Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,137
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, amelalamika kubaguliwa katika mapokezi ya ndege mpya, Boeing 787-8 Dreamliner, ambapo wachungaji wengine walipewa nafasi ya kusema chochote na kuiombea ndege hiyo lakini yeye akabaguliwa.
Mzee wa Upako amejitapa kwamba mvua iliyonyesha siku hiyo, ilikuwa ni ufunuo wa Mungu kuonesha jinsi yeye alivyobarikiwa kwani eneo alilokaa yeye tu, ndiyo mvua haikufika na kusababisha viongozi wengine kukimbilia ili kukaa naye.
Akazidi kufunguka kwamba watu wanamu-ignore sana na wanasubiri siku atakapokufa ndiyo waje kutoa ushuhuda wa jinsi alivyokuwa na upako mtakatifu.