kuhusu fani yake. Kibaya ni anapiga porojo tu bila action.
 
Wazungu wameanza kudondoka na ndege zaidi ya miaka mia iliyopita. Ila mpaka leo hawajaweza kufanya usafiri wa anga uwe accident free...
In the end of the day, hakuna anayeweza kuzuia ajali kwa asilimia mia. Tunachofanya ni kuminimize impact ya ajali na kupunguza kabisa uwezekano wa kutokea ajali.
Mmh!,mulemule[emoji106]
 
Back
Top Bottom