Mbasha, Flora wasaka suluhu kurudiana

Mbasha, Flora wasaka suluhu kurudiana

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Kuna kila dalili kwamba mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili nchini, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha wanatamani kurudiana, baada ya kuwapo mgogoro katika uhusiano wao wa ndoa, ulioingia katika vyombo vya habari yapata mwezi mmoja sasa.

Kwa nyakati tofauti jana, kila mmoja wao alimwambia mwandishi wetu kwamba yupo tayari kurudiana na mwenzake, hatua ambayo inaweza kuondoa mgogoro huo ambao umefifisha taswira yao ya kiutumishi.

Akizungumza nyumbani kwake Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Mbasha alisema ameshamsamehe mkewe na kwamba anamsubiri muda wowote arudi nyumbani kusuluhisha mgogoro wao.

“Nawapenda Watanzania wote wazidi kutuombea ili mimi na mke wangu turudiane.”

Kauli hiyo ni sawa na ile aliyoitoa Flora wiki iliyopita pale aliposema: “Ninawaomba Watanzania waendelee kuniombea ili niweze kushinda majaribu haya, kilichotokea ni sehemu tu ya kupimwa imani yangu”.

Jana, Flora alirudia kauli hiyo kupitia kwa wakili wake, Addo Mwasongwe ambaye alisema mwimbaji huyo yupo tayari kukutana na mumewe na ndugu ili waondoe tofauti zao.

Maelezo ya Mbasha

Kwa upande wake Mbasha alisema: “Mi namwomba Flora ajishushe akubali, aje home (nyumbani) tuyamalize na maisha yaendelee. Yeye ni mke wangu namtaka. Kama ananipenda arudi, tuite wazazi tutatue mgogoro huu.”

Aliongeza kuwa hakuna binadamu yeyote asiyesamehewa na kwamba kilichotokea katika ndoa yao ni sehemu ya maisha ambayo wengi hupitia.

“Siku zote naamini tunachotakiwa ni kujenga na siyo kubomoa… Flora asing’ang’anie kwa watu arudi hapa… apige hodi… ‘mume wangu’ nimerudi …na mimi nitampokea tuendelee kulea watoto.”

Mbasha anakabiliwa na tuhuma za kumbaka shemejiye wa miaka 17 na kesi yake inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na sasa yupo nje kwa dhamana.
 
Acheni uzushi nyie, inamaana nyie mnafurahi sana mbasha kuish maisha hayo, inamana nyie hamjawahi kuvutana na vidosho vyenu bhana, mnashangaa nini. Acheni hizo nyie
 
Acheni uzushi nyie, inamaana nyie mnafurahi sana mbasha kuish maisha hayo, inamana nyie hamjawahi kuvutana na vidosho vyenu bhana, mnashangaa nini. Acheni hizo nyie

samahan mkuu unaongea na nani? unaposema 'nyie' unakosea
 
Flora hafai kua mke tena labda suluhu ya kugawa kidogo walichonacho lakini sio ndoa tena.
 
Eti hamtaki warudiane, hu hu watu wanafiki sana
 
Mbasha kama ana akili arudiane nae kimaslahi zaidi..lakn yule syo mke mamaae keshatombekaaaaaaaa weeeee kaona sasa airdishe nyumbani khaaaa
 
mimi naomba warudiane,halafu waanzishe makongamano ya vijana ,wanandoa.ili kufundisha wanandoa jinsi ya kushinda vikwazo katika ndoa,maana waliyopitia wameyashinda.Warudiane wamwaibishe Shetani
 
Back
Top Bottom