Mbasha, Flora wasaka suluhu kurudiana

Mbasha, Flora wasaka suluhu kurudiana

Hapo Mkuu umenikumbusha wimbo mmoja hiv........ Sikumbuki ni Bend ipi waliimba.

Upo hivi:

".......Nilikueleza tokea mwanzo tunapofarakana kashfa haifai.....umenikashfu hadharani tulipoasiana... umenisimanga kwa watuuuu, leo tupo pamoja, aibu sasa ni ya nani kama siyo yako na yangu; naomba jibu kwakoooo.....naomba jibu kwakooo.................."

Nimeupenda sana wimbo huu kutokana na tukio hili la Mbasha.

HONGERAKWA MTUNZI NA WAIMBAJI WA WIMBO HUU.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
Kweli muziki ni kila kitu ndio kiasi hutufanya kukumbuka yale yanayoimbwa na matukio yanayotupata kila siku na hata Plato na mishemishe zake zote za kisomi alisema "muziki huifanya nafsi kuelea angani, muziki ni mabawa ya akili ambayo husafirisha hisi na kutoa faraja kwa kila mwanadamu"
 
hii ni biblia ya wapi mnayoisoma nusunusu kutetea ujinga? hebu tujibu na yesu aliyeruhusu talaka ni yesu wa magomeni?

na hiyo talaka aliruhusu katika mazingira yapi? Mungu anachukia kuachana. mm naamini sisi sote hatuna ukweli wa hiyo issue tunahisi na kutoa hukumu tu!
 
Haina makombo hiyo irudishe tu nyumbani yaani harua. Hata hivyo sijui atafanyaje maana li Flora nimenogewa na michango ya kanisha. Akiishiwa pesa analianzisha apate 10m.
 
Hapo Mkuu umenikumbusha wimbo mmoja hiv........ Sikumbuki ni Bend ipi waliimba.

Upo hivi:

".......Nilikueleza tokea mwanzo tunapofarakana kashfa haifai.....umenikashfu hadharani tulipoasiana... umenisimanga kwa watuuuu, leo tupo pamoja, aibu sasa ni ya nani kama siyo yako na yangu; naomba jibu kwakoooo.....naomba jibu kwakooo.................."

Nimeupenda sana wimbo huu kutokana na tukio hili la Mbasha.

HONGERAKWA MTUNZI NA WAIMBAJI WA WIMBO HUU.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
Kweli muziki ni kila kitu ndio kiasi hutufanya kukumbuka yale yanayoimbwa na matukio yanayotupata kila siku na hata Plato na mishemishe zake zote za kisomi alisema "muziki huifanya nafsi kuelea angani, muziki ni mabawa ya akili ambayo husafirisha hisi na kutoa faraja kwa kila mwanadamu"
 
Jamaa akirudiana naye atakua ------ sana.
Kama mazingira yanaruhusu wakati mwingine unapiga moyo konde unaurudia mzigo maana ni heri uliegombana nae maana kuna uwezekano wa kujirekebisha though kwa sie wanaume wa kibantu ni ngumu kumeza kutokana na makuzi yetu
 
aisee jamaa ana moyo...wife kagongwa nje na nabii, kataka kumpeleka jela miaka 30...yupo tayari kurudiana nae! jamaa jasiri!
 
Ni ukweli kuwa kila ndoa ina misukosuko yake. Kinachowakuta Mbasha na Flora ni boat ile ile iliyowabeba wanandoa wengine baadhi. Ugomvi wa wanandao humalizwa na wanandoa humalizwa na wanandoa wenyewe. Kuongeza baadhi ya hao mnaowaita wasuluishi ni kudanganya nafsi zenu. Wakae wao wawili wamalize yao!

Kinachotokea hapa nafikiri sasa ni kufufua majina baada ya kutokuwa kwenye vichwa vya habari kwa kitambo sasa! Wasanii wengi hujaribu kurudi kwenye headings hata kwa njia chafu!
 
Kuna kila dalili kwamba mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili nchini, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha wanatamani kurudiana, baada ya kuwapo mgogoro katika uhusiano wao wa ndoa, ulioingia katika vyombo vya habari yapata mwezi mmoja sasa.

Kwa nyakati tofauti jana, kila mmoja wao alimwambia mwandishi wetu kwamba yupo tayari kurudiana na mwenzake, hatua ambayo inaweza kuondoa mgogoro huo ambao umefifisha taswira yao ya kiutumishi.

Akizungumza nyumbani kwake Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Mbasha alisema ameshamsamehe mkewe na kwamba anamsubiri muda wowote arudi nyumbani kusuluhisha mgogoro wao.

“Nawapenda Watanzania wote wazidi kutuombea ili mimi na mke wangu turudiane.”

Kauli hiyo ni sawa na ile aliyoitoa Flora wiki iliyopita pale aliposema: “Ninawaomba Watanzania waendelee kuniombea ili niweze kushinda majaribu haya, kilichotokea ni sehemu tu ya kupimwa imani yangu”.

Jana, Flora alirudia kauli hiyo kupitia kwa wakili wake, Addo Mwasongwe ambaye alisema mwimbaji huyo yupo tayari kukutana na mumewe na ndugu ili waondoe tofauti zao.

Maelezo ya Mbasha

Kwa upande wake Mbasha alisema: “Mi namwomba Flora ajishushe akubali, aje home (nyumbani) tuyamalize na maisha yaendelee. Yeye ni mke wangu namtaka. Kama ananipenda arudi, tuite wazazi tutatue mgogoro huu.”

Aliongeza kuwa hakuna binadamu yeyote asiyesamehewa na kwamba kilichotokea katika ndoa yao ni sehemu ya maisha ambayo wengi hupitia.

“Siku zote naamini tunachotakiwa ni kujenga na siyo kubomoa… Flora asing’ang’anie kwa watu arudi hapa… apige hodi… ‘mume wangu’ nimerudi …na mimi nitampokea tuendelee kulea watoto.”

Mbasha anakabiliwa na tuhuma za kumbaka shemejiye wa miaka 17 na kesi yake inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na sasa yupo nje kwa dhamana.

Tunawaombea kumbukeni ni nyie wawili tu na Mungu wenu mlio na suluhu ya tatizo lenu
 
Back
Top Bottom