Mbashara J2: Kutoka kanisa la Mzee wa Upako, Ubungo

Hivi ni nani anauyerasimisha maneno ya kiarabu kuwa kiswahili karne hii? hayo yaliyopo yanatutosha kwani yalitokea katika karne za giza , kwani walishindwa kutohoa kutoka kabila lolote la kiasili?
Sahihi kabisa mkuu, Tanzania si nchi ya kiarabu sasa kwanini tuchukue sana maneno toka huko, hayo ya nyuma yalitokea kutokana na mazingira ya wakati huo. Binafsi hilo neno silipendi kabisa, sina namna tu ya kulikataa, lakini "msema kweli ni mpenzi wa Mungu " silipendi.
 
Pasuka...!!
 
Anasema hakubali kuzoewa haraka haraka.

Usikubali kupewa lifti na usiyemfahamu.

Hata ukipewa lifti na rafiki yako panda garini ila usicheke cheke.

Haloooo
Waumini wanajibu 'halooo'
 
Ni mdadisi sana anafahamu hadi "kamatia chini"

Anaongelea "zitakuja nyakati za hatari"

Wanaume wanavaa hereni na kusuka

Zamani si sasa. Maudhui na ujumbe nyimbo za zamank na sasa ni tofauti.

Nyakati mbaya zimekuja.
 
Aisee kumbe huyu mzee naye huwa anaonjaonja kidogo, kwa hiyo alionja ili akawatukane majirani zake, daaah mpaka nije nimuamini tena mimi, marafiki zangu, Ndugu zangu na familia yangu itachukua muda sana
Nduguyangu uonjali wake mm naona toomuch...maana huenda castle,castle lite,safari,pulsner ,kilimanjaro,zilidunda..kuhamia bapa bila kutanguliza hizo naokama haiwezekani..huyu mzoefutu!
 
Hakuna mkamilifu hapa duniani,hata ukiwa mtumishi haimaanishi umeuvua ubinadamu tusiwahukumu maana nawenyewe ni binadamu kama sisi kama isivyo rahisi sisi waumini kuzishinda dhambi basi na wao ni hivyohivyo tena wao zaidi maana wana majaribu sana na shetani anawawinda sana so kama una hofu ya Mungu ni vyema kuwaombea watumishi wa Mungu na Mungu atakubariki maana utakuwa umegusa moyo wa Mungu,kinyume chake basi ni kugusa mboni ya jicho lake.



Hata Yakobo alipokutana na malaika,alipomng'ang'ania ambariki,alimshinda ila aliteguliwa mguu showing kwamba bado alikuwa dhaifu mbele za Mungu,binafsi hata nikinung'unika juu ya viongozi wangu wa dini rohoni naambiwaga kutubu,kikubwa ni kuwaombea tu.
 
Kwa haya mahubiri ya sa hivi Shigongo atalipwa hela zake. Amezungumzia umuhimu wa kulipa deni. Kwamba usipolipa deni unaumiza anayekudai.
 
Mkuu mbona unawalisha members matango pori?? Nilidhani update za humu ni za live coverage?
Unayo update wewe si live but recorded
 
meongelea chukizo la uharibifu askofu uingereza shoga. Kaongelea Utabiri wa TB joshua kutotimia. Kwa nini hajaomba msamaha na kuendelea kujifanya mjanja huku wengine wajinga.
 
 

Amen! Amem Sista..
Hata mfalme Daudi aliyetumiwa na Mungu kumjengea hekalu takatifu aliteleza dhambini, Mfalme Solomon kiongozi wa taifa teule aliteleza dhambini, Petro aliyeawekwa kiongozi wa mitume mingine alimkana yesu kwahiyo si jambo la ajabu Lusekelo akiteleza pia..

Ila dada kwenye ishu ya kuwaombea mimi simo, am not religious hata kidogo na wala sio mtu wa imani.. Kwahiyo jitahidi sista kuwaombea.. Mimi nawafuatilia tu kwa reasons zangu nyingine!
 

Kanisani tunajua ni sehemu au mahala ambapo Waumini wanatakiwa kuwa na ' furaha ' na ' nyuso ' za ' bashasha ' kabisa ili kuweza kumkaribisha Roho Mtakatifu na kuonyesha Upendo wao lakini katika hiyo picha hapo nawaona hao ' Waumini ' karibia wengi wao wana ' nyuso ' za ' Hasira ' na kutaka ' kupovuka '. Je kwa hali hiyo ' maombi ' yao ya leo Mwenyezi Mungu atayakubali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…